Tetesi: Serikali yadaiwa kumvua uraia Padri wa Kanisa Katoliki

Tetesi: Serikali yadaiwa kumvua uraia Padri wa Kanisa Katoliki

kama wewe ni mtanzania,huwezi kushindwa kuonesha walipozikwa wazee wako,muite Helsinki nae awe mkimbizi wa kiuchumi
Kwani viongozi walio tangulia hawakuwa wanawajua kuwa ni warundi?mbona kuna wasomali wamejaa lkn hamuwaandami kiasi hicho?
 
Zamani makaburi yalikuwa hayajengewe kama sasa. Utakuta wameshajenga majumba ama shamba la mazao. Kwa wale wenyeji wa Arusha ilipo stand ndogo ilikuwa eneo la makaburi ya serikali kwa sasa ni stand ya vihaice pamoja na maduka ukute sasa babu yako alizikwa hapo sijui utaonyesha nini
 
Kigoma ni lazima iangaliwe kwa jicho pevu kwa sababu ni sehemu muhimu sana kwa usalama wa nchi yetu. Tusilaumu tu kwa sababu za kisiasa. Usalama wa Tanzania ni mihimu kuliko chochote ukijuacho. Tanzania inazungukwa na nchi jirani za Msumbiji, Malawi, Zambia, DR Congo, Burundi, Rwanda, Uganda na Kenya. Lakini kati ya hizo zote Burundi na Congo ziko kwenye hali tete kiusalama na zote hizo ziko karibu sana na mkoa wa Kigoma. Hapo unaweza kuona umuhimu wa kiusalama kwa mkoa wa Kigoma. Lakini pia Kigoma ndo mkoa pekee wenye lango linalounganisha nchi tatu za nje ambazo ni Burundi, Congo na Zambia hivyo kuwa na uwezekano mkubwa wa kuwa na wageni wengi wasio raia. Hivyo basi kwa kila raia wa Tanzania anayetoka Kigoma lazima uwe nae makini sana kwani anaweza kuwa katoka nje ya nchi akajifanya anatoka Kigoma.

Lakini pia mkoa wa Kigoma unapakana na nchi zenye matatizo ya kiuchumi kiasi kwamba raia wengi wa nchi hizo hupenda sana kukimbilia Kigoma kutafuta kazi na vibarua vya kufanya kukidhi mahitaji yao. Ni kama ilivyo kwa South Africa inavyovutia wahamiaji wengi kutoka nchi zote za kusini mwa Africa.
Mimi ni mzaliwa wa Kigoma nafahamu maisha ya huko. Mara nyingine kumtofautisha muha wa Muyama kwetu na Kayogoro au Makamba Burundi inakuwa vigumu sana. Ama kumtofautisha Mbembe wa Helembe, Sunuka, Sibwesa na Mbembe wa Moba, Baraka na hata Kalemii au Uvira Congo inakuwa vigimu.

Ni kwa misingi hiyo kama nchi huru tunapaswa kuwa waangalifu kwenye uraia wa wananchi wetu.
Watu wa Kigoma sisi kama raia halal wa nchi hii tunao wajibu wa kuilinda mipaka yetu na kuwachunguza watu wasio raia miongoni mwetu.
Hatuna nchi nyingine Tanzania ndo nchi yetu.
Nchi jirani nao wana utaratibu wao wa kuwashughulikia watu wasio raia wa nchi zao.
Kigoma tusigombanishwe na serikali yetu na wajinga wachache kwamba serikali haitupendi. Tuendelee kuipenda na kuilinda nchi yetu kuanzia Mashariki mpaka Mafharibi na kutoka Kusini mpaka Kaskazini.

Karibuni kijijini kwetu Muyama mpakani kabisa na Burundi.
Aksante.
 
Inauma miongoni mwa Mapadre ninaowapenda na kuwakubali sana Ni katibu Mkuu Padre Raymond Saba inauma sana unafiki wa baadhi ya Maaskofu wakatoliki kuficha na kushindwa kuusema ukweli huyo anaeagiza wahoji uraia ni raia wa wapi
SIKU MOJA DINI ZITAKUFA NA NDIPO DUNIA ITAKUWA SALAMA.
 
