Serikali yaagiza mamlaka husika kuwachukulia hatua wafanyabiashara waliopandisha bei za vifaa vya ujenzi na bidhaa nyingine muhimu

Kumbe mamlaka na serikali ni vitu viwili tofauti maana naona serikali inaiagiza mamlaka .

Tusijesikia tu serikali ikiilaumu mamlaka.
 
Serikali mara hii imesha sahau kuwa yenyewe ndio ilianza kuwashawishi wafanya biashara kupandisha bei za bidhaa kwa kuongeza kodi na tozo kwenye mafuta na bidhaa nyingine? Au wamesahau? Huyu kijaju ni mwehu?
 
Wanyonge tunaumizwa sn
 
Dk Ashatu Kijaji, na wengine wa jinsia hii hii wamepewa wizara muhimu ila performance zao na brain workability zao very low.
Wananchi wapimpiga kimya na machungu yao
 
dah ! nimelazika kununua nondo milimita 12 kwa sh. elfu 28 na ciment kwa elfu 21 maana hakuna namna 😔
 
Dk Ashatu Kijaji, na wengine wa jinsia hii hii wamepewa wizara muhimu ila performance zao na brain workability zao very low.
Wananchi wapimpiga kimya na machungu yao
Naomba kuuliza.
Hivi waziri Kama huyu akifika ofisini kwake hua anadhughulika na mafaili gani? Au yanayo husu Nini?
Wa nishati tunajua Yuko bize na shirika la Maharage, je huyu? Au yule wa jinsia na wazee😂
Sijaona hata siku moja akimpongeza Malisa kwa anavyofanya kazi yake waziri kwa ufanisi.
 
dah ! nimelazika kununua nondo milimita 12 kwa sh. elfu 18 na ciment kwa elfu 21 maana hakuna namna 😔
Kaka jiongeze nunua milimita 16 uondoe usumbufu baadae. Nondo za siku hizi sio nondo tulizozoea.
16 itakula kwako. Talking from experiece
 
Shida iko ngazi za juu hao wanaoleta kutoka china na india huko mimi mfanya biashara mdogo nauza mali yangu kulingana na nilivyoinunua sokoni huko
 
Waziri wa viwanda na biashara Dr Kijaji amezitaka mamlaka zinazohusika kuwachukulia hatua wafanyabiashara waliopandisha bei za Soda, Cement, Nondo na bidhaa nyingine kinyume cha utaratibu.

Dr Kijaji amesema uchunguzi umeonyesha kuwa wakati bidhaa hizo zinapandishiwa bei gharama za uzalishaji zilikuwa chini na hakukuwa na sababu yoyote ile ya kuongeza bei.

Source: ITV habari

========

Serikali imeziagiza mamlaka zote za udhibiti kuchukua hatua kali dhidi ya walimbikizaji na wauzaji kupitia mlango wa nyuma (black market) wanaosababisha bei za bidhaa kupanda sokoni ili kuhakikisha bidhaa zinafika sokoni kwa wakati na bei shindani.

Agizo hilo limetolewa leo Jumatatu Februari 7, 2022 na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Dk Ashatu Kijaji wakati akitoa tathimini ya mwenendo wa uzalishaji, usambazaji na bei za vifaa vya ujenzi na bidhaa nyingine muhimu nchini.

“Ninawaelekeza wazalishaji na wafanyabiashara wa vifaa vya ujenzi kushusha mara moja bei za bidhaa walizopandisha kiholela na kuuza bidhaa bila kuzingatia gharama halisi za uzalishaji na usambazaji,” alisema.

Pia amewaagiza wazalishaji wa vifaa vya ujenzi kuweka mifumo mizuri ya usambazaji wa vifaa ili kuzuia kupanda kwa bei kunakoweza kuzuilika.

Dk Kijaji amewataka maofisa biashara wa mikoa kote nchini waendelee kufuatilia kwa karibu mwenendo wa bei za bidhaa mbalimbali kwenye maeneo yao na kuwasilisha taarifa hizo mara kwa mara kwenye wizara hiyo kupitia ofisi za makatibu tawala mikoa ili itakapobidi hatua stahiki zichukuliwe kwa wakati.

Amesema tathimini iliyofanyika nchini imwegundua kuwa ongezejko holela la bei ya vifaa vya ujenzui hususan saruji na nondo linasababishwa na wazalishaji wa bidhaa husika kufanya uzalishaji banifu.

Pia amesema ongezeko hilo wamebaini limesababishwa na kutokuwa na mfumo wa wazi wa usambazaji wa bidhaa kutoka kiwandani mpaka kumfikia mlaji wa mwisho.

