Tetesi: Serikali yadaiwa kumvua uraia Padri wa Kanisa Katoliki

Tetesi: Serikali yadaiwa kumvua uraia Padri wa Kanisa Katoliki

Hakuna mtu mwenye asili ya tanzania, wote hapa ni wahamiaji haramu, kabla ya wazungu kugawa mipaka ya nchi mbalimbali kwa ajili ya makoloni yao most of makabila yalitokea maeneo ya central africa na mengine north africa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Watanzania acheni ushabiki wa kisiasa katika masuala muhimu ya nchi, hususan ya amani, utulivu na usalama. Hao wote waliotajwa wanamizizi katika nchi ambazo zimemwaga damu. Hivyo, wangependa waione TZ inaingia huko. Kumbukeni kwamba, nchi ya kishosharisti ya Urusi, USSR, ilisambaratishwa na Rais Gobachevu, ambaye mizizi yake ipo Marekani. Marekani walimtumia na nchi ya Urusi ikasambaratika. Hivyo, hata kama watu hao walizaliwa TZ, kuna haja ya kuwafuatilia kwa kuna juu ya maneno na vitendo vyao. Uhamiaji fanyeni kazi yenu, msiogope maneno ya wana siasa au wana harakati wa haki za binadamu, hao wanafadhiriwa wa watawala wetu wa zamani.
 
vizuri, sasa nikuulize kwanini mtu ahojiwe uraia wake pindi tu akiongea maneno ya kuikosoa siri kali?
Wanahojiwa kila siku sema tu huwa hupati taarifa mpaka atakaye hojiwa awe ni mtu anayejulikana. Kuna watu wengi sana wanahojiwa kila siku usiku na mchana lakini hupati taarifa. Wahindi, Warabu, Wasomali, Wakongo, Wazungu na wengine wengi. Askari wa uhamiaji ndo kazi zao wakikushuku huwa wanataka uthibitishe uraia wako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nchi ipo kwenye giza nene sana


Nina uhakika leo hii huyu Rais Magufuli akiambiwa akaonyeshe Makaburi ya Babu na Bibi zake huko kwao Geita, I am sure he'll never show nothing...!Kuna tetesi kuwa hata yeye siyo Mtanzania ni Mnyalenge au Intarahamwe toka Rwanda au Burundi...!!!
Hivi huyu Joka Magufuli ana tofauti yoyote na NDULI IDDI AMIN DADA(rip) aliyeitawala Uganda kwa mabavu?
Kilichomwondoa Nduli Idd Amin pia kitamwondoa huyu Joka mwenye sumu kali kwa Uhuru na Demokrasia ya Watanzania...!!!
 
Kwa hiyo anaanza utaratibu nchi nzima kuwaondoa au mpaka utoe tamko fulani ndio uchunguzi uanze
Kiukweli kwa [mtazamo wangu] serikali inafanya mpinduzi makubwa ya kusahihisha utendaji wa watendaji wake bila ya kujali wananchi wametoa matamko gani.

Ukitoa matamko ya kisiasa wakati hauna mtiririko mzuri wa kumbukumbu za uraia wako au ulipaji wa kodi basi ujue una harakisha hayo mapinduzi ya kujisahihisha serikali yakukute haraka sana kuliko wenzio.

Ukitaka siasa hasa za kukosoa wenzio anza kutafuta makaburi ya mababu zako na hakikisha unafuata sheria zote za nchi vizuri. Kwani nawe utaanza kuhojiwa, kukosolewa na kuwajibishwa kwa mapungufu yako kama unavyo wakosoa wenzio na kujaribu kuwawajibisha kwa mapungufu yao. Sasa usipofanya hivyo yakikukuta mapigo mazito usitafute huruma toka kwa jamii/wananchi vinginevyo wewe jali yako kaendelee kufanya shughuli zako za kiroho au kibiashara kimya kimya.
 
Anaandika Ansbert Ngurumo:

UTAWALA wa Rais John Magufuliumeendelea kujizolea kashfa ya kutumia “silaha ya uraia” katika kukomoa raia, kuzima sauti za wananchi na kulipiza visasi.

