Unajua kwa nini watu hawalipi kodi Mkuu? ni kwa sababu ya mlundikano wa kodi. Mfano; Mtu mwenye Duka la Rejareja anatakiwa kulipa kodi zifuatazo:
1. Kodi ya TRA
2. Kodi ya Leseni ya Biashara
3. Kodi ya Service Levy
4. Kodi ya TBS
5. Kodi ya Usafi wa Mazingira
6. Kodi ya Pango (TRA)
Kwa uchache kodi za Mfanyabiashara mmoja tu ni hizo.
Hapo unategemea utalipa kodi au utakwepa kodi?
Mbaya zaidi ukienda kulipa kodi Wafanyakazi wa TRA, Jiji au Manispaa na TBS wana nyodo ni hatari. Kukuprintia tu control number inachukua siku nzima!