Serikali ya Tanzania inavyoshikilia uchumi wa Zanzibar

Serikali ya Tanzania inavyoshikilia uchumi wa Zanzibar

Tangu mama aukwae urais kumekuwa na mlipuko wa miradi mbali mbali ZnZ haihitaji fikra kubwa kujua wapi fedha hizo zilipotoka.
Mwinyi hapati ukwasi huo kwa kukodisha visiwa wala hotel za shamba

acha fikra za vijiweni
 
Hizo hisa za Zanzibar zinatokana na Pato gani. Lazima uzalishe kipato/fedha zinazowekwa kwenye BOT government Bond. Ni karafuu, samaki, au utalii au madini au mafuta ?
Mimi nazungumzia hisa sasa wewe unazungumzia kipato. Wapi na wapi?
Kama mnazalisha na kuingizwa BOT mbona kuna bank ya Zanzibar na watumishi wake tofauti na BOT ?
Huu wako ni ulofa uliopitiliza. Hivi BOT na Benki ya Zanzibar ina uhusianaje na mada hii? NBC iko Bara na wafanyakazi wake toauti. Inauhusiano na mada hii? Kumbuka tunajadiliana kwa hoja na sio potojo. JF sio uwanja wa porojo na ujinga.
Hakuna anayetubeba. Hili la kuondoka ndoa nalisubiria kwa hamu ili mutuone tunakuja na bakuli. Tuombe isiwe kinyume chake.
 
Mimi nazungumzia hisa sasa wewe unazungumzia kipato. Wapi na wapi?
Huu wako ni ulofa uliopitiliza. Hivi BOT na Benki ya Zanzibar ina uhusianaje na mada hii? NBC iko Bara na wafanyakazi wake toauti. Inauhusiano na mada hii? Kumbuka tunajadiliana kwa hoja na sio potojo. JF sio uwanja wa porojo na ujinga.
Swali halijajibiwa. Zanzibar anaweka hisa BOT kivipi wakati ana PBZ. Kwa nini asiweke PBZ badala yake aweke BOT ? Na kama ameweka sheria za kifedha yeye kama mwekezaji, lazima zikiiva anapewa hela yake. Unawezaje kuweka hisa bila kuwa na chanzo cha pato. Kinachoanza sio hisa,, ila pato. Ndiyo nikataka kujua tu, chanzo kilichompa Zanzibar fedha/mtaji halafu akaziweka BOT. Bila jibu sahihi, utaishia kutukana matusi yote na huna jibu.
 
Mkuu hapa hatupo kusaidiana. Itoshe tu kujua kwamba Zanzibar ilishatawala huko na haishindwi kujilisha. Nikukumbushe tena, kwamba Zanzibar haigaiwi/haipewi bure chakula kutoka Tanganyika wala nchi nyingine yoyote, bali inanunua kwa pesa zake yenyewe. Au umeshasikia serikali ya Tanganyika inasema inaigaia Zanzibar chakula? Kinyume chake Zanzibar ikiacha kununua bidhaa kutoka Bara, Bara itakuwa imekosa soko muhimu kwa uchumi wake..
Yawezekana, Tanganyika ikakosa pesa eti Zanzibar haijanunua, mahindi na mchele wa Kyela na Igunga ? Vipi kuhusu umeme wa Tanesco umelipwa ? Sipendi Muungano uvunjike, ila ukweli ni kwamba Tanganyika ndiye mlishaji wa Zanzibar. Kuweni na shukrani.
 
Swali halijajibiwa. Zanzibar anaweka hisa BOT kivipi wakati ana PBZ. Kwa nini asiweke PBZ badala yake aweke BOT ?
Niseme tu hujui hata maana ya hisa. Tujaalie ni hivyo unavyojua wewe. Kwani mtu hawezi kuwa na hisa kwenye mradi/uwekezaji zaidi ya mmoja?
 
Na:Abdull Najad Faiq

Zote Tanzania bara na Zanzibar linapokuja jambo ambalo lipo ndani ya orodha ya mambo ya Muungano, huwakilishwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ndio Serikali mama inayopanga sera na dira ya nchi kimataifa

Uchumi wa Zanzibar na Tanzania bara kamwe hauwezi kuwa sawa kutokana na jeografia ya nchi husika.

Uchumi wa Zanzibar zaid unategemea biashara ya huduma ikiwemo Utalii pamoja na Bandari, Zanzibar haina madini wala kilimo cha kuweza kutosheleza zaid ya zao la biashara la Karafuu pamoja na Mwani.

Pia soma: Muungano wa Tanganyika na Zanzibar: Una faida gani na kwa manufaa ya nani?

Kutokana na kwamba Fedha, Sarafu pamoja na Mabank ni katika mambo ya muungano basi bila ya shaka Uchumi wa Zanzibar utategemea sera za kiuchumi za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kupiga hatua kimaendeleo

Upatikanaji wa mikopo kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya kimkakati Zanzibar, kunategemea na dhamana ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Waziri wa Fedha kutokana na kwamba Zanzibar haina uwezo wa kukopa katika taasisi za Kimataifa

Katika njia nyengine ambayo Serikali za nchi duniani huweza kupata mapato kwa ajili ya kuinua uchumi wake ni "misaada na mikopo ya kimataifa" sote tulikua mashahidi jinsi fedha za "Uviko19" zilivyokuja kuibua miradi mbali mbali nchini, ukuaji wa uchumi wa Zanzibar unategemea utashi wa kiongozi wa Tanzania ikiwa ataipatia Zanzibar senti 2 katika kila senti 10 zitakazo kuja kutoka duniani kupitia jina la Tanzania