Inauma miongoni mwa Mapadre ninaowapenda na kuwakubali sana Ni katibu Mkuu Padre Raymond Saba inauma sana unafiki wa baadhi ya Maaskofu wakatoliki kuficha na kushindwa kuusema ukweli huyo anaeagiza wahoji uraia ni raia wa wapi
Warundi wanawafukuza watanzania nchini kwao
 
Kila likija hili swala la uraia najaribu kwenda kutembelea walipolala babu na bibi zangu (makaburini) ili nisije kupasahau .
 
Msaidie kupata asylum nae aishi huko ughaibuni!
nitakuwa wa mwisho kuamini kwamba upo sawa kichwani wewe. kichwa kimejaa usaha kama wale wabunge kina waitara wanaohama vyama kisa tu ya kumkomoa mbowe bila kusahau kuwa wengine waliwachagua bila hata kuwa na vyama. jitafakari mkuu. hata kama uligelezea mitihani lakink ficha kudesa kwako huku kwenye mitandao
 
Niwakati muafaka kwenda kulitafuta na kuliimarisha kaburi la Babu.
 
Huyu mh t atawamaliza wenzao ila walisema wachaga in watu wa baya
 
Anaandika Ansbert Ngurumo:

UTAWALA wa Rais John Magufuliumeendelea kujizolea kashfa ya kutumia “silaha ya uraia” katika kukomoa raia, kuzima sauti za wananchi na kulipiza visasi.

Zamu hii serikali imemnyang’anya uraia Padri Raymond Saba, wa Kanisa Katoliki, ambaye hadi wiki chache zilizopita alikuwa Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC). Padri Saba ni mzaliwa wa Kigoma.

Tunazo taarifa za uhakika kuwa idara ya uhamiaji ilimchukulia hatua hiyo akiwa katibu mkuu wa TEC. Hiyo ndiyo sababu iliyozingatiwa na TEC kumwondoa katika wadhifa huo na kuteua Dk. Charles Kitima.

Maaskofu walipobadili uongozi wa juu – rais na makamu wake ambao walikuwa wanamaliza muda wao – wakamwondoa na katibu mkuu. Kwa sababu kanisa halikupiga kelele, mbele ya umma suala hili lilionekana kama mabadiliko ya kawaida tu ya uongozi, lakini kulikuwa na sababu zilizotokana na msukosuko wa serikali na vyombo vyake.

Serikali, kupitia idara ya uhamiaji, imekamata pasipoti ya Padri Saba ikimtuhumu kuwa si Mtanzania, na inamtaka athibitishe uraia wake. Miongoni mwa mambo ambayo wamekuwa wanataka afanye ni kuwaonyesha makaburi ya bibi na babu zake – jambo ambalo wamekuwa wanalifanya kwa kila wanayemtuhumu kuwa si raia.

Sababu ya serikali kumtia msukosuko padre huyo ni waraka wa kichungaji wa TEC ambao ulitolewa katika kipindi cha kwaresima mwaka huu, yeye akiwa katibu mkuu. Waraka huo, miongoni mwa mambo mengine, ulizungumzia kutetereka kwa amani ya nchi na kutaka viongozi wa nchi wajitafakari.

Serikali ilichukizwa na waraka huo, na baadhi ya viongozi wa kisiasa walijiapiza kulipiza kisasi kwa kukomoa au kuumbua baadhi ya viongozi wa dini kwa namna mbalimbali. Wapo waliozushiwa kutelekeza watoto. Wapo wanaotafutiwa kesi. Wapo wanaozuiwa kusafiri nje ya nchi. Wapo wanaopigwa kwa uraia – hasa watokao katika maeneo ya mipakani. Wengi wao wanaumia kimya kimya.

Msukosuko dhidi ya Padri Saba ulifikia kilele katika kipindi ambacho Mwigulu Nchemba, aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani, alisimamisha kazi Merlin Komba, msajili wa vyama katika wizara yake ambaye alikuwa ameagizwa na Ikulu kuandika barua za maonyo kwa Kanisa Katoliki na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT).

Barua ya serikali kwa TEC haikuvuja, lakini serikali ilikerwa na mawasiliano ya kanisa, na msimamo wa Padri Saba katika majibu ambayo kanisa lilitoa kwa maandishi, huku Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa, aliyekuwa rais wa TEC akisumbuliwa na kuitwa ajieleze serikalini.

