BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
SERIKALI imeagiza mabasi yote yanayobeba wanafunzi kuwa na kondakta wa kike na mabasi yote yafungwe Camera maalum.
Waziri wa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wanawake na Makundi Maaalum, Dk. Dorothy Gwajima ametoa agizo hilo alipokuwa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Godwin Gondwe katika Shule ya Star Light Pre and Primary School, ambapo mtoto wa miaka sita wa darasa la kwanza anadaiwa kubakwa na kondakta wa gari hilo.
Dk. Gwajima amesema “Watuhumiwa kwa sasa wapo ndani na wameshapanda mahakamani, pongezi wote waliowajibika haraka kesi inaendelea,” amesema Gwajima.
“Na hapa hakuna cha gharama kuongezeka maana jinsia tu ndio inabadilika. Hii itawezesha ulinzi imara kwa mtoto wa kwanza kuchukuliwa na wa mwisho kurejeshwa,” amesema na kuongeza.
“Huko mbele kuna haja ya kufunga camera kwenye mabasi ya shule tunaangalia uwezekano. Lazima wateja walindwe yaani mtoto ni mteja jamani inakuwaje analipia huduma halafu anafanyiwa vitendo vya kikatili?” amehoji.
Tamko hilo la Serikali linakuja ikiwa ni siku chache baada ya kusambaa kwa taarifa katika mitandao ya kijamii inayosema ‘Dereva na anko wabaka mtoto wa miaka sita’