Serikali ya Tanzania yasema Nemes Tarimo alihukumiwa miaka 7 jela, akafariki akiwa vitani

Serikali ya Tanzania yasema Nemes Tarimo alihukumiwa miaka 7 jela, akafariki akiwa vitani

Mambo mengine ya ajabu sana.

Diaspora wakipata tatizo afisi za balozi nyingu huwa hazitoi ushirikiano.

Diaspora wengi tu wamefanikiwa kupiga hatua na walienda huko muda ila wameshidwa kuwapa fursa y uraia pacha.

Wanasubiri diaspora mmoja akivuruga mambo ndio waingilie hapo kuwa diaspora ni wabaya.
 
Serikali inalaumiwa kwa kutoiwajibisha Russia hasa balozi wake hapa Tz atoe maelezo kwa nini jamaa ambaye alikuwa mfungwa kwenye jela za serikali ya urusi achukuliwe na kuandikishwa kupigana nchini Ukraine kwa kupitia kikundi cha wanamgambo kiitwacho Wagner?Je sheria za kimataifa zinazolinda haki za wafungwa zinaruhusu kitu hicho
Mtu kapewa conditions za kuachiwa gerezani kakubali, angekuwa anaweza pia kukataa, kwani unatak kuniambia magereza ya Russia sasahivi hayana wafungwa? Kama wapo maana yake jua kwamba kujiunga Wagner hakuna mtu analazimishwa bado itabaki kuwa ni choice ya mtu.

Kwa maana hiyo hoja ya Tanzania kuiwajibisha Russia kwa choice za mtu binafsi bado hazina mashiko.

Halafu jamani.. hivi watanzania leo hii ndo tunajidai tunatambua sheria za kimataifa?... Mbona Tundu Lissu amepigwa risasi mpaka leo hakuna uchunguzi wowote umefanyika... mchana kweupe... criminal offence ya aina ile bado hata uchunguzi hamna, halafu ndo mnasema tumuwajibishe Russia kisheria??

Hahahahaaa... hatuna huo usafi. Tusimamie haki kwanza nyumbani kwetu.. Ya Russia na Ukraine tuwaachie wao. Ukraine mwenyewe anatumia wafungwa na wahalifu vitani... hakuna msafi
 
Jamii ya Tanzania inapungukiwa kitu tunaita misingi ya individual liberty, yaani watu wanaamini kwamba nchi inamiliki raia, ndo mana watu wanajaribu sana kutaka kukosoa serikali kwa hii issue.

Nchi za magharibu wameimarika sana kwenye issue za individual liberty, ndo mana huwezi sikia serikali zao zinalaumiwa kwa raia wao kufia Ukraine, kwasababu wanajali misingi ya Liberty... 'Your choices, your consequences'....

Ukichagua kwenda Ukraine kupigana, Ruksa, ukifa ni kivyako na maisha yako...

Ndo mana kuna raia wa ujerumani wawili wamekamatwa wakipigana upande wa Wagner.. huwezi sikia kwamba analaumiwa wazir wa ujerumani, wanaelewa misingi ya uhuru wa mtu binafsi.

Narudia tena, tusi force mambo kwa hii issue, maisha lazima yaendelee
 
Mbona hatuonyeshwi kosa lake lilipelekea kufungwa na hukumu yake. Mtu akifanya makosa na kufungwa lazima kuwe na maelezo kuhusu kosa na hukumu kwenye vyombo vya habari, mahakama za Urusi.

Serikali ilitakiwa kuomba ushahidi wa makosa, hukumu yake na ushahidi kama kweli alitaka kujiunga na Wagner group.

Ila serikali ya Tanzania haijali kabisa raia wake eakiwa nje. Wanaona poa tu ameshafariki.
 
