Tena jambo hilo ni kijume na taratibu na sheria za NEC, hupaswi kusema ulifanya nini bali utafanya nini ili wagombea wote wawe level moja, tuchane chane upuuzi huo.Nimeona vipeperushi vinaelezea mafanikio ya awamu ya tano. Vipeperushi hivi vinakuja baada ya joto la uchaguzi kuwa kali na kuonekana ngoma si kama tulivyoivalia kibwebwe.
Ushauri: CCM achaneni na mliyofanya, jikiteni kuwaeleza wananchi mtakayofanya. TBC kwa miaka mitano imekuwa inatueleza mliyofanya tena kwa picha na video. Kama hatukuelewa kupitia TBC ni vigumu sana kuelewa vipeperushi kwa sababu sisi hatuna tabia ya kujisomea.