Serikali yafafanua kauli ya Rais Samia kuhusu Bei za Mafuta

Inside10

Platinum Member
Joined
May 20, 2011
Posts
34,776
Reaction score
42,933
Serikali kupitia Msemaji Mkuu wake, Gerson Msigwa, imetoa ufafanuzi wa kauli ya Rais Samia aliyotoa mchana wa leo Aprili 8, 2026, kuhusu bei za mafuta;

Soma: Rais Samia: Bei ya mafuta Marekani na Ulaya ni Dola 800 na Euro 400/600 lita 1, Sisi tuko vizuri, tuna uhakika wa miezi 3

UFAFANUZI​

Leo tarehe 08 Aprili, 2026, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati akiwaapisha viongozi aliowateua hivi karibuni amezungumzia changamoto ya kupanda kwa bei za mafuta Duniani.

Kutokana na baadhi ya watu kuhitaji ufafanuzi wa kauli hiyo, Mheshimiwa Rais alimaanisha ifuatavyo;

1. Bei za mafuta ya dizeli katika soko la dunia zimeongezeka kwa dola za Marekani 800 kwa tani ambapo zimetoka dola 650 ya mwezi Februari 2026 hadi kufikia dola 1,450 mwezi Machi 2026.

2. Bei za mafuta ya petroli katika soko la dunia zimeongezeka kwa dola za Marekani 434 kwa tani ambapo zimetoka dola 618 ya mwezi Februari 2026 hadi kufikia dola 1,052 mwezi Machi 2026.

3. Bei za mafuta ya taa na mafuta ya ndege katika soko la dunia zimeongezeka kwa dola za Marekani 821 kwa tani ambapo zimetoka dola 679 ya mwezi Februari 2026 hadi kufikia dola 1,500 mwezi Machi 2026.

Pamoja na kuwepo kwa athari za kupanda kwa bei za mafuta kwa watumiajiu duniani kote, bado viwango vya bei za mafuta vya Tanzania ni vidogo ikilinganishwa na nchi zingine.

Kupanda kwa bei za mafuta kumesababishwa na athari za vita inayoendelea kati ya Irani dhidi ya Israel na Marekani iliyosababisha kufungwa kwa lango la Hormus ambalo hupitisha mafuta mengi yanayotumiwa Tanzania na nchi zingine za Afrika.

Gerson Msigwa
Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Msemaji Mkuu wa Serikali

​


Pia soma: Hotuba ya Samia kwenye page ya Ikulu imefutwa muda mfupi baada ya kuhutubia
 
Niljua tu, toilet paper iitwayo Gerson Msigwa lazima itatumika.

Na kichekesho ni kwamba vitu vinavyotolewa ufafanuzi ni tofauti hata na alichokiongea muuaji wa Kizimkazi .

Msigwa kaja na mambo yake mengine na ni mapya.

Na tangu lini mafuta yakauzwa kwa tani??

Kijamaa kitapeli sana hebu hapo ona kimewasha VPN na kuconnect server za Australia kinakuja kutweet uongo kwenye mtandao walioufungia.
 
Hapo kwenye mafuta kuuzwa kwa tani ndio Msigwa nae kaniongezea maumivu ya kichwa aliyoyaanzisha Samia.

Simuoni kama Msigwa amekuja kutoa ufafanuzi, huyu amekuja kutuongezea changamoto vichwani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…