Serikali ya Urusi yakanusha kuhusika na mauaji ya Evgeny Prigozhin

Ikulu ya Urusi (Kremlin) imekanusha vikali kuhusika kwa namna yoyote na ajali ya ndege inayosemekana kumuua Mkuu wa kundi la mamluki la Wagner, Yevgeny Prigozhin, ikisema tuhuma hizo ni uzushi usiokuwa na maana.

Msemaji wa Ikulu ya Urusi, Dmitry Peskov, amesema shutuma dhidi ya Nchi yake hazina mashiko yoyote na badala yake ametizupia lawama nchi za Magharibi kwa kusambaza uvumi usio maana.

"Tazama, kwa sasa kuna uvumi mwingi sana kuhusiana na ajali hii ya ndege na vifo vya abiria wa ndege hiyo akiwemo Yevgeny Prigozhin, bila shaka, katika Nchi za Magharibi, uvumi huo unawekwa kwa njia fulani na wote ni uongo mtupu na bila shaka ni muhimu kutumia ukweli unaporipoti kuhusiana na suala hili, kwa sasa ukweli ni mchache kwa sababu uchunguzi bado unaendelea”
FB_IMG_1692991323588.jpg
 
Nakupata mkuu, lakini pia usisahau kwamba siku ile Prigozhin alipoamuru vikosi vyake vigeuze na vielekee Moscow kumkabili Shoigu na Gerasimov, vikosi hivyo vilitungua ndege za jeshi la anga la Russia na kuua marubani wapatao 16 waloanza kuwakabili.

Hivyo jeshi nalo bado lilikuwa na hasira kwamba Wagner na Prigozhin wameachwa wazurure bila ku chukuliwa hatua zozote.
Asante sana Mkuu kwa nyongeza hii.
Kwa hiyo Prigozin alifanya makosa kweli na kama alifanya makosa hayo basi inawezekana hiyo na mengine tusiyoyajua ndio yalikua sababu tosha ya kumla kichwa.
Pengine alikua kama mgema aliesifiwa tembo alilitia maji.
 
Prighozin alipewa msamaha bandia kwa ule uasi uliomponza.
Sawa kabisa,ni kweli,
kama ni kweli lile jaribio la uasi lilikua ni la kweli na wala sio igizo kama watu wengi wanavyofikiria basi alistahili kuliwa kichwa.

Ilibidi itumike akili kubwa sana kwanza kabla ya kumla kichwa.

Mbinu ya kumla kichwa isiyoweza kuvuruga maendeleo ya SMO

Ilibidi kwanza yeye apumbazwe,wafuasi wake wapumbazwe na Warusi wapumbazwe kwa kuonesha kama kasamehewa utafutwe muda muafaka kisha aliwe kichwa ili kusiwe na machafuko ama vurugu kwa wale wanaompenda.

Kama kweli alifanya kwa makusudi jaribio lile basi alikosea,kwa sababu katikati ya operation yeye analeta mambo ya mapinduzi.
Maana yake alitaka jeshi lisifocus na smo lianze kupambana na watu wake hivyo kutoka kwenye malengo na hatimae kumpa adui advantage.
Sasa akili kubwa ya Moscow ikakataa kuingia kwenye mtego huo.

Hata hivyo.
Hii naiandika lkn Kwa assumption kwamba jaribio lile kama ilikua la kweli.
Maana Mimi sijui kama lilikua la kweli ama igizo.hayo ni mambo ya ndani,Mimi sijui.
 
Nakupata mkuu, lakini pia usisahau kwamba siku ile Prigozhin alipoamuru vikosi vyake vigeuze na vielekee Moscow kumkabili Shoigu na Gerasimov, vikosi hivyo vilitungua ndege za jeshi la anga la Russia na kuua marubani wapatao 16 waloanza kuwakabili.

Hivyo jeshi nalo bado lilikuwa na hasira kwamba Wagner na Prigozhin wameachwa wazurure bila ku chukuliwa hatua zozote.
Du! Marubani 16.ebu fafanua vizuri hapo[emoji23][emoji23]
 
Ikulu ya Urusi (Kremlin) imekanusha vikali kuhusika kwa namna yoyote na ajali ya ndege inayosemekana kumuua Mkuu wa kundi la mamluki la Wagner, Yevgeny Prigozhin, ikisema tuhuma hizo ni uzushi usiokuwa na maana.

Msemaji wa Ikulu ya Urusi, Dmitry Peskov, amesema shutuma dhidi ya Nchi yake hazina mashiko yoyote na badala yake ametizupia lawama nchi za Magharibi kwa kusambaza uvumi usio maana.

"Tazama, kwa sasa kuna uvumi mwingi sana kuhusiana na ajali hii ya ndege na vifo vya abiria wa ndege hiyo akiwemo Yevgeny Prigozhin, bila shaka, katika Nchi za Magharibi, uvumi huo unawekwa kwa njia fulani na wote ni uongo mtupu na bila shaka ni muhimu kutumia ukweli unaporipoti kuhusiana na suala hili, kwa sasa ukweli ni mchache kwa sababu uchunguzi bado unaendelea”

Yule muhuni alikuwa na maadui wengi sana. Waliomuua ni ufaransa. Maana kitu alichowafanyia Sahel hawatakuja kukisahau.
 
Back
Top Bottom