Serikali ya Tanzania inafanya "Cultural genocide" Ngorongoro

Serikali ya Tanzania inafanya "Cultural genocide" Ngorongoro

Mto Songwe

JF-Expert Member
Joined
Jul 17, 2023
Posts
6,683
Reaction score
14,060
Ni huzuni lakini inabidi tukubaliane na ukweli kuwa tumekubali kuwa kimya ili serikali iendeleze operation yake ya "cultural genocide" Ngorongoro.

Wazungu kutoka ulaya wakati wanafika bara la America walikuta wakazi wa pale walio pingana nao kwa ubabe wa kifala na kipuuzi wazungu wale waliamua kufanya ushenzi mmoja mkubwa ambao mpaka leo ni historia mbaya ya America wale wazungu waliamua kuangamiza wakazi wa pale kwa kuwaua na kuua tamaduni zao kwa kiasi kikubwa sana.

Pia Wazungu waliofika Botswana nao walifanya cultural genocide kubwa kwa wakati ule same kwa Australia na sehemu mbalimbali za dunia.

Cultural genocide ina historia ndefu hapa duniani kwa jamii ngeni kuangamiza kabisa jamii asili kwa namna mbalimbali.

Operation inayo endelea Ngorongoro dhidi ya jamii ya wamasai ni cultural genocide katika hii miaka ya sasa.

Kama miaka ya sasa kungekuwa hakuna mapinduzi makubwa ya kiteknolojia kama kipindi wazungu wa ulaya wanafika marekani basi serikali ya Tanzania ingeweza kuangamiza maasia wote kabisa tushukuru teknolojia kwa kiasi chake inasaidia kuweka wazi hata udogo wake.

Viongozi wa serikali ya Tanzania niwaulize swali moja . Ngorongoro pangekuwa ndio kwenu na wale wamasai ndio ndugu zako na umasai ndio urithi wako uliobaki hii cultural genocide mgefanya ?

Leo hii kuna Watanzania(Watanganyika) wanaishi kama wakimbizi katika ardhi yao ya asili kisa maamuzi ya kipuuzi ya watu wachache, ni kipi kinacho shindikana wamasai wakaishi vyema pale Ngorongoro kuliko hii cultural genocide kuendelea ?

Tunapo lalamika wazungu waliangamiza babu na bibi zetu na tamaduni zetu tunasahau nasi pia tuna rudia makosa yale yale tunao lalamikia wao kututendea sisi nasi tuna tendeana wenyewe kwa wenyewe.

Cultural genocide ina matokeo mengi negative kwa maisha ya miaka mingi ijayo historia ya dunia imekwisha tuonesha hilo kwa matukio ya kale.

Kiburi, dharau, kutokusikiliza, kutokujali sio sifa za viongozi bora bali manyang'au pekee.

F3k78Z8a0AAldWM.jpeg
 
Kinachofanyika Ngorongoro ni Uangamizaji wa watu wa Maasai.

Tamaduni zao zimekuwa zikilawitiwa taratibu na Wafia dini na Vibaraka wao.

Tusimumunye maneno, yanayoendelea kwa wenzetu Wamasai, Watanzania na ndugu zetu kabisaaaa ni Genocide.

Serikali ya Tanzania Ilaaniwe kwa hili.
 
Hakika
 
Kwani sheria inayoruhusu uthamini wa mali kufanyika kisha wahusika kulipwa fidia kwa maeneo na mali zao zilizopo kwenye maeneo yao kama vile nyumba, miti, mashamba n.k. wewe unaionaje
Kulipwa fidia kwa ajili ya nini ?
 
Kinachofanyika Ngorongoro ni Uangamizaji wa watu wa Maasai.

Tamaduni zao zimekuwa zikilawitiwa taratibu na Wafia dini na Vibaraka wao.

Tusimumunye maneno, yanayoendelea kwa wenzetu Wamasai, Watanzania na ndugu zetu kabisaaaa ni Genocide.

Serikali ya Tanzania Ilaaniwe kwa hili.
Mbona watu wengi walihamishwa kupisha ardhi itwaliwe kwa ajili ya maendeleo sasa huko Ngorongoro kwa nini wasihame.
 
Mbona watu wengi walihamishwa kupisha ardhi itwaliwe kwa ajili ya maendeleo sasa huko Ngorongoro kwa nini wasihame.
Kwenu kuna Maendeleo?

Mbona weye Usiwapishe Serikali ifanye hayo "maendeleo" kwenu? au muwapishe Wamasai waje kwenu. Mfyuuuuuuuuuuu
 
Back
Top Bottom