Serikali ya Tanzania kuajiri watumishi 44,096 na kupandisha madaraja watumishi 92, 619

Legacy pekee aliyoiacha mwendazake ni kujenga ukuta mereran Ili tanzanite isiibiwe na watu still wakawa wanamwibia KWA kuchimba underground...
 
Wacha tupige hesabu kidogo...

Watumishi 44,000 lets say average kila mmoja take home salary itakuwa 600,000. (Average) kuna wengine wa 1.5m na wengine laki laki tatu na nusu.

44,000 x 600,000 = 26.4 bilion

Kwa hiyo mzunguko wa hela Tanzania utaongezeka kwa 26.4 billion kwa mwezi - sijapiga watakaopanda madaraja ambao pia mishahara yao itakuwa juu....

Aisee nchi imepata uhuru tena. Maisha hayakwenda kurudi mdogo mdogo, mzunguko wa Tshs 30 billion kwa mwezi mtaani si haba.
 
Mkuu kwani zikiongezwa kwenye mishahara ya walimu waliopo haziendi bank ama sector binafsi?

Kua na watu 10 wanalipwa milioni 10 na kua na watu 200 wanalipwa milioni 10 effects zake kwenye uchumi ni zile zile.

Purchasing power haiongezeki kwa mtindo kua watu wengi wawe na hela kidogo kidogo. Purchasing power inaongezeka kwa watu wengi kua na hela nyingi.
 
Vp kuhusu ajira za jwtz?
JWZT sio watumishi wa umma kwa maana ya utumishi. Wana taratibu zao tofauti kidogo na watumishi wengine wa serikali.

Hawalindwi na sheria za utumishi wa umma.

Hilo halina maana kua hawalipwi mshahara kutoka kwenye pesa za umma.
 
Itakuwa vizuri sana kama utekelezaji utafanyika. Hii itasaidia kupunguza wahitimu wasio na ajira ambao wamekata tamaa uraiani.

Hii pia itakuwa na mwanzo mzuri kwa Mhe. Rais SSH.
We unaona hao watu 40,000 ndio watapunguza wahitimu wasio na ajira? kuna wahitimu takribani 200,000 wameingia mtaani toka JPM aingie madarakani mpaka sasa na katika hio figure naweza kisia maybe ni 7% ya hao jamaa tu ndio wanaweza kuwa wamejiongeza kujiajiri na bodaboda na shughuli zingine!

To make it worse bado hizo nafasi 40,000 kuna ambao wako makazini sasahivi maybe sector binafsi nao watazikimbilia pia hizo application!

Serikali iangalie fursa za uwekezaji tu ambazo zitawanufaisha watu wengi zaidi pia sio kutegemea kuajiri watu 40K tu!
 
Huyu ndiye rais!
Hatutaki mambo ya kujenga uwanja wa ndege Chato na kununua wanasiasa halafu watoto wetu hawapati ajira!
 
Huyu mama ni[emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91]mwendazake nashauri kaburi lake lilindwe asije fufuka akatuletea balaa
 
Mkuu kwani zikiongezwa kwenye mishahara ya walimu waliopo haziendi bank ama sector binafsi?
Kwanini waliopo wasiongezwe na hawa waajiriwe?
Kua na watu 10 wanalipwa milioni 10 na kua na watu 200 wanalipwa milioni 10 effects zake kwenye uchumi ni zile zile.
Hebu nielezee effect inakuwa vipi?
-Watu 10 wakiwa na milioni 10 ni milioni 100 na watu 200 wakiwa na milioni 10 ni bilioni 2, wote wakiweka hela zao Bank tofauti huoni Bank moja utafaidika kuliko nyengine?
Purchasing power haiongezeki kwa mtindo kua watu wengi wawe na hela kidogo kidogo. Purchasing power inaongezeka kwa watu wengi kua na hela nyingi.
Unaweza kuwa sahihi ama sio sahihi hapo kwenye purchasing power.
Watu 40,000 wakiwa na bilioni 20 biashara ndogo zote zitaneemeka kama vile vyakula, nguo etc

Ila watu 10 wakiwa na bilioni 20 purchasing power itaongezeka kwenye vitu luxury kama magari ya kifahari, nyumba za kifahari etc.


Na unapowapa watu wengi uwezo wa kununua biashara inakuwa kuliko watu wa chache Sababu kuna vitu mtu Ana limit ya kufanya.

Mfano chakula, mtu kama hela atakula mlo mmoja ama miwili, ila mtu akiwa na hela hawezi kula milo 10 ama 20 kwa siku.
 
uongo vyuo vyetu vyote ukijumlisha vinatoa graduate 1200 tu wa ualimu kwa mwaka ukipiga kwa miaka 20 nyuma ni elfu 24 tu!! hiyo laki tano umeitoa wapi?
Wewe kwa akili ulionayo unaona graduates ni walimu tu?
Kwa chuo nilichosoma mimi graduates walikuwa mikondo 5! Uhasibu, Sheria, Masoko, Uchumi, Ugavi na Rasilimali watu! Hao ni undergraduates tu! Sijazungumzia diploma wala, certificates ambao ni wengi pia!

Kwa undergraduates tu uki combine figure wanaweza kufika kati ya 900-1000 kama wastani! Sasa zidisha hio figure mara 5 uone itakupaje? Likely 4500 kila baada ya miaka mitano na wanaoajiriwa na kujiajiri hawafiki 500 katika hilo kundi lote!

Vyuo vikuu viko vingapi bongo? Mzumbe,Sua, Tumaini, UDSM, St.Joseph,IFM,CBE, UDOM hivyo ni baadhi tu! Nafikiri vinafika hata 10 au zaidi! Kwa mwaka tu ni 45,000 graduates!

Kwa miaka mitano unazungumzia 225,000 graduates! Kuchekelea ajira 40,000 haingii akilini
 
Hapo ndio unajouliza nchi hii hao tuu ndio watumishi wanaotakiwa kuajiriwa?

Mbona sijasikia wahandisi na wengineo? Bungeni Ummy amesema Halmashauri Wana wahandisi 80 tuu sasa badala ya kuajiri eti wataomba wawatumie wanajeshi wenye fani hiyo,huu ni upuuzi
 
Sijakataa wasiajiriwe wapya.

Pili sikusema watu 10 kila mmoja alipwe milioni 10 ama watu 200 kila mmoja alipwe milioni 10.

Nakubaliana na mtazamo wako lakini pia kuna mengine sikubaliani na mtazamo wako.

Ahsante.
 
Huyu waziri vipi mbona kwenye madini na gesi hawaajiri. Wakati hizo sekta ndio zinaliingizia taifa pato kubwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…