Serikali ya Tanzania kwa roho zenu mnatukwaza sana

Serikali ya Tanzania kwa roho zenu mnatukwaza sana

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Imesikika miito ya kuwataka vinara wake kujiuzulu.

Kuna ya uhaba wa umeme na maji. Kuna ya kuwatelekeza wahanga wa ajali na majanga mbalimbali. Kuna ya kuwatwisha wananchi mizigo ya tozo na kodi zisizo wahusu nyie.

Kuna ya kuwalazimisha wananchi kuikopesha serikali. Kuna upigaji Kila kona. Kuna ya kuwauwa watuhumiwa mikononi mwenu. Kuna ya ubambika kesi.

Kuna ya kujipanga kuwafilisi watu. Agiza chochote nje uone utakavyo bambikiwa tozo, kodi na storage charges mbalimbali zenye lengo la kukitaifisha ulichoagiza.

Angalia faulo zao mabarabarani na magari yao.

Angalia ukubwa wa tozo na kodi. Angalia malipo na marupurupu kwao. Angalia msururu wa ma faini kwetu yasiyowahusu wao..

Kwa kujua wafanyayo kwetu si ajabu kuwa hawataki katu kusikia habari ya katiba mpya.

"Kwani mnayo hata haja ya kumtafuta mchawi?"

Pana hata haja ya kumung'unya maneno basi?

"Mna roho mbaya sana wandugu."
 
Hizi kelele za kuwataka viongozi wajiuzulu huwa zinakuja na kupotea kama upepo, inawezekana hata hao viongozi wenyewe wameshajua hiyo tabia yetu..

Ilianzia kwa Mwigulu na tozo, mpaka leo iko kwa PM na ajali ya Precision, wameshatuzoea sie ni waimbaji mapambio wazuri sana tusiochukua hatua yoyote zaidi.
 
Kuwafahamisha hawa ndugu kutambua wana roho mbaya na kuwa tunajua hivyo ni jambo la muhimu.

Wamejisahau kuwa walipaswa kuwa wawakilishi wetu kwa yote.

Kutufilisi, kutunyanyasa, kujineemesha, kutunyamazisha nk ndiyo imekuwa agenda zao.

Kwamba wanaitishwa kujiuzulu wanapuuza au kutafuta wachawi? Hayo ni mambo mengine, kwani hayapo marefu yasiyokuwa na mwisho.
 
Back
Top Bottom