Serikali ya Tanzania yazuia ndege kutoka shirika la Kenya Airways kutua Dar, Kilimanjaro na Zanzibar

Serikali ya Tanzania yazuia ndege kutoka shirika la Kenya Airways kutua Dar, Kilimanjaro na Zanzibar

Sema kujidanganya! Munapenda kujidanganya watanzania. KQ ilikuwa inakuja Dar mara 14 kwa wiki hiyo ni mara mbili kwa siku kuanzia 2015. Linganisha hiyo na KQ mara 5 kwa siku kuenda entebbe, Jambo jet mara 3 kwa siku kuenda entebbe.

Hata kibiashara, Kenya inafanya biashara mingi na uganda na Rwanda kushinda Tanzania. Biashara kati ya Kenya na Uganda ni karibu mara tatu kati ya Kenya na Tanzania.
Subiria impact zake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imefuta kibali kilichokuwa kikiruhusu ndege za Shirika la Ndege la Kenya (KQ) kutua Tanzania, uamuzi huo umekuja baada ya Kenya kutoijumuisha Tanzania katika orodha ya Nchi ambazo Raia wake wataruhusiwa kuingia Kenya kuanzia Agosti 01. https://t.co/eAHnSfq4UO

IMG_20200801_054845.jpg
IMG_20200801_054852.jpg
 
Corona imetuletea ubaguzi na chuki, Ingeisha tu tuishi vizuri na majerani zetu.
 
Wakenya wanalia lia, kwanza ndo wamemaliza idadi yaajira nchini so wakizingua itakuwa fresh dada na kaka zetu wapate ajira.
JPM hajaribiwi zama zimebadilika

Na kampeni zinaanza mwezi huu, ndugu zangu wa chadema wasijisahau wakasimama na kenyata katika hili maana wapo kupinga kila kitu.
 
Wamepata hoja ya kipuuzi wananchi hatuwasikilizi na uchaguzi utakuwa huru na haki
Na kampeni zinaanza mwezi huu, ndugu zangu wa chadema wasijisahau wakasimama na kenyata katika hili maana wapo kupinga kila kitu.
 
HAHAHAHA, Kelele za chura hiyo. Uganda ama Rwanda zikifunga Kenya inaweza kuumia lakini si Tanzania. KQ na mtoto wake jambo jet zinaenda entebbe na kigali kushinda dar na hizo vitu zingine umetaja.
KQ unafanya safari 49 kwa wiki kuja Dar, huko Kigali itampeleka Nani?
 
Nilisema juzi nahofia majibu ya Magufuli kwa huu uamuzi wa Kenya yakawa mabaya zaidi kwa mstakabali wa EAC hasa Kibiashara.

Nchi zote lazima ziathirike kwa kiwango kikubwa.

Russia Wameruhusu Tanzania kutua kwao Kenya wanatuzuia ili kuionyesha Dunia Tanzania hatuko makini kwenye mapambano ya CORONA

Kenya ilibidi waende mbali zaidi kwa kuzuia Ndege zao kuja Tanzania kuchukua korona, badala yake wamezuia za Tanzania kupeleka korona Ila wameruhusu za Kenya kuja kuchukua Korona.
 
Kenya, Kenya, Kenya.
Hiyo choko choko yako itakula faida yako.

Kama wataka chokonoa kamchokonoe samaki Pweza pale baharini Mombasa.
Tanzania huta iweza.

Sasa kula jeuri yako.
Hatuna shida na Kenya
Tunalinda heshima yetu

Ibakie hivyo hivyo, kaa kwako nikae kwangu.
Ndivyo ulivyo taka na umeipata.

Sasa walia lia nini tena.
 
Sema kujidanganya! Munapenda kujidanganya watanzania. KQ ilikuwa inakuja Dar mara 14 kwa wiki hiyo ni mara mbili kwa siku kuanzia 2015. Linganisha hiyo na KQ mara 5 kwa siku kuenda entebbe, Jambo jet mara 3 kwa siku kuenda entebbe.

Hata kibiashara, Kenya inafanya biashara mingi na uganda na Rwanda kushinda Tanzania. Biashara kati ya Kenya na Uganda ni karibu mara tatu kati ya Kenya na Tanzania.
Basi sawa, kuna shida kwani?
 
Kama umezaliwa mwaka 1985 halafu huu ndio uwezo wako,pole sana!
Mbona KQ pekee, si mungefungia hata Jambo jet ambayo ni mtoto 100% wa KQ, pia precision air ambayo ni 50% mtoto wa KQ? Yani hapo hakuna kazi imefanyika ni vitisho tu. Hata mufungie KQ na jambo jet bado KQ itapata pesa kupitia precision air.
 
Back
Top Bottom