Brigedia Chan-ocha
JF-Expert Member
- Mar 7, 2014
- 1,353
- 2,846
Ewe Serikali ya wanyonge nini kinajiri huko kwenye viwanda vya vifaa vya ujenzi? mbona Bei inapaa sana na hatusikii tamko la serikali kuhusu kupaa huku kwa bei?
Mathalani, kanda ya ziwa Cement ilikuwa inauzwa sh. 18500, baadae ikapaa hadi 19000, baada ya siku 5 ikapaa hadi 19500, baada ya siku 4 ikapaa hadi 21000 kwa mfuko, sasa najiuliza tatizo ni nini huko viwandani? na Nondo nimejulishwa kwamba zimepanda kutoka sh. 20000 kwa nondo ya milimita 12 hadi sh. 22000, serikali ipo wapi?
Waziri yupo wapi? hili nalo hadi tumsubirie Tundu Lissu alisemee ndo tutoke mafichoni kulielezea? kama mahitaji yamekuwa makubwa kwa nini msiruhusu vifaa kutoka nchi jirani ya kenya au Uganda au Rwanda viingie nchini ili ku-stabilize Bei na kutomuumiza mwananchi wa kawaida?
Sisi wananchi tunahitaji maelezo ya kina ya kwa nini Hali hii ipo hivi.