"Mathayo 21:42 Yesu akawaambia, Hamkupata kusoma katika maandiko, Jiwe walilolikataa waashi, Hilo limekuwa jiwe kuu la pembeni; Neno hili limetoka kwa Bwana, Nalo ni ajabu machoni petu?
Mathayo 21:43 Kwa sababu hiyo nawaambia, Ufalme wa Mungu utaondolewa kwenu, nao watapewa taifa lingine lenye kuzaa matunda yake.
Mathayo 21:44 Naye aangukaye juu ya jiwe hilo atavunjika-vunjika; naye ye yote ambaye litamwangukia, litamsaga tikitiki.
Mathayo 21:45 Wakuu wa makuhani na Mafarisayo, waliposikia mifano yake, walitambua ya kuwa anawanenea wao."
Nadhani JIWE limeeleweka.
Jiwe walilokikataa waashi sasa limekuwa Jiwe Kuu la Pembeni.
Mkilichezea lita wavunjavunja na kuwasaga kabisa yaani tikitiki
Nadhani Majirani wanafahamu kuwa nawanenea wao. Kwa kusikia mfano huu.
Jesus is Lord.