Wizara ya Ardhi
Govt Institution
- May 14, 2024
- 306
- 165
RUVUMA: Serikali kupitia Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeendelea kutoa huduma kwa wananchi kupitia Kliniki za Ardhi, zinazolenga kupunguza migogoro ya ardhi na kuongeza uelewa kuhusu sheria na taratibu za umiliki wa ardhi.
Kwa mkoa wa Ruvuma, kliniki hiyo ya Ardhi ya Kidigiti ilianza sept 22, 2026 na inatarajia kuhitimishwa Okt 3, 2026 katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea ambapo wananchi wameendelea kupata fursa ya kuwasilisha changamoto zao sambamba na kupata ufafanuzi na ushauri wa kitaalamu kuhusu masuala ya ardhi.
Baadhi ya wananchi waliohudhuria kliniki hiyo wameipongeza Serikali kwa kuendelea kupeleka huduma hizo karibu na wananchi, huku wakiomba kliniki kuendelea hadi maeneo ya vijijini ambako bado kuna changamoto mbalimbali za ardhi.
Kwa upande wake, Kamishna wa Ardhi Msaidizi Mkoa wa Ruvuma, Said Kijiji, amesema kliniki hiyo pia inatoa huduma za umilikishaji ardhi, utoaji wa hati, usikilizaji kero na ushauri wa kitaalamu kwa wananchi.
Ameongeza kuwa, kupitia kliniki hiyo wananchi wanapatiwa elimu kuhusu mfumo wa kidijiti wa kuomba umiliki wa ardhi unaowezesha kuwasilisha maombi ya hati bila kufika ofisi za ardhi.
Kwa mujibu wa Kijiji, Serikali inaendelea kutoa elimu kwa wananchi na viongozi wa vijiji ili kupunguza migogoro ya ardhi, huku akiwataka wananchi kujiridhisha katika ofisi za ardhi kabla ya kununua ardhi ili kuepuka hali ya kiwanja kimoja kuuzwa kwa watu zaidi ya mmoja.