Baada ya maaskofu kubaini msukosuko na usumbufu uliokuwa unamkabili Padri Saba walimwondoa kwenye nafasi hiyo ili suala hilo lisiwe sababu ya nyongeza ya serikali kuendelea kuandama kanisa. Baadhi ya wapambe wa Rais Magufuli walichekelea alipoondolewa wakisema, “tumemkomoa.”

Serikali inaendelea kushikilia pasipoti yake kama inavyoshikilia pasopoti za wengine inaowachapa “kiboko cha uraia” kwa sababu za kisiasa.

Katika muda mfupi wa madaraka ya Rais Magufuli, suala la uraia limegeuzwa silaha ya kisiasa na linaendelea kuumiza wananchi kadhaa, hasa wanaokosoa serikali au wasiokubaliana na mambo kadhaa inayotenda.

Orodha ni ndefu lakini wengine wanaotajwa na vyombo vya habari, mbali na Padre Saba, ni hawa wafuatao:

Askofu Zakaria Kakobe wa Full Gospel Bible Fellowship. Alitoa mahubiri makali katika Krismasi ya 2017, akaonya serikali juu ya dhuluma, hasa mauaji ya raia. Alimtaka rais atubu. Askofu Kakobe alitiwa misukosuko na polisi na Mamlaka ya Mapato Tanzania. Walipokosa jinsi ya kumtia hatiani, idara ya uhamiaji iliibua suala la uraia wake. Sasa anachunguzwa uraia.

Aidan Eyakuze mkurugenzi mtendaji wa Twaweza, shirika lisilo la kiserikali ambalo limetangaza matokeo ya utafiti unaoonyesha kuwa umaarufu wa rais miongoni mwa wananchi umeshuka kutoka asilimia 96 (2016) hadi 54 (2018).

Wakati Twaweza walipotangaza kuwa rais alikuwa anapendwa na waanchi kwa asilimia 96 mwaka 2016, serikali haikutilia shaka uraia wa mkurugenzi wake. Ilipotangaza kushuka kwa umaarufu wake, taasisi yake ilisakamwa.

Baadhi ya vijigazeti vinavyofadhiliwa na serikali kwa ajili ya propaganda za kisiasa za CCM, vimekwenda mbali zaidi, vikamtaja kuwa ni mwanachama wa chama cha siasa (Chadema), jambo ambalo taasisi yake imekanusha. Sasa anachunguzwa uraia.

Askofu Severine Niwemugizi wa Jimbo Katoliki la Rulenge. Mwaka 2017 alitoa kauli kuhusu umuhimu wa kuwa na katiba mpya ili hatua nzuri zinazochukuliwa na serikali zizingatie misingi ya katiba badala ya kutegemea uamuzi wa mtu. Rais Magufuli ameshasema kuwa katiba mpya si ajenda yake.

Haikuchukua muda mrefu, idara ya uhamiaji ikaanza kuhoji uraia wa askofu huyo. Bado pasipoti yake imeshikiliwa. Anachunguzwa uraia.

Abdul Nondo, mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Alitoa taarifa kupitia simu yake kuhusu watu waliomteka usiku, wakamsafirisha usiku kucha kutoka Dar es Salaam hadi Iringa.

Kwa kuwa “watu wasiojulikana” ambao wamekuwa wanateka na kupoteza watu wanahusishwa na vyombo vya dola, yalitoka maagizo mengi ya kisiasa yakitaka kijana huyo ashughulikiwe. Serikali imemfumgulia kesi mahakamani. Amesimamishwa masomo chuoni. Anachunguzwa uraia.

Padri Saba, Askofu Kakobe, Eyakuze, na Nondo ni wazaliwa wa Kigoma. Askofu Niwemugizi ni mzaliwa wa Kagera. Orodha ya wanaoshughulikiwa “kimfumo” ni ndefu.

Na kama siyo raia kweli serikali imekosea nini???!!!
 
Wengine hat kuwa na utaratibu wa jujengea makaburi, yale matuta yamesha titia. Tutainyesha nini?
 
unaweza kua sahihi,lakini huyo padri ni mrundi,hapo hata akipiga novena itamrudia hakuna dhulma hapo,ametendewa haki
Tanzania ndio nchi pekee dunia,mgeni anaweza kujichanganya na raia,akapata pasi na kadi ya kura akajifanya mtanzania
Mlijua lini kuwa ni Mrundi
 
Back
Top Bottom