Serikali ya Wanyonge, bei ya vifaa vya ujenzi yapaa maradufu, kunani?

Serikali ya Wanyonge, bei ya vifaa vya ujenzi yapaa maradufu, kunani?

1601911041403.png
 
Hela ya kampeni kwa maccm. Viwanda vya cement vipo vinne. Wazo, mbeya cement, tanga cement na dangote. Mbona uzalishaji na mahitaji ni mbingu na ardhi! % kubwa ya mali ghafi zinapatikana hapa hapa bongo. Watakuwa wamepandishiwa kodi, na mlaji ndio mlipaji. Hamna namna inabidi ununue tu maana pesa haiwekeki. Na hatujui baada ya uchaguzi kama hawa mashetani yatarudi kuitawala hii nchi ndio tutanyooshwa sawasawa.

Msisahau 28/10 kura kwa Lissu.
 
Miradi ya serikali ni mingi, SGR, Stingler, Ubungo flyover, Salender Bridge, Dodoma Projects etc

Lazima cement iwe adimu

Cement sio adimu bali ni ghali sana. Viwanda vingi vinavyozalisha fifaa vya ujenzi vimepunguza kwa kiasi kikubwa kutokana na mauzo/mahitaji ya bidhaa wanazozalisha kupungua sana, hivyo ili kuhimili gharama za uendeshaji na wapate faida pia inabidi wapandishe bei za bidhaa zao inapokua lazima.
 
Ewe Serikali ya wanyonge nini kinajiri huko kwenye viwanda vya vifaa vya ujenzi? mbona Bei inapaa sana na hatusikii tamko la serikali kuhusu kupaa huku kwa bei?

Mathalani, kanda ya ziwa Cement ilikuwa inauzwa sh. 18500, baadae ikapaa hadi 19000, baada ya siku 5 ikapaa hadi 19500, baada ya siku 4 ikapaa hadi 21000 kwa mfuko, sasa najiuliza tatizo ni nini huko viwandani? na Nondo nimejulishwa kwamba zimepanda kutoka sh. 20000 kwa nondo ya milimita 12 hadi sh. 22000, serikali ipo wapi?

Waziri yupo wapi? hili nalo hadi tumsubirie Tundu Lissu alisemee ndo tutoke mafichoni kulielezea? kama mahitaji yamekuwa makubwa kwa nini msiruhusu vifaa kutoka nchi jirani ya kenya au Uganda au Rwanda viingie nchini ili ku-stabilize Bei na kutomuumiza mwananchi wa kawaida?

Sisi wananchi tunahitaji maelezo ya kina ya kwa nini Hali hii ipo hivi.
Viwanda vingi vinamilikiwa na wageni ama wazawa wenye asili ya India au Arabia. Miaka yote uchaguzi ukikaribia viwanda vingi hufungwa, wamiliki huenda nje kusubiria matokeo ya uchaguzi. Kifuatacho ni uhaba wa bidhaa na kuipeleka bei juu.
 
Maisha yataendelea kuwa magumu sanaaaa tuuu, hakuna ongezeko la mshahara kwa waajiriwa ila gharama za maisha zinazidi kupanda kwa kas kubwa ndani ya miaka 5 mshahara ni uleule ila sukari imepanda, Ada ipo juu, cement, nondo hazishkiki yani shida tupu...
 
Unajulishwa halafu unataka utulishe matango pori na sisi, nenda kapige picha hizo bei, au tupigie picha risiti ya hivyo vifaa ulivyonunua tuone hapa, usituletee stori zako za nadharia leta ushahidi hapa, watanzania tumechoka kulishwa Matango pori.
Tunasimama na msema kweli wetu Magufuli, na tutamchagua yeye Magufuli ndiye msema kweli wetu na mtetezi wetu.
wewe na Nani?
 
Ewe Serikali ya wanyonge nini kinajiri huko kwenye viwanda vya vifaa vya ujenzi? mbona Bei inapaa sana na hatusikii tamko la serikali kuhusu kupaa huku kwa bei?

Mathalani, kanda ya ziwa Cement ilikuwa inauzwa sh. 18500, baadae ikapaa hadi 19000, baada ya siku 5 ikapaa hadi 19500, baada ya siku 4 ikapaa hadi 21000 kwa mfuko, sasa najiuliza tatizo ni nini huko viwandani? na Nondo nimejulishwa kwamba zimepanda kutoka sh. 20000 kwa nondo ya milimita 12 hadi sh. 22000, serikali ipo wapi?

Waziri yupo wapi? hili nalo hadi tumsubirie Tundu Lissu alisemee ndo tutoke mafichoni kulielezea? kama mahitaji yamekuwa makubwa kwa nini msiruhusu vifaa kutoka nchi jirani ya kenya au Uganda au Rwanda viingie nchini ili ku-stabilize Bei na kutomuumiza mwananchi wa kawaida?

Sisi wananchi tunahitaji maelezo ya kina ya kwa nini Hali hii ipo hivi.
Unajua kuna watu walijua uchumi ni just an issue like mixing chemicals and observing reactions.
Uchumi ni Demand na Supply bhana. Mahitaji makubwa alafu mtu anabana nchi jirani wasiingize bidhaa zao wakati ndani uzarishaji mdogo matokeo yake ndio haya sasa!
Mbaya zaidi bado mtu anataka tena aongezewe muda sera zikiwa zile zile za kununua midege which has nothing to do with people's welfare
 
Back
Top Bottom