Sasa hivi (PM2:57) waziri wa Afya Kenya(Muthai Kagwe) kama sijakosea kuandika jina lake, yuko anahutubia , miongoni mwa jambo ambalo anazungumzia ni hili suala, kwa machache anadai kuwa wao hawajazui ndege wala mtanzania kuingia Kenya, anakiri kuwa wao hawana uwezo huo wa kuzuia Mtanzania au ndege ya Tanzania kuingia Kenya, aidha anaendelea kwa kusema kuwa Tanzania ni mdau muhimu sana wa maendeleo ya Kenya, amedai kuwa leo asubuhi wameongea na mh Kamwerwe/re waziri husika wa Tanzania na kuomba hili jambo liishe haraka sana kwani wao hawajafunga anga kwa ajili ya Tanzania bali wameruhusu baadhi ya nchi na kesho jumapili wataendelea kutoa orodha ya nchi nyingine ambazo zitaruhusiwa kuingia Kenya. Pia mdahalo unaendelea baadhi ya wajumbe wanasisitiza ni lini ili suala litaisha maana ni kosa kubwa sana kuizuia Tanzania, majibu ni yaleyale kuwa wao wameomba Tanzania kwa dhati kabisa hili jambo liishe haraka sana maana wao hawakulenga kama serikali ya Tanzania ilivyolipokea. Pia amewaeleza wakenya kuwa ifikapo kesho wanatumaini watakuwa wamepata majibu mazuri kutoka Tanzania na hili jambo litakuwa limeisha.