“Gharama halisi za uzalishaji wa saruji haiakisiwi katika bei ya saruji iliyopo sokoni ikilinganishwa na uwiano huo katika nchi jirani na kwingineko duniani,”amesema.

Aidha, amesema wamebaini kuwa ongezeko la bei ya saruji na nondo halina uwiano halisi na gharama za usafirishaji na usambazaji na bei ya saruji iliyopo sokoni haina uhusiano na mwenendo wa nguvu za utashi wa mlaji na ugavi.

Dk Kijaji amesema kuna ucheleweshaji wa makusudi kwa utoaji wa saruji kutoka viwandani kwenda kwa wasambazaji na wanunuzi wa ndani hususani wale wasambazaji na wanunuzi wadogo ambao tayari wanakuwa wamekwisha lipia saruji husika tofauti na wanunuzi wa nje ambao hupatiwa saruji kwa urahisi zaidi.

Amesema pamoja na mambo mengine hali hiyo imesababisha wasambazaji kupandisha bei za saruji ili kufidia gharama zilizotumika kuchukua mzigo.

Chanzo: Mwananchi
Kuna siku Tanzania hii itabidi turudi tuanze mwanzoni tulikotoka baada ya Uhuru. Wakati wa Awamu ya tatu ya Serikali, Mheshimiwa Mkapa alikwisha jenga utaratibu wa sheria ambazo zingesimamia Uchumi wa soko ambao ndio sera tuliyonayo sasa. Sheria ya Ushindani inahusu sekta za uchumi ambazo zinaweza kushindana na Sheria 4 za Udhibiti kwa ajili ya sekta ambazo kwa mantiki zake za uzalishaji na usambazaji haziwezi kushindanishwa, kwa mfano; Usambazaji Umeme, barabara, bandari, maji.
Maudhui ya namna ya kuendesha hizo sheria zote 5 ni shirikishi kwa kuhusisha taasisi za wazalishaji (Private sector), taasisi za mlaji (Consumer) na Serikali yenyewe. Pia uteuzi wa viongozi wakuu na uwajibikaji katika uendeshaji wa sekta hizo ni shirikishi kwa mujibu wa sheria na una masharti ya viongozi kuchaguliwa kupitia matangazo ya nafasi na usaili kisha Serikali kuwa na usemi wa mwisho kati ya majina yanayopendekezwa. Nia ilikuwa sekta hizo ziwe uongozi usiotiliwa mashaka; wenye sifa na weledi kadri ya wataalam tulio nao nchini, na siyo uteuzi! Lakini kama tulivyo Watanzania hatufuati sheria zetu wenyewe; pamoja na Serikali yenyewe ambaye ndiye mwanzilishi na msimamizi mkuu wa sheria zote! Tunaendesha uchumi wa soko kwa kutumia vigezo vya Ujamaa. Tumeanza kuteua tunaowaoenda!
Suala la bei kupanda pamoja kwa bidhaa zinazoshindana si jambo la kawaida. Kwanza, lazima kuchunguza kama washindani wanapanga hizo bei; wakifanya hivyo kosa ni sawa na kupanga matokeo ya mechi za mpira? Kama wanafanya hivyo kuna adhabu kali kweli kweli kwenye sheria zetu hizi hizi za Tanzania. Kwa hiyo tangazo la Waziri wa Viwanda linasikitisha kama vile hajui uchumi unaendeshwaje au hakuna wataalam wa kumweleza kwa undani suala hili. Pia Rais wetu hajaelezwa kuwa FCC, EWURA nk viongozi hawateuliwi kama U DC, U Waziri nk. Kuna mchakato wa kisheria ndipo mwishowe unamteua aliyependekezwa, ambaye atakuwa ameridhiwa na mzalishaji, mlaji na Serikali yenyewe. Wengi wa wanasheria Tanzania hawajui kuwa utaratibu shirikishi wanaoulilia kwenye sekta mbalimbali nyeti upo kwenye baadhi ya sheria na unatakiwa tu uwe extended na kuurekebisha kufuata mazingira halisi; kisha ufuatiliwe katika utekelezaji.
Utaratibu wa kufuata mchakato wa uteuzi na masharti mengine ulizimwa awamu ya tano ambapo inawezekana Serikali ilianza kuvunja sheria zake yenyewe. Viongozi wa serikali pia mjifunze kwanza kabla ya kutoa matamko ambayo hayatekelezeki. Pia ni faida kwa serikali kiuendeshaji kuwa na vyombo vya uwakilishi wa wazalishaji na mlaji vyenye uwezo; vinarahisisha utendaji wa Serikali kuwa na taarifa sahihi kwenye uchumi wakati wote. Ndivyo uchumi wa soko unavyoendeshwa. Vyombo hivyo vinatakiwa vijengwe viwe na nguvu badala ya kufanya mbinu ya kuvidhoofisha kimkakati kama inavyotokea kwenye vyama vya siasa! Haya ni maelezo na ushauri tu kwa watu wanaopenda kuelewa. Kila la kheri Tanzania!
 
