Serikali ya Tanzania yasema Nemes Tarimo alihukumiwa miaka 7 jela, akafariki akiwa vitani

Mambo mengine ya ajabu sana.

Diaspora wakipata tatizo afisi za balozi nyingu huwa hazitoi ushirikiano.

Diaspora wengi tu wamefanikiwa kupiga hatua na walienda huko muda ila wameshidwa kuwapa fursa y uraia pacha.

Wanasubiri diaspora mmoja akivuruga mambo ndio waingilie hapo kuwa diaspora ni wabaya.
 
Mtu kapewa conditions za kuachiwa gerezani kakubali, angekuwa anaweza pia kukataa, kwani unatak kuniambia magereza ya Russia sasahivi hayana wafungwa? Kama wapo maana yake jua kwamba kujiunga Wagner hakuna mtu analazimishwa bado itabaki kuwa ni choice ya mtu.

Kwa maana hiyo hoja ya Tanzania kuiwajibisha Russia kwa choice za mtu binafsi bado hazina mashiko.

Halafu jamani.. hivi watanzania leo hii ndo tunajidai tunatambua sheria za kimataifa?... Mbona Tundu Lissu amepigwa risasi mpaka leo hakuna uchunguzi wowote umefanyika... mchana kweupe... criminal offence ya aina ile bado hata uchunguzi hamna, halafu ndo mnasema tumuwajibishe Russia kisheria??

Hahahahaaa... hatuna huo usafi. Tusimamie haki kwanza nyumbani kwetu.. Ya Russia na Ukraine tuwaachie wao. Ukraine mwenyewe anatumia wafungwa na wahalifu vitani... hakuna msafi
 
Jamii ya Tanzania inapungukiwa kitu tunaita misingi ya individual liberty, yaani watu wanaamini kwamba nchi inamiliki raia, ndo mana watu wanajaribu sana kutaka kukosoa serikali kwa hii issue.

Nchi za magharibu wameimarika sana kwenye issue za individual liberty, ndo mana huwezi sikia serikali zao zinalaumiwa kwa raia wao kufia Ukraine, kwasababu wanajali misingi ya Liberty... 'Your choices, your consequences'....

Ukichagua kwenda Ukraine kupigana, Ruksa, ukifa ni kivyako na maisha yako...

Ndo mana kuna raia wa ujerumani wawili wamekamatwa wakipigana upande wa Wagner.. huwezi sikia kwamba analaumiwa wazir wa ujerumani, wanaelewa misingi ya uhuru wa mtu binafsi.

Narudia tena, tusi force mambo kwa hii issue, maisha lazima yaendelee
 
Mbona hatuonyeshwi kosa lake lilipelekea kufungwa na hukumu yake. Mtu akifanya makosa na kufungwa lazima kuwe na maelezo kuhusu kosa na hukumu kwenye vyombo vya habari, mahakama za Urusi.

Serikali ilitakiwa kuomba ushahidi wa makosa, hukumu yake na ushahidi kama kweli alitaka kujiunga na Wagner group.

Ila serikali ya Tanzania haijali kabisa raia wake eakiwa nje. Wanaona poa tu ameshafariki.
 
Jamaa mwili wake umekuja nusu na umeharibika sana.jana nilikuwepo kuaga,jeneza halikufunuliwa,kuna ndugu yake akasema mwili umekuja kiwiliwili cha juu tu,ni kama vile jamaa alipigwa bomu vitani.halafu issue ya kufungwa ni kweli jamaa alikua kafungwa na hata ndugu zake walikua wanaijua coz akiwa jela alikua anawasliana nao na lengo ilikua iuzwe nyumba yake ili pesa zikamsaidie kutoka jela,so wakati ndugu wanashauriana nini cha kufanya ndio jamaa akapata hiyo offer ya wiegner group akapigane miezi 6 then aachiwe ndio hivyo bahati mbaya ikatokea akafa.
 