Zamu hii serikali imemnyang’anya uraia Padri Raymond Saba, wa Kanisa Katoliki, ambaye hadi wiki chache zilizopita alikuwa Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC). Padri Saba ni mzaliwa wa Kigoma.

Tunazo taarifa za uhakika kuwa idara ya uhamiaji ilimchukulia hatua hiyo akiwa katibu mkuu wa TEC. Hiyo ndiyo sababu iliyozingatiwa na TEC kumwondoa katika wadhifa huo na kuteua Dk. Charles Kitima.

Maaskofu walipobadili uongozi wa juu – rais na makamu wake ambao walikuwa wanamaliza muda wao – wakamwondoa na katibu mkuu. Kwa sababu kanisa halikupiga kelele, mbele ya umma suala hili lilionekana kama mabadiliko ya kawaida tu ya uongozi, lakini kulikuwa na sababu zilizotokana na msukosuko wa serikali na vyombo vyake.

Serikali, kupitia idara ya uhamiaji, imekamata pasipoti ya Padri Saba ikimtuhumu kuwa si Mtanzania, na inamtaka athibitishe uraia wake. Miongoni mwa mambo ambayo wamekuwa wanataka afanye ni kuwaonyesha makaburi ya bibi na babu zake – jambo ambalo wamekuwa wanalifanya kwa kila wanayemtuhumu kuwa si raia.

Sababu ya serikali kumtia msukosuko padre huyo ni waraka wa kichungaji wa TEC ambao ulitolewa katika kipindi cha kwaresima mwaka huu, yeye akiwa katibu mkuu. Waraka huo, miongoni mwa mambo mengine, ulizungumzia kutetereka kwa amani ya nchi na kutaka viongozi wa nchi wajitafakari.

Serikali ilichukizwa na waraka huo, na baadhi ya viongozi wa kisiasa walijiapiza kulipiza kisasi kwa kukomoa au kuumbua baadhi ya viongozi wa dini kwa namna mbalimbali. Wapo waliozushiwa kutelekeza watoto. Wapo wanaotafutiwa kesi. Wapo wanaozuiwa kusafiri nje ya nchi. Wapo wanaopigwa kwa uraia – hasa watokao katika maeneo ya mipakani. Wengi wao wanaumia kimya kimya.

Msukosuko dhidi ya Padri Saba ulifikia kilele katika kipindi ambacho Mwigulu Nchemba, aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani, alisimamisha kazi Merlin Komba, msajili wa vyama katika wizara yake ambaye alikuwa ameagizwa na Ikulu kuandika barua za maonyo kwa Kanisa Katoliki na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT).

Barua ya serikali kwa TEC haikuvuja, lakini serikali ilikerwa na mawasiliano ya kanisa, na msimamo wa Padri Saba katika majibu ambayo kanisa lilitoa kwa maandishi, huku Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa, aliyekuwa rais wa TEC akisumbuliwa na kuitwa ajieleze serikalini.

Baada ya maaskofu kubaini msukosuko na usumbufu uliokuwa unamkabili Padri Saba walimwondoa kwenye nafasi hiyo ili suala hilo lisiwe sababu ya nyongeza ya serikali kuendelea kuandama kanisa. Baadhi ya wapambe wa Rais Magufuli walichekelea alipoondolewa wakisema, “tumemkomoa.”

Serikali inaendelea kushikilia pasipoti yake kama inavyoshikilia pasopoti za wengine inaowachapa “kiboko cha uraia” kwa sababu za kisiasa.

Katika muda mfupi wa madaraka ya Rais Magufuli, suala la uraia limegeuzwa silaha ya kisiasa na linaendelea kuumiza wananchi kadhaa, hasa wanaokosoa serikali au wasiokubaliana na mambo kadhaa inayotenda.

Orodha ni ndefu lakini wengine wanaotajwa na vyombo vya habari, mbali na Padre Saba, ni hawa wafuatao:

Askofu Zakaria Kakobe wa Full Gospel Bible Fellowship. Alitoa mahubiri makali katika Krismasi ya 2017, akaonya serikali juu ya dhuluma, hasa mauaji ya raia. Alimtaka rais atubu. Askofu Kakobe alitiwa misukosuko na polisi na Mamlaka ya Mapato Tanzania. Walipokosa jinsi ya kumtia hatiani, idara ya uhamiaji iliibua suala la uraia wake. Sasa anachunguzwa uraia.

