Serikali yaeleza sababu kuu 4 za kupanda kwa bei ya chakula nchini

Nyabukika

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2022
Posts
1,440
Reaction score
1,046
Your browser is not able to display this video.


Serikali yaeleza sababu kuu 4 za kupanda kwa bei ya chakula nchini :-
1. Athari za janga la Uviko-19
2. Athari za vita ya Ukraine
3. Mabadiliko ya tabia nchi
4. Kupanda kwa bei ya mafuta duniani

Kupanda kwa gharama za maisha imesababishwa na kupanda kwa mfumuko wa bei duniani na ndio maana Serikali ya Rais Samia Suluhu inapunguza gharama za kilimo kupitia ruzuku ya pembejeo za kilimo ili kupunguza gharama za mazao.
 
1. Kwamba watu wameshindwa kulima kwa sababu ya covid 19
2. Tumeahindwa kulima kwa sababu ya vita Ukraine tumepata mawazo sana. Ukraine yenye vita inaendelea kutoa msaada wa vyakula Africa
3. Mvua imeshindwa kunywsha ila tunatakiw tutoke kwenye kilimo kinachotegemea mvua na tufanye kilimo cha umwagiliaji.
 
Gwajima amewalipua mza Leo,

Kawambia wanaoleta sababu mfu juu ya mfumuko wa Bei za Bidhaa hawana AKILI hata kama wapo CCM!!!
 
1. Athari za janga la Uviko-19
Wangekufafanuliwa TZ iliathirikaje zaidi? Virusi walishambulia mashamba?

2. Athari za vita ya Ukraine
Sisi tukiathirikaje sasa?

3. Mabadiliko ya tabia nchi
Mazao yapo au hayapo?

4. Kupanda kwa bei ya mafuta duniani.
Rudhuku haikufanya kazi? Bei imeshuka huko, huku inapanda, kulikoni?
 
Gwajima amesema mza Leo kuwa Nchi ilipata chakula Cha kutosha wakati Nchi zingine zikiwa LOCKDOWN wakati wa corona.

Uhaba umekuja sababu majirani walikuwa na njaa na waliokuja na Bei kubwa hivyo wakulima wakauza bila akiba.

At least ameongea KWELI sio Hawa machawa wenye akili za kushikiwa.
 
Duniani kote kuna mfumuko wa bei. Hapa ni tujue hatua zilizochukuliwa na matokeo yake.
 
Kila mmoja anatoka pangoni na lake 🤣🤣🤣
 
Nilifikiria Gwagima ana issue za ufufuko tu kumbe ana hoja chanya, hapo umenena.
 
UONGO MTUPU watanganyika Sio Wajinga kihivyo hatudanganyiki
 
Vipi kuhusu kuuza chakule nje ya nchi?
 
Of course bila kusahau kuwa kupanda kwa EU ya nyama na maharagwe ni good news kwa wakulima na wafugaji, amvao ni 88% ya Watanzania. This means that- in net terms - we are as Tanzanians grateful for the increase in farm prices this gives good income.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…