Waziri wa viwanda na biashara Dr Kijaji amezitaka mamlaka zinazohusika kuwachukulia hatua wafanyabiashara waliopandisha bei za Soda, Cement, Nondo na bidhaa nyingine kinyume cha utaratibu.

Dr Kijaji amesema uchunguzi umeonyesha kuwa wakati bidhaa hizo zinapandishiwa bei gharama za uzalishaji zilikuwa chini na hakukuwa na sababu yoyote ile ya kuongeza bei.

Source: ITV habari

========

Serikali imeziagiza mamlaka zote za udhibiti kuchukua hatua kali dhidi ya walimbikizaji na wauzaji kupitia mlango wa nyuma (black market) wanaosababisha bei za bidhaa kupanda sokoni ili kuhakikisha bidhaa zinafika sokoni kwa wakati na bei shindani.

Agizo hilo limetolewa leo Jumatatu Februari 7, 2022 na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Dk Ashatu Kijaji wakati akitoa tathimini ya mwenendo wa uzalishaji, usambazaji na bei za vifaa vya ujenzi na bidhaa nyingine muhimu nchini.

“Ninawaelekeza wazalishaji na wafanyabiashara wa vifaa vya ujenzi kushusha mara moja bei za bidhaa walizopandisha kiholela na kuuza bidhaa bila kuzingatia gharama halisi za uzalishaji na usambazaji,” alisema.

Pia amewaagiza wazalishaji wa vifaa vya ujenzi kuweka mifumo mizuri ya usambazaji wa vifaa ili kuzuia kupanda kwa bei kunakoweza kuzuilika.

Dk Kijaji amewataka maofisa biashara wa mikoa kote nchini waendelee kufuatilia kwa karibu mwenendo wa bei za bidhaa mbalimbali kwenye maeneo yao na kuwasilisha taarifa hizo mara kwa mara kwenye wizara hiyo kupitia ofisi za makatibu tawala mikoa ili itakapobidi hatua stahiki zichukuliwe kwa wakati.

Amesema tathimini iliyofanyika nchini imwegundua kuwa ongezejko holela la bei ya vifaa vya ujenzui hususan saruji na nondo linasababishwa na wazalishaji wa bidhaa husika kufanya uzalishaji banifu.

Pia amesema ongezeko hilo wamebaini limesababishwa na kutokuwa na mfumo wa wazi wa usambazaji wa bidhaa kutoka kiwandani mpaka kumfikia mlaji wa mwisho.

“Gharama halisi za uzalishaji wa saruji haiakisiwi katika bei ya saruji iliyopo sokoni ikilinganishwa na uwiano huo katika nchi jirani na kwingineko duniani,”amesema.

Aidha, amesema wamebaini kuwa ongezeko la bei ya saruji na nondo halina uwiano halisi na gharama za usafirishaji na usambazaji na bei ya saruji iliyopo sokoni haina uhusiano na mwenendo wa nguvu za utashi wa mlaji na ugavi.

Dk Kijaji amesema kuna ucheleweshaji wa makusudi kwa utoaji wa saruji kutoka viwandani kwenda kwa wasambazaji na wanunuzi wa ndani hususani wale wasambazaji na wanunuzi wadogo ambao tayari wanakuwa wamekwisha lipia saruji husika tofauti na wanunuzi wa nje ambao hupatiwa saruji kwa urahisi zaidi.

Amesema pamoja na mambo mengine hali hiyo imesababisha wasambazaji kupandisha bei za saruji ili kufidia gharama zilizotumika kuchukua mzigo.

Chanzo: Mwananchi
Serikali inampangia bei mfanya biashara? Wakitaka waanzishe maduka yao ambamo watauza kwa bei nafuu. Au waagize nyingi ambazo watauza kwa masharti ya bei angalizi.

Amandla...
 
Na wewe waziri kazalishe Vifaa vyako uuze bei Cheee,,, Ule kwa urefu wa kamba yako..

Vifaa haviwezi shuka kwa matamko tu.
 
Waziri wa viwanda na biashara Dr Kijaji amezitaka mamlaka zinazohusika kuwachukulia hatua wafanyabiashara waliopandisha bei za Soda, Cement, Nondo na bidhaa nyingine kinyume cha utaratibu.
Hii wizara ni nyeti kwa uchumi wetu, waziri wake anatakiwa mtu mwenye uzoefu na uwezo wa masuala ya biashara na sio kuangalia jinsia na hijab tu
 
Back
Top Bottom