Serikali Yaainisha Mikakati ya Kuwawezesha Vijana Kushindana Kwenye Soko la Ajira

Serikali Yaainisha Mikakati ya Kuwawezesha Vijana Kushindana Kwenye Soko la Ajira

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

maxresdefaultcvfgty.jpg

BUNGE limeelezwa mikakati mitano inayofanywa na serikali katika kukabiliana na tatizo la ajira kwa vijana nchini na namna kumudu ushindani kwenye soko la ajira.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema hayo Februari 10, 2025 bungeni wakati akijibu swali la Mbunge wa Mpendae (CCM), Mhe. Toufiq Turky aliyehoji kuna mpango gani wa kuwandaa vyema vijana waweze kushindana katika soko la ajira ndani na nje ya Tanzania ili kukabiliana na upungufu wa ajira nchini.

Akijibu swali hilo, Waziri Kikwete ametaja mipango ya serikali katika kuwaandaa vijana ili kumudu ushindani katika soko la ajira ndani na nje ya nchi.

Mhe. Kikwete amesema, mipango hiyo ni pamoja na kubuni na kutekeleza programu maalum zinazowawezesha vijana kujifunza kwa vitendo kupitia sekta zinazozalisha ajira kwa wingi kama vile sekta ya kilimo kupitia programu ya Jenga Kesho iliyobora (BBT), ujasiriamali, na madini kupitia Programu ya Mining for a better Tommorrow (MBT).

Pia, amesema kufanya maboresho ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 Tolea la Mwaka 2023 ambayo yanasisitiza mafunzo kwa kuandaa wataalamu.

“Kupitia ujenzi wa miundombinu ya Kimkakati muhimu inayochochea uchumi, vijana wameajiriwa na kunufaika na urithishwaji ujuzi kutoka kwa wataalamu wa nje mfano ujenzi wa Bwawa la umeme la Mwalimu Nyerere na barabara za mwendokasi (BRT),” amesema Mhe. Kikwete

Kadhalika, amesema Serikali itaendelea kubuni na kutekeleza programu ya kukuza ujuzi ambayo inalenga kukuza ujuzi kwa nguvu kazi ili kuwezesha vijana kushindana katika soko la ajira mfano mafunzo ya kuongeza ujuzi kwa wafanyakazi waliopo kazini na kwa wajasiriamali.

Waziri Kikwete amesema mkakati mwingine ni kuweka msisitizo kwenye matumizi ya TEHAMA katika kuzalisha fursa nyingi za ajira kwa vijana.

“Napenda kulihakikishia Bunge lako Tukufu kwamba serikali itaendelea kusimamia na kuhakikisha vijana wanaandaliwa ili wapate ujuzi unaohitajika katika soko la ajira na hivyo kumudu ushindani wa ajira,” amesema.
 

Attachments

  • GjcDwetWoAI5eR3.jpg
    GjcDwetWoAI5eR3.jpg
    162.9 KB · Views: 2
Jamaa Mmoja Mganda aliwahi kuniambia kuwa Tanzania tuna database nzuri Sana ya kila kitu! Tuna maandiko matamu Sana Sana na MENGi yako kwenye internet na website za taasisi husika BUT hakuna hata moja linalotekelezwa.
Nikakumbuka enzi za Mkurabita, Mkukuta, Kilimo kwanza, na recently Miradi ya kuwapa ng'ombe na vitalu Vijana wahitimu WA SUA, Miradi ya kilimo Dodoma ya Vijana Chini ya Msomali Bashe......

Yote inavutia Sana, kuna siku nilitembelea website ya TPDC, TIB, na nyingine, kule kuna maandiko ya Miradi mikubwa Tu na baadhi imeshafanyiwa Hadi feasibility study na maeneo yametengwa......

Nikakumbuka tena miaka minne iliyopita kila halmashauri ilikua inatangaza fursa zinazopatikana kwenye halmashauri husika.

Nilivyomaliza na Mimi kwa kuwa pia ni Mtanzania, nikapiga goti nikamshukuru MUNGU nikajiapiza kuwa sijatoka Tanzania.....na Hadith ikaishia hapo
 
Aanze yeye kuonyesha njia, mara hii ampishe mwengine yeye aje tujengenae kesho pamoja.
 
Back
Top Bottom