Serikali ya Wanyonge, bei ya vifaa vya ujenzi yapaa maradufu, kunani?

Serikali ya Wanyonge, bei ya vifaa vya ujenzi yapaa maradufu, kunani?

Hela ya kampeni kwa maccm. Viwanda vya cement vipo vinne. Wazo, mbeya cement, tanga cement na dangote. Mbona uzalishaji na mahitaji ni mbingu na ardhi! % kubwa ya mali ghafi zinapatikana hapa hapa bongo. Watakuwa wamepandishiwa kodi, na mlaji ndio mlipaji. Hamna namna inabidi ununue tu maana pesa haiwekeki. Na hatujui baada ya uchaguzi kama hawa mashetani yatarudi kuitawala hii nchi ndio tutanyooshwa sawasawa.

Msisahau 28/10 kura kwa Lissu.
Lake cement, Camel cement, Kilimanjaro cement vipo vingi. Demand ni kubwa, demand ikishuka na bei inashuka.
 
Ninamifuko kama 150 ya cement kuna ka project nilikua nakavutia kasi. Ikipanda sana naiuza afu mwakani ikishuka nanunua mingi zaidi

Unahifadhi vipi hiyo cement bila kuganda?
 
Bei ya vifaa vya ujenzi haina vyama, uzuri wote tunaisoma namba!
 
Saruji inatoka Dubai inafika Zanzibar inauzwa 13,000, inatoka Tanga ikifika zanzibar bei hio hio! Sukari inapanda meli tokea Brasil ikifika hapa inauzwa kwa unafuu ila inayotoka mtibwa inakuwa ghali, vitunguu maji vinatoka dubai rahisi kuliko kununua bara. Yaani kuagiza vitu nje ni rahisi kuliko vinavyozalishwa hapa hapa. Ukweli tugawane fito tu 😀
 
Back
Top Bottom