Tetesi: Serikali yadaiwa kumvua uraia Padri wa Kanisa Katoliki

Wengine hat kuwa na utaratibu wa jujengea makaburi, yale matuta yamesha titia. Tutainyesha nini?
Mimi hii habari nadhani huenda inapotosha. Kwanini nasema hivyo? Ni siku chache zilizopita maaskofu walifanya kikao na rais na kulingana na mazungumzo yao baada ya kikao inaonyesha wanaridhika kwa kiasi kikubwa na uongozi wa serikali ya awamu hii. Je, kungekuwa na tatizo kubwa kama hili la padri tena aliyekuwa katibu mkuu wa maaskofu kunyang'anywa uraia kwa sababu tu ya ule waraka wangeonyesha furaha namna ile? I mean maaskofu wote wale wangeweza kuwa wanafiki kiasi kile na kuamua kumsaliti mwenzao?
 
Petro alimkana Yesu mara tatu, pamoja na kiapo chake kwamba asingefanya hivyo.
 
Hii habari imetiwa chumvi sana. Rev Fr Saba ni mmoja wa watu makini sana, msomi na mtu asiyependa makuu. Ni mwalimu mzuri na mnyenyekevu. Ninachompendea zaidi ni ile self determination aliyonayo daima. He did great work hata alipokuwa Roma.

Kama serikali inahoji uraia wake, basi itakuwa ni moja ya serikali za kizwazwa sana, tena serikali iliyotopea.

The church is greater than this government. Kama walishindwa kumshughurikia Gwajima (kama c mtu wa system), basi kwa mkatoliki huyu wanatafuna chuma cha reli kwa meno ya makaratasi!!
 
Serikali inaendelea kushikilia pasipoti yake (Padri Saba) kama inavyoshikilia pasopoti za wengine inaowachapa “kiboko cha uraia” kwa sababu za kisiasa.
Hii umenishtua kumbe Padri alikuwa anafanya siasa? Sidhani kama hii nikazi ya Padri, ninachojua Padri anatunza imani na kuongeza idadi ya waumini. Na mambo mengine yahusuyo dini. TEC nadhani waliona hoja kumuondoa.
Padri Saba, Askofu Kakobe, Eyakuze, na Nondo ni wazaliwa wa Kigoma. Askofu Niwemugizi ni mzaliwa wa Kagera. Orodha ya wanaoshughulikiwa “kimfumo” ni ndefu.
BlackBold: Hapa ama unania ya kumuaharibia Eyakuze, ama habari yako hii ni ya uongo. Ninachojua Eyakuze alisema yeye ni Muhaya, nadhani rekodi zipo hapa JF wakati akitoa maelezo hayo.
 
Haya mambo ya uraia si mchezo.
Kila mmoja akifuatiliwa uraia wake (Hasa uraia wa mababu/bibi) na wasi wasi karibu watanzania wote si raia wa Tanzania. Maana kabla ya makoloni kugawana bara hili, kunafamilia zilikuwa zinaishi sehemu moja, ila mipaka ilipowekwa na wakoloni, basi familia zile ziligawanywa na kuishi sehemu/nchi karibia tatu.
Hao watu wa uamihaji pia nao yawezekana si raia.
 
Huu ni mkwala.
 
nimeona hii trend ya huyu padre inavuma sana, kama ni kweli basi kazi ipo
 
Mimi ni mtanzania original lakini kweli ukiniambia nikuonyeshe kaburi la bibi mzaa baba sijui nitaanzia wapi. Kwa kigezo hichi cha makaburi wengi sii raia.

Criteria zetu ni za karne ya 17
 
Acheni Wafu wazike wafu wenzao. Unamtetea huyo kwani wewe ni askofu? Punguzeni viherehere mtakuja kufa vifo si vyenu
 
Duuh...wapi huko na mwaka gani? Mwenyezi Mungu hujibu Maombi
 
Acheni Wafu wazike wafu wenzao. Unamtetea huyo kwani wewe ni askofu? Punguzeni viherehere mtakuja kufa vifo si vyenu
Aisee Mmteule,

VIONGOZI WENGI WA SERIKALI NDIYO VIHEREHERE , WAKIONGOZWA NA JIWE.
 
Jiwe anajionaa wakati kazaliwa Burundi aahaaa...hatutaki kuongozwa na pua ndefu tena..watanzania amkeni ...
 
vizuri, sasa nikuulize kwanini mtu ahojiwe uraia wake pindi tu akiongea maneno ya kuikosoa siri kali?
 
Ila Kigoma kz ipo uraia wao huwa una mashaka kwa sababu ya mwingiliano Mkubwa na tamaduni zinazofanana na akina kurunziza.Na wao wapunguze ubishi maana ni wabishi kupita kiasi!
Hili siyo tatizo la Kigoma peke yake, mikoa yote ya mipakani tatizo hilo la mwingiliano lipo, Wamasai wa Kenya vs Wamasai wa Tanzania, Wakurya wa Kenya vs wakurya wa Tanzania, Wangoni, Makonde, wanyasa, wagunya, nk
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…