Tuko karne ya 21 sasa, hao wamasai wanataka elimu, huduma zingine za kijamii na maendeleo pia. Haiwezekani wakaachwa kuja kuonwa na kupigwa picha na watalii na kushi porini na wanyama.
Hizo mbuga ni hifadhi na zinaleta pesa nyingi za kigeni kwa taifa. Wamasai wanaongezeka na wanahitaji huduma ambazo zikijengwa ndani ya hifadhi zitaharibu lengo la hifadhi. Kwa hiyo ni kuwatafatutie eneo lingine waishi.
Makabila mengi hapa nchini yamepisha au yametoa ardhi zao kwa ajili ya miradi yenye maslahi ya taifa lote.
Wakara walihamishwa kutoka kisiwa cha ukara na kupelekwa Uzinza ambako wamenufaika zaidi.
Wamasai pia wanahitaji fursa za maebdeleo kwa hiyo lazima watoke kwenye mbuga.