Uchumi wa Zanzibar unategemea faida inayoweza kupata kupitia majukwaa ya kimataifa mfano Jumuiya ya Afrika Mashariki, Zanzibar nayo pia ni mwanachama wa jumuiya hiyo, kupitia jukwaa hili Zanzibar inaweza kunufaika moja kwa moja kupitia fursa zilizopo ikiwemo masoko ya kibiashara

Zanzibar kama mshirika wa Muungano wa Jamhuri ya Tanzania iliwahi kujiunga na jumuiya ya OIC ili kunufaika kichumi ila iliamuriwa kujitoa na Serikali ya Tanzania na badala yake Serikali ya Jamhuri ikasema itajiunga badala yake sababu Zanzibar si nchi katika nyanja za kimataifa ila hadi leo Tanzania haijajiunga na jumuiya ya OIC

Kuna watu wanasema kwamba jumuiya ya OIC haina maslahi,ipo kisiasa zaid ila kwa maoni yangu wanaotoa hoja za aina hii ndio wapo kisiasa zaid sababu Zanzibar kama ni miongoni mwa mshirika wa Muungano anapaswa kuwa na Uhuru wa kufanya kile anacho kiamini ilimradi anahisi kina maslahi kwake na yeye ndie atakae wajibika kwa kila kitu, kusiwepo na hali ya kuwekeana vikwazo

Sera za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa 70% zinaamua hali ya uchumi wa Zanzibar, sote tunajua kwamba Zanzibar ina idadi ya watu wapatao milioni 2 huku Tanzania bara ikiwa na watu wapatao milioni 59, ikiwa hii leo Mamlaka inayo husiana na "Utoaji wa Leseni za Viwanda Tanzania" ni moja ila muwekezaji aliyewekeza kiwanda Zanzibar akitaka kupeleka bidhaa yake katika soko la Bara inakutana na vikwazo, ila kiwanda hicho hicho kikileta bidhaa katika soko la Zanzibar ni sawa huko ni kuua uchumi wa Zanzibar na kuwaambia wawekezaji kwamba njooni Bara mutakua salama na musiende Zanzibar

Jambo jengine linaloweza kuinua ghafla uchumi wa Zanzibar ni kupatikana kwa usuluhisho kamili juu ya masuala yote ya kifedha baina Zanzibar pamoja na Serikali ya Tanzania bara ikiwemo mgogoro kuhusu hisa za Zanzibar BoT pamoja na Mapato yanayotokana na Account ya Pamoja ya Fedha, mgogoro ambao ni wa muda mrefu, ulioota mizizi na uliobeba Pesa nyingi

Kwahiyo kivyovyote mifumo bora ya ya kiuchumi pamoja na ya Kisera na ya kiutatuzi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndiyo pekee inayoweza kuamua "Hatma ya Uchumi wa Zanzibar" iwe na uchumi wa aina gani.

View attachment 3194842
Bora yenu mna nchi sisi Tanganyika yetu ishapotea
 
Swali hili linaweza kujibiwa vizuri na TANESCO. Mimi hata nikikujibu hutoamini.
Hapa tunaenda vizuri. Miaka zaidi ya 61 ya Muungano ni umri wa mtu aliyestaafu. Bado isemwe wazi, Tanganyika alipoteza na Zanzibar akanufaika. Tudumishe Muungano lakini tuukubali ukweli.
 
Wakati mnaingia kwenye muungano hamkuyajua yote hayo?

Kwa nini msijitoe katika muungano huu unaowatia hasara,?

Zungumzeni huko zanzibar kisha huku mje na msimamo mmoja je mnataka au hamtaki muungano
Kweli; uamuzi ni wao, kama wanaona muungano hauna manufaa wafanye mchakato wa kisiasa na kisheria wajitoe kwa amani kabisa; hakuna sababu ya kugombana, tutabaki kuwa majirani daima maana Tanganyika na Zanzibar hazitahama hapo zilipo; tutaendelea kutembeleana, kuoana, kufanya biashara; kila nchi ikiendesha mambo yake kwa amani bila manung'uniko.
Lila na fila hazitangamani; na mtaka nyingi nasaba, hakosi mingi misiba.
 
  • Thanks
Reactions: RMC
Bado isemwe wazi, Tanganyika alipoteza na Zanzibar akanufaika. Tudumishe Muungano lakini tuukubali ukweli
Sema tu. Hiyo ni haki yako. Nami niseme wazi , Zanzibar ilipoteza na inaendelea kupoteza wakati Tanganyika ananufaika.

Hili la kudumisha muungano limo mikononi mwa Watanganyika.
 
Sema tu. Hiyo ni haki yako. Nami niseme wazi , Zanzibar ilipoteza na inaendelea kupoteza wakati Tanganyika ananufaika.

Hili la kudumisha muungano limo mikononi mwa Watanganyika.
Raisi si mzanzibar anashindwa nini kubadili vifungu vinavyowanyonya wazanzibar?
 
Raisi si mzanzibar anashindwa nini kubadili vifungu vinavyowanyonya wazanzibar?
Mkuu naona umekuja na kasi. Hivi unajua nini majukumu Rais kwa mujibu wa sheria za nchi hii?

Nikuambie tu kwamba jukumu la kutunga sheria hapa nchini liko kwenye bunge. Ni bunge ndo linalotunga sheria. Rais huwa hatungi sheria kwani sio kazi yake. Jifunze hilo. Mkuu jitahidi unapofanya mjadala humu kujifananisha na hadhi ya jukwaa hili. Wenye wanaliita "Jamiiforum. Home of great thinkers". Wenyewe huwa hawakurupuki. Watakucheka watu!
 
Back
Top Bottom