Aidan Eyakuze mkurugenzi mtendaji wa Twaweza, shirika lisilo la kiserikali ambalo limetangaza matokeo ya utafiti unaoonyesha kuwa umaarufu wa rais miongoni mwa wananchi umeshuka kutoka asilimia 96 (2016) hadi 54 (2018).

Wakati Twaweza walipotangaza kuwa rais alikuwa anapendwa na waanchi kwa asilimia 96 mwaka 2016, serikali haikutilia shaka uraia wa mkurugenzi wake. Ilipotangaza kushuka kwa umaarufu wake, taasisi yake ilisakamwa.

Baadhi ya vijigazeti vinavyofadhiliwa na serikali kwa ajili ya propaganda za kisiasa za CCM, vimekwenda mbali zaidi, vikamtaja kuwa ni mwanachama wa chama cha siasa (Chadema), jambo ambalo taasisi yake imekanusha. Sasa anachunguzwa uraia.

Askofu Severine Niwemugizi wa Jimbo Katoliki la Rulenge. Mwaka 2017 alitoa kauli kuhusu umuhimu wa kuwa na katiba mpya ili hatua nzuri zinazochukuliwa na serikali zizingatie misingi ya katiba badala ya kutegemea uamuzi wa mtu. Rais Magufuli ameshasema kuwa katiba mpya si ajenda yake.

Haikuchukua muda mrefu, idara ya uhamiaji ikaanza kuhoji uraia wa askofu huyo. Bado pasipoti yake imeshikiliwa. Anachunguzwa uraia.

Abdul Nondo, mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Alitoa taarifa kupitia simu yake kuhusu watu waliomteka usiku, wakamsafirisha usiku kucha kutoka Dar es Salaam hadi Iringa.

Kwa kuwa “watu wasiojulikana” ambao wamekuwa wanateka na kupoteza watu wanahusishwa na vyombo vya dola, yalitoka maagizo mengi ya kisiasa yakitaka kijana huyo ashughulikiwe. Serikali imemfumgulia kesi mahakamani. Amesimamishwa masomo chuoni. Anachunguzwa uraia.

Padri Saba, Askofu Kakobe, Eyakuze, na Nondo ni wazaliwa wa Kigoma. Askofu Niwemugizi ni mzaliwa wa Kagera. Orodha ya wanaoshughulikiwa “kimfumo” ni ndefu.


Baada ya hao anaefuata ni mkurugenzi wa JF Maxio Melo,
Hii ndo CCM bwana,ukileta fyoko unashughulikiwa.sasa humu jf mnajifanya kutiririka sasa watamshughulikia Melo na jf itakwisha
 
For the security purpose of ourselves, mali na taifa letu.....hakuna namna......tuwe pamoja ktk kujaribu kuwareveal watu wanaohamia nchini kwa kutumia cover ya kujishughulisha na majukumu nchini.....ni hatar sana .....tuwe wadadisi ktk mauala ya kiusalama wetu wenyewe.
 
Sasa kama bibi na babu yake wako hai ataonesha kaburi lipi?!!
 
Watanzania acheni ushabiki wa kisiasa katika masuala muhimu ya nchi, hususan ya amani, utulivu na usalama. Hao wote waliotajwa wanamizizi katika nchi ambazo zimemwaga damu. Hivyo, wangependa waione TZ inaingia huko. Kumbukeni kwamba, nchi ya kishosharisti ya Urusi, USSR, ilisambaratishwa na Rais Gobachevu, ambaye mizizi yake ipo Marekani. Marekani walimtumia na nchi ya Urusi ikasambaratika. Hivyo, hata kama watu hao walizaliwa TZ, kuna haja ya kuwafuatilia kwa kuna juu ya maneno na vitendo vyao. Uhamiaji fanyeni kazi yenu, msiogope maneno ya wana siasa au wana harakati wa haki za binadamu, hao wanafadhiriwa wa watawala wetu wa zamani.
Rubbish!
 
Ninachoelewa kila jambo lina muda na muda haumsubiri mtu!!Yote yatapita!!Just matter of time!!Time don't wait!!Mungu atupe uzima
 
Back
Top Bottom