Mkuu yule mama aliweka saini ya dole gumba (fingerprints). Hawezi kusema alama hizo ziligushiwa.
Soma hapo chini.
Doesn’t add up, yaani aridhie jambo; halafu akalipinge ardhi na polisi wakati mumewe yupo hai baada ya kujua ukweli na jalada lifunguliwe.
Hati ya kubadili kiwanja imefanyika vipi bila ya taarifa zake au ushahidi wake.
Mkuu tafuta mtu ambae anataka kununua hata kiwanja leo, ambae hataki shida mbele ya safari anataka muende kisheria.
Kwa njia halali za sheria za Tanzania kubadili umiliki wa kiwanja ukutane na mteja ambae hataki matatizo huko mbeleni anataka mfanye kila kitu kisheria unaweza susa kuuza na kiwanja chenyewe. Kuna mlolongo wa vielelezo balaa, sijui picha, sign huku na kule, mashahidi waende ardhi, mkamuine mwenyekiti wa mtaa yaani mpaka unaweza sema inatosha.
Ishanitokea hiyo sema ile nataka kususa tu kwa usumbufu wa sheria, mteja akaona isiwe shida atamaliza mwenyewe. Jamaa akatumbukiza hela yote siku hiyo hiyo baada ya kuwa anadengua kutoa hela kwa miezi miwili anataka kufuata sheria. Kiwanja chenyewe ilikuwa kama nakitoa sadaka tu kwa bei ya kutupa.
Sasa ije kuuza nyumba ya familia bila ya mke kujua na mashahidi hakuna. Hapo kuna foul play, the mere fact hata eviction process hawakufuata hao ni wahuni.
Not many land exchanges in Tanzania follow due processes ndio msingi wa future disputes na familia.