Nilisoma sehemu serikali ya Tz ilikataa jeneza lisifunguliwe sasa hicho kiwiliwili ulikiona wapi?
 
🚮🚮🚮
Utakuwa hujafikishwa kileleni muda mrefu bila shaka..
Maana siyo kwa pumba hizi🙄
 
Wacha ujinga, CDM siyo msemaji wa Serikali. Kibali cha kutoka nje ya nchi unapewa na Serikali kupitia passport na visa
CDM watajua, ni mtu wao, tuanzie kwenye Uchaguzi aliposhindwa. Inaonekana hakuaga mtu wala kupitia njia rasmi baada ya kurudi masomoni. In other words ni mzamiaji nadhani alijificha kwenye meli hadi Urusi. Wa kuulizwa ni CHADEMA, sera yao ni kusaidia diaspora. Si inasemekana hata mbowe na tindulissu mke na watoto wao raia wa Marekani? Tutajuaje kama hawako Ukraine.
 
Tanzania haiwajali wananchi wake wa ndani na nje, serikali imefunga mjadala! Warusi ni marafiki zetu wa damu.
Tanzania inawahali sana raia wake ndiyo maana imeleta mwili ingawa mwenyewe alishaikana. CHADEMA waulizwe hii sera yao ya uraiapacha mi ya nini hasa kama si kutetea magaidi na walioimimbia nchi yetu?
 
Ukiingia tu ngozi nyeusi unatupwa mstari wa mbele uwe chambo
Exactly! Sasa kwa nini uende huko? Kwa nini uitukane Tanzania? Mpaka sasa bado sijaelewa alienda wapi baada ya kushindwa Ubunge, hadi aibukie Ukraine?
 
Ushawishi wa pesa unanguvu kuliko kushikiwa mtutu wa bunduki, kama alienda kupigana kwa kulazimishwa usingesikia jambo la pesa.
Alitumwa na CHADEMA aende kutafuta tumehuru
 
Swali: waliendaje huko in the first place? Kwa nini hakukaa tu Ubungo na kuchapa kazi?
 
Swali la kwanza: aliaga? La pili, alipofika alijiandikisha Ubalozini? La tatu, alifungwa kwa kosa la madawa ya kulevya au mauaji inategemea unasoma ripoti ipi je, Serkali ilimtuma kuuza madawa ya kulevya au kuua? Usisahau alitokea CHADEMA, aliagaje Tawini?
 
Serkali inahitaji ushirikiano, tundulissi hadi leo ni matusi tupu wala hajaripoti Polisi na dereva wake kamficha Ulaya. Na Tarimo hivi hivo. Kwanza, alipofika Urusi angejiandikisha Ubalozini. Pili, alipokamatwa na kosa angeomba awasiliane na Ubalozi kwanza, haki hiyo ipo, mbona hakutumia? Ikiwa alitumwa na CHADEMA kwa vile hawana dola si rahisi kusaidia.
 
Mkuu hao maaskari maalumu ambao hawapigani kazi yao ni kunilinda mimi nipigane je siwezi kuwapiga risasi ama siwezi kuwatoroka na je ina maana wenyewe kambi ikishambuliwa wanakimbia na kuwaacha wapiganaji ama inakuwaje emu toa ifafanuzi zaidi kwa sababu najua kuwa, frontline kila askrai anakuwa ana silaha za kutosha bunduki yenye risasi za kutosha mabomu na magrenade ya kutosha sasa, inashindikana vip mimi kuwalipua hawa wanaonilinda mimi nisitoroke yaani kwani wao wanakuwa na ngao ya risasi au mabomu? T14 Armata
 
Uasi wa kumpiga askari jeshi mlio upande mmoja vitani hauwezi kukuacha salama ukifanya hivyo utauawa within a minute wala hutapiga hatua hata kumi za kukimbia watu walio Frontline wako full equiped na vidole viko kwenye trigger all the time.Unaweza toroka ukiwa backbencher au uwe mpishi

Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…