Serikali yafungua milango ya majadiliano kwa magazeti yaliyofungiwa

Serikali yafungua milango ya majadiliano kwa magazeti yaliyofungiwa

“Nasikia kuna vyombo vya habari mlifungia, vifungulieni na vifuate sheria, tusiwape mdomo wa kusema kwamba tanaminya uhuru wa kuzungumza.

“Tusifungie kibabe, wafungulieni na kuhakikisha wanafuata sheria na miongozo ya Serikali. Hakikisheni kila mliyempa ruhusa ye kuendesha chombo cha habari afuate sheria.

Kanuni ziwe wazi kuwa kosa hili adhabu yake ni hii na mnakwenda kulingana na adhabu mlizoziweka kwenye kanuni, tusifungie kibabe, viacheni vifanye kazi,” alisema Rais Samia.
Mbona maelekezo ya rais yapo wazi tu. Ni wapi kaongelea "tv za mitandaoni" pekee?!!!

MATAGA wa wizarani wana mamlaka juu ya rais, au?!!!

Kitendo cha Abbas na genge lake KUDUNISHA na KUSIGINA maelekezo ya rais na amiri jeshi mkuu yaliyotolewa hadharani ni dalili mbaya sana kwa mustakabali wa taifa.

Ina maana hakuna haja ya kukubali, kutii wala kutekeleza maelekezo yake🙄
 
Tangu lini Chadema wakaitakia mema ccm hadi wajipe kazi ya kumsifia rais Samia?.

Kazi ya kumsifia rais Samia ni ya MATAGA siyo ya chadema
Wanaomsifia mh. Bi-mkubwa ni umma wa Watanzania, siyo wanachama wa vyama
 
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa amesema agizo la Rais Samia Suluhu Hassan kutaka vyombo vya habari vilivyofungiwa kufunguliwa, linahusu televisheni za mtandaoni pekee.

Hata hivyo, Bashungwa ameeleza leo Jumatano, Aprili 7 2021 kuwa Serikali inafungua milango yake kwa vyombo vingine vya habari vilivyofungiwa kuangalia namna gani vinaweza kufunguliwa kwa mujibu wa sheria.

Kauli ya Bashungwa inatokana na madai ya wadau wa habari nchini, kutaka vyombo vya habari yakiwemo magazeti yaliyofungiwa kufunguliwa kupitia agizo hilo la Rais Samia.

Juzi, wakati akiwaapisha makatibu na manaibu makatibu wakuu wa wizara mbalimbali, Rais Samia aliagiza kufunguliwa kwa vyombo vya habari vilifungiwa na kwamba, vipewe uhuru katika kutekeleza majukumu yake bila kuvunja sheria.

“Nasikia kuna vyombo vya habari mlifungia, vifungulieni na vifuate sheria, tusiwape mdomo wa kusema kwamba tanaminya uhuru wa kuzungumza.

“Tusifungie kibabe, wafungulieni na kuhakikisha wanafuata sheria na miongozo ya Serikali. Hakikisheni kila mliyempa ruhusa ye kuendesha chombo cha habari afuate sheria.

Kanuni ziwe wazi kuwa kosa hili adhabu yake ni hii na mnakwenda kulingana na adhabu mlizoziweka kwenye kanuni, tusifungie kibabe, viacheni vifanye kazi,” alisema Rais Samia.

Baada ya kauli hiyo, wadau wa habari walipongeza uamuzi huo wa Rais Samia huku wakiomba agizo hilo lifanyiwe kazi mara moja na mamlaka husika.

Hata hivyo, mjadala mkali uliibuka baada ya Katibu Mkuu wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Hassan Abbasi kuhojiwa na kituo cha luninga cha Wasafi, akieleza kuwa uamuzi huo utahusu televisheni za mtandaoni pekee.

Baadhi ya wadau wa habari walitegemea kuona vyombo vyote vilivyofungiwa yakiwemo magazeti yakifunguliwa. Hata hivyo, kauli ya Bashungwa kuwa vyombo vingine nje ya televisheni za mtandaoni vinaweza kukaa mezani na wizara hiyo kila kimoja kulingana na kesi yake iliyosababisha kufungiwa.

Mwananchi
Haki inajadiliwa au inatolewa ? Kukaa mezani ni kutaka kuweka masharti kinyume na katiba kwenye uhuru wa vyombo vya habari. Ni nini huyo aliyefunga hivyo vyombo anataka kujadili ili hali wakati anavifungia hakuwaita mezani? Avifungulie kama alivyovifunga. Aache longolongo zisizo na msingi.
 
Tangu lini Chadema wakaitakia mema ccm hadi wajipe kazi ya kumsifia rais Samia?.

Kazi ya kumsifia rais Samia ni ya MATAGA siyo ya chadema
Stupidity of the highest order. There is no president of ccm , there is president of TANZANIA and for Tanzanians.
 
Rais pekee atayekuja kuibadilisha Tanzania ni kutoka upinzani. Mungu atupe maisha marefu tuje kushuhudia hii.
 
Walah madam President asipokuwa kuwa makini ataendeshwa Sana na hawa masalia ya mataga

Kauli ya Rais n sheria Haina mjadala lakn watendaj wameifanya kuwa mjadala anacheza na nyani ..asubir mavuno
Hawa kenge Abbas na Bashungwa ningekua mimi rais asubuhi tu hawana kazi.
 
Rais mbona analaumiwa kuwa hana msimamo? kwa kipi?, mbona watu hatuna subira? kwani Rais alishinikizwa kufungulia vyombo vