Ranchi ya Makurunge iliyopo Bagamoyo ni mali halali ya SMZ. Tena tuna bahati wakoloni Wajerumani walitusaidia, ukanda wa maili 10 za Pwani yote ya bahati ya Hindi kuanzia Sofala hadi Mombasa ilikuwa ni mali ya Sultan of Zanzibar!. Sultan alipewa eneo hilo na mkutano wa Berlin kugawana Africa ile 1884. Miaka 6 baadae 1890, ndipo Ujerumani, na Uingereza wakaingia mkataba za Sultan of Zanzibar awaachie, na wao wakaahidi kumlinda.
Mkataba huo unaitwa The Heligoland Treaty, huku Ujerumani na Uingereza wakiachiana maeneo, visiwa vya Witu na Heligoland, na ni mkataba huu ndio wakahamisha mipaka ya Ziwa Nyasa kulifanya la Malawi!.
Ni kweli SMZ Ilipewa eneo la Makurunge litumike kama Ranch na Stock Holding point, kwa ajili ya Mifugo inayo safirishwa kutoka Mainland kwenda Z"bar. Walipatiwa na Baba wa Taifa Mwl Julius Nyerere na wanalimiliki kihalali