Jamaa mwili wake umekuja nusu na umeharibika sana.jana nilikuwepo kuaga,jeneza halikufunuliwa,kuna ndugu yake akasema mwili umekuja kiwiliwili cha juu tu,ni kama vile jamaa alipigwa bomu vitani.halafu issue ya kufungwa ni kweli jamaa alikua kafungwa na hata ndugu zake walikua wanaijua coz akiwa jela alikua anawasliana nao na lengo ilikua iuzwe nyumba yake ili pesa zikamsaidie kutoka jela,so wakati ndugu wanashauriana nini cha kufanya ndio jamaa akapata hiyo offer ya wiegner group akapigane miezi 6 then aachiwe ndio hivyo bahati mbaya ikatokea akafa.
 
Nilisoma sehemu serikali ya Tz ilikataa jeneza lisifunguliwe sasa hicho kiwiliwili ulikiona wapi?
 
Mbowe kuachiwa ile kesi ya Ugaidi na wale makomandoo wa JWTZ serikali ilikuwa sahihi

Chadema ilipeleka watu wake Wagner Grouo kupindua nchi 2015

Lema akadakwa kama kamanda wa uasi kupewa dhamana akatoroka akatororokea kanada kamanda mwingine wa maasi Tundu Lisu akakimbia nchi mbio ubeligiji baada ya mission kufeli

Sababu serikali ina mkono mrefu kupitia chama tawala ilipandikiza mamluki kiibao Chadema

Wahusika wakuu Wakatoroka nchini kwenda nje ya nchi zigo wakambwagia Mbowe
Aliyesota ndani

Serikali ikamuonea huruma ikafuta kesi sababu hakujua kuwa wenzie wanapeleka wana Chadema kwenda Urusi kwa kisingizio cha kusoma kumbe wanaenda kambi za Wagner mercenaries fighters mamluki wa kupigana kwa malipo

Anyway Lisu karibu Tanzania uje kumzika huyo Tarimo mliyempeleka Wagner Group.Russia japo bado wako kule wengi wa Chadema

Ila serikali hailali kuhakikisha watanzania wako salama na nchi inakuwa na amani

Karibu Tundu Lissu uje kumzika kamanda wako Mliyempeleka. Urusi ajiunge.na Wagner group apate uzoefu wa vita aongoze vita kuitoa CCM madarakani kwa mtutu
Wa bunduki akirudi na kuhitimu Russia ambako ndiko kambi kubwa za wagner.group
🚮🚮🚮
Utakuwa hujafikishwa kileleni muda mrefu bila shaka..
Maana siyo kwa pumba hizi🙄
 
Wacha ujinga, CDM siyo msemaji wa Serikali. Kibali cha kutoka nje ya nchi unapewa na Serikali kupitia passport na visa
CDM watajua, ni mtu wao, tuanzie kwenye Uchaguzi aliposhindwa. Inaonekana hakuaga mtu wala kupitia njia rasmi baada ya kurudi masomoni. In other words ni mzamiaji nadhani alijificha kwenye meli hadi Urusi. Wa kuulizwa ni CHADEMA, sera yao ni kusaidia diaspora. Si inasemekana hata mbowe na tindulissu mke na watoto wao raia wa Marekani? Tutajuaje kama hawako Ukraine.
 
Tanzania haiwajali wananchi wake wa ndani na nje, serikali imefunga mjadala! Warusi ni marafiki zetu wa damu.
Tanzania inawahali sana raia wake ndiyo maana imeleta mwili ingawa mwenyewe alishaikana. CHADEMA waulizwe hii sera yao ya uraiapacha mi ya nini hasa kama si kutetea magaidi na walioimimbia nchi yetu?
 
Ukiingia tu ngozi nyeusi unatupwa mstari wa mbele uwe chambo
Exactly! Sasa kwa nini uende huko? Kwa nini uitukane Tanzania? Mpaka sasa bado sijaelewa alienda wapi baada ya kushindwa Ubunge, hadi aibukie Ukraine?
 
Ushawishi wa pesa unanguvu kuliko kushikiwa mtutu wa bunduki, kama alienda kupigana kwa kulazimishwa usingesikia jambo la pesa.
Alitumwa na CHADEMA aende kutafuta tumehuru
 
Hili watu wengi wanaonekana kulipinga ikiwemo familia yake pia

Inavyoonekana huko waafrika wanalazimishwa kwenda vitani na inapotokea bahati mbaya wameuwawa, wanatoa taarifa kuwa alikuwa mfungwa

Fatilia kifo cha yule kibopa wa Malawi sijui Zambia alivyokufa ripoti ni ile ile kama hii

Bado kuna m-algeria mwingine naye alidanja vitani kwa tuhuma hizo hizo
Swali: waliendaje huko in the first place? Kwa nini hakukaa tu Ubungo na kuchapa kazi?
 
Serikali inalaumiwa kwa kutoiwajibisha Russia hasa balozi wake hapa Tz atoe maelezo kwa nini jamaa ambaye alikuwa mfungwa kwenye jela za serikali ya urusi achukuliwe na kuandikishwa kupigana nchini Ukraine kwa kupitia kikundi cha wanamgambo kiitwacho Wagner?Je sheria za kimataifa zinazolinda haki za wafungwa zinaruhusu kitu hicho
Swali la kwanza: aliaga? La pili, alipofika alijiandikisha Ubalozini? La tatu, alifungwa kwa kosa la madawa ya kulevya au mauaji inategemea unasoma ripoti ipi je, Serkali ilimtuma kuuza madawa ya kulevya au kuua? Usisahau alitokea CHADEMA, aliagaje Tawini?
 
Mbona hatuonyeshwi kosa lake lilipelekea kufungwa na hukumu yake. Mtu akifanya makosa na kufungwa lazima kuwe na maelezo kuhusu kosa na hukumu kwenye vyombo vya habari, mahakama za Urusi.

Serikali ilitakiwa kuomba ushahidi wa makosa, hukumu yake na ushahidi kama kweli alitaka kujiunga na Wagner group.

Ila serikali ya Tanzania haijali kabisa raia wake eakiwa nje. Wanaona poa tu ameshafariki.
Serkali inahitaji ushirikiano, tundulissi hadi leo ni matusi tupu wala hajaripoti Polisi na dereva wake kamficha Ulaya. Na Tarimo hivi hivo. Kwanza, alipofika Urusi angejiandikisha Ubalozini. Pili, alipokamatwa na kosa angeomba awasiliane na Ubalozi kwanza, haki hiyo ipo, mbona hakutumia? Ikiwa alitumwa na CHADEMA kwa vile hawana dola si rahisi kusaidia.
 
Kuna maaskari maalum kazi yao ni kuzuia usikimbie, wao hawapigani wako kuhakikisha unapigana wewe. Na ukiwa vitani hela unatunza wapi, kuondoka frontline mpaka kufika benki ukachukue hela tiyari warranty ishatoka ukamatwe. Na mipaka sasa hivi imekazwa ulinzi. Chance ya kutoroka ipo kidogo, ila kutoroka na hela haipo kabisa
Mkuu hao maaskari maalumu ambao hawapigani kazi yao ni kunilinda mimi nipigane je siwezi kuwapiga risasi ama siwezi kuwatoroka na je ina maana wenyewe kambi ikishambuliwa wanakimbia na kuwaacha wapiganaji ama inakuwaje emu toa ifafanuzi zaidi kwa sababu najua kuwa, frontline kila askrai anakuwa ana silaha za kutosha bunduki yenye risasi za kutosha mabomu na magrenade ya kutosha sasa, inashindikana vip mimi kuwalipua hawa wanaonilinda mimi nisitoroke yaani kwani wao wanakuwa na ngao ya risasi au mabomu? T14 Armata
 
Uasi wa kumpiga askari jeshi mlio upande mmoja vitani hauwezi kukuacha salama ukifanya hivyo utauawa within a minute wala hutapiga hatua hata kumi za kukimbia watu walio Frontline wako full equiped na vidole viko kwenye trigger all the time.Unaweza toroka ukiwa backbencher au uwe mpishi

Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom