Serikali ya Tanzania inavyoshikilia uchumi wa Zanzibar

Tangu mama aukwae urais kumekuwa na mlipuko wa miradi mbali mbali ZnZ haihitaji fikra kubwa kujua wapi fedha hizo zilipotoka.
Mwinyi hapati ukwasi huo kwa kukodisha visiwa wala hotel za shamba

acha fikra za vijiweni
 
Hizo hisa za Zanzibar zinatokana na Pato gani. Lazima uzalishe kipato/fedha zinazowekwa kwenye BOT government Bond. Ni karafuu, samaki, au utalii au madini au mafuta ?
Mimi nazungumzia hisa sasa wewe unazungumzia kipato. Wapi na wapi?
Kama mnazalisha na kuingizwa BOT mbona kuna bank ya Zanzibar na watumishi wake tofauti na BOT ?
Huu wako ni ulofa uliopitiliza. Hivi BOT na Benki ya Zanzibar ina uhusianaje na mada hii? NBC iko Bara na wafanyakazi wake toauti. Inauhusiano na mada hii? Kumbuka tunajadiliana kwa hoja na sio potojo. JF sio uwanja wa porojo na ujinga.
Hakuna anayetubeba. Hili la kuondoka ndoa nalisubiria kwa hamu ili mutuone tunakuja na bakuli. Tuombe isiwe kinyume chake.
 
Swali halijajibiwa. Zanzibar anaweka hisa BOT kivipi wakati ana PBZ. Kwa nini asiweke PBZ badala yake aweke BOT ? Na kama ameweka sheria za kifedha yeye kama mwekezaji, lazima zikiiva anapewa hela yake. Unawezaje kuweka hisa bila kuwa na chanzo cha pato. Kinachoanza sio hisa,, ila pato. Ndiyo nikataka kujua tu, chanzo kilichompa Zanzibar fedha/mtaji halafu akaziweka BOT. Bila jibu sahihi, utaishia kutukana matusi yote na huna jibu.
 
Yawezekana, Tanganyika ikakosa pesa eti Zanzibar haijanunua, mahindi na mchele wa Kyela na Igunga ? Vipi kuhusu umeme wa Tanesco umelipwa ? Sipendi Muungano uvunjike, ila ukweli ni kwamba Tanganyika ndiye mlishaji wa Zanzibar. Kuweni na shukrani.
 
Swali halijajibiwa. Zanzibar anaweka hisa BOT kivipi wakati ana PBZ. Kwa nini asiweke PBZ badala yake aweke BOT ?
Niseme tu hujui hata maana ya hisa. Tujaalie ni hivyo unavyojua wewe. Kwani mtu hawezi kuwa na hisa kwenye mradi/uwekezaji zaidi ya mmoja?
 
Bora yenu mna nchi sisi Tanganyika yetu ishapotea
 
Swali hili linaweza kujibiwa vizuri na TANESCO. Mimi hata nikikujibu hutoamini.
Hapa tunaenda vizuri. Miaka zaidi ya 61 ya Muungano ni umri wa mtu aliyestaafu. Bado isemwe wazi, Tanganyika alipoteza na Zanzibar akanufaika. Tudumishe Muungano lakini tuukubali ukweli.
 
Wakati mnaingia kwenye muungano hamkuyajua yote hayo?

Kwa nini msijitoe katika muungano huu unaowatia hasara,?

Zungumzeni huko zanzibar kisha huku mje na msimamo mmoja je mnataka au hamtaki muungano
Kweli; uamuzi ni wao, kama wanaona muungano hauna manufaa wafanye mchakato wa kisiasa na kisheria wajitoe kwa amani kabisa; hakuna sababu ya kugombana, tutabaki kuwa majirani daima maana Tanganyika na Zanzibar hazitahama hapo zilipo; tutaendelea kutembeleana, kuoana, kufanya biashara; kila nchi ikiendesha mambo yake kwa amani bila manung'uniko.
Lila na fila hazitangamani; na mtaka nyingi nasaba, hakosi mingi misiba.
 
Reactions: RMC
Bado isemwe wazi, Tanganyika alipoteza na Zanzibar akanufaika. Tudumishe Muungano lakini tuukubali ukweli
Sema tu. Hiyo ni haki yako. Nami niseme wazi , Zanzibar ilipoteza na inaendelea kupoteza wakati Tanganyika ananufaika.

Hili la kudumisha muungano limo mikononi mwa Watanganyika.
 
Sema tu. Hiyo ni haki yako. Nami niseme wazi , Zanzibar ilipoteza na inaendelea kupoteza wakati Tanganyika ananufaika.

Hili la kudumisha muungano limo mikononi mwa Watanganyika.
Raisi si mzanzibar anashindwa nini kubadili vifungu vinavyowanyonya wazanzibar?
 
Raisi si mzanzibar anashindwa nini kubadili vifungu vinavyowanyonya wazanzibar?
Mkuu naona umekuja na kasi. Hivi unajua nini majukumu Rais kwa mujibu wa sheria za nchi hii?

Nikuambie tu kwamba jukumu la kutunga sheria hapa nchini liko kwenye bunge. Ni bunge ndo linalotunga sheria. Rais huwa hatungi sheria kwani sio kazi yake. Jifunze hilo. Mkuu jitahidi unapofanya mjadala humu kujifananisha na hadhi ya jukwaa hili. Wenye wanaliita "Jamiiforum. Home of great thinkers". Wenyewe huwa hawakurupuki. Watakucheka watu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…