Serikali yaanzisha kodi mpya kwenye miamala ya fedha kupitia Benki

Serikali yaanzisha kodi mpya kwenye miamala ya fedha kupitia Benki

Kwa hiyo hutaki au na je imeongezeka, imepungua au makato mapya na ni miamala ipi inahusika? Majibu tafadhali ndugu mleta hoja[emoji848]
Hana majibu maana yeye yupo gizani mara baada ya jiwe kumtoka bila kutarajia
 
Kweli kila zama na kitabu chake.
Kwenye Nishati boss wake anatembea na mitungi ya gesi ya kilo 6 hanamasisha matumizi ya gesi. Ukiuliza gesi hiyo iko wapi? Jibu. Mo gesi au Taifa gesi.
Nchi gesi iliuza. Kwahiyo nchi imekuwa mpiga debe wa Mwenye gesi
 
Madelu bana ile LC 300 anayotembelea inamsahaulisha shida tulizo nazo
 
Siipendi CCM, ila suala la kulipa kodi, kuchangia maendeleo ya nchi ni jukumu la kila Mtanzania.
Amani tuliyonayo leo kuna watu wanalipwa mishahara na motisha mbalimbali kuhakikisha tunalala bila bugudha.
 
Nchi ngumu hiii .kwanza zile tozo za kwenye simu walidai wanajenga madarasa .ina maana hayo madarasa bado hayajaisha ili wazitoe hizo tozo??? Tena tozo za bank ?? Agrrrr mtafnya wizi wa majumbani urudi kwa kasi mana tutaweka hela kwenye magodoro sasa tuvamiwe.........

Serikali badala ya kupunguza maumivu wao ndio kwanza wanawaza tutawanyonya vipi wananchi wetu....
 
😆😆 Haya maneno ya kijinga mliwahi sema hata kwenye tozo za miamala ya simu.. Uchumi sio hisia ni hesabu..

Matokeo yake yakawa hivi 👇
Huenda ni maneno ya kojijga ila nadhani hukuwa unapata report za makapuni ya simu ndo maana unaona mbeno ya kijinga
 
Madawa watanunua na mawe..?

Barabara watajenga kwa kutumia nini

Mishahara ya watumishi mnayotaka iongezwe pesa itatoka wapi...?

Ajira mpya mnazolilia kila siku unadhani hao watu tutawalipa upepo..?

Huduma zote za kijamii zinategemea kodi zetu mimi na wewe
Ujinga ni mzigo.

Haya niambie serikali gani ya Tanzania iliendesha bajeti yake kwa TOZO?

Kilichobaki ni kuanza kupekuliwa majumbani na kukwapuliwa vijisenti kwenye vibubu.
 
Watanzania kelele nyingi tunapopigiliwa msumari wa moto ukipoa tunasahau bila kujua msumari bado upo mwilini.

Kama tozo kwenye miamala ya simu watu walisema hatutumii tena mpesa lakini leo hii miamala ya simu bado inaendelea vizuri tu na serikali inaendelea kutukamua tozo.
 
Kusema kweli Mimi nasikia hasira na Serikali hii.Hawajui maana ya Kodi.na je wajifunza kutoka nchi nyengine? Mwisho wake watu hawataweka hela bank.unazichimbia ardhini
 
Yaani mfano umelipwa mshahara na hio hio serikali ukaingia benki halafu unaenda benki au atm kutoa hela serikali tena wanakukata TOZO(Hapo kama bank nao huwa wanatoza unaliwa huku na huku)
Si afadhali wewe umeajiriwa Serikalini.hii inaitwa recycling phenomenon
 
Bank SIO msaada ni jini mufirith.
Hela zako lala nazo ndani Kama Mhindi tu.
 
Uongo mtupu

Siipendi CCM, ila suala la kulipa kodi, kuchangia maendeleo ya nchi ni jukumu la kila Mtanzania.
Amani tuliyonayo leo kuna watu wanalipwa mishahara na motisha mbalimbali kuhakikisha tunalala bila bugudha.
Nakubaliana na wewe kabisa
Kulipa kodi ni jukumu la kila mwananchi ila unalipaje na kwa kiasi gani; kwa nchi masikini inakuwa na different approach......
 
Hapo serikali inatakiwa kutafuta njia mbadala ya kuongeza mapato,maana mtanzania mwenye kipato cha chini ndo anaumia zaidi mfano umetoa hela kwenye cm umekatwa kodi, unaenda kupanda gari stand kubwa unalipa kodi haya na kama unashikia stand kubwa pia unalipa kodi,hata kama tutafuta maendeleo lakini hapaswi kuumizwa mtu, hivyo naona serikali ingeliangalia hili swala la kodi kwa jicho la pili
 
Back
Top Bottom