Kigoma ni lazima iangaliwe kwa jicho pevu kwa sababu ni sehemu muhimu sana kwa usalama wa nchi yetu. Tusilaumu tu kwa sababu za kisiasa. Usalama wa Tanzania ni mihimu kuliko chochote ukijuacho. Tanzania inazungukwa na nchi jirani za Msumbiji, Malawi, Zambia, DR Congo, Burundi, Rwanda, Uganda na Kenya. Lakini kati ya hizo zote Burundi na Congo ziko kwenye hali tete kiusalama na zote hizo ziko karibu sana na mkoa wa Kigoma. Hapo unaweza kuona umuhimu wa kiusalama kwa mkoa wa Kigoma. Lakini pia Kigoma ndo mkoa pekee wenye lango linalounganisha nchi tatu za nje ambazo ni Burundi, Congo na Zambia hivyo kuwa na uwezekano mkubwa wa kuwa na wageni wengi wasio raia. Hivyo basi kwa kila raia wa Tanzania anayetoka Kigoma lazima uwe nae makini sana kwani anaweza kuwa katoka nje ya nchi akajifanya anatoka Kigoma.
Lakini pia mkoa wa Kigoma unapakana na nchi zenye matatizo ya kiuchumi kiasi kwamba raia wengi wa nchi hizo hupenda sana kukimbilia Kigoma kutafuta kazi na vibarua vya kufanya kukidhi mahitaji yao. Ni kama ilivyo kwa South Africa inavyovutia wahamiaji wengi kutoka nchi zote za kusini mwa Africa.
Mimi ni mzaliwa wa Kigoma nafahamu maisha ya huko. Mara nyingine kumtofautisha muha wa Muyama kwetu na Kayogoro au Makamba Burundi inakuwa vigumu sana. Ama kumtofautisha Mbembe wa Helembe, Sunuka, Sibwesa na Mbembe wa Moba, Baraka na hata Kalemii au Uvira Congo inakuwa vigimu.
Ni kwa misingi hiyo kama nchi huru tunapaswa kuwa waangalifu kwenye uraia wa wananchi wetu.
Watu wa Kigoma sisi kama raia halal wa nchi hii tunao wajibu wa kuilinda mipaka yetu na kuwachunguza watu wasio raia miongoni mwetu.
Hatuna nchi nyingine Tanzania ndo nchi yetu.
Nchi jirani nao wana utaratibu wao wa kuwashughulikia watu wasio raia wa nchi zao.
Kigoma tusigombanishwe na serikali yetu na wajinga wachache kwamba serikali haitupendi. Tuendelee kuipenda na kuilinda nchi yetu kuanzia Mashariki mpaka Mafharibi na kutoka Kusini mpaka Kaskazini.
Karibuni kijijini kwetu Muyama mpakani kabisa na Burundi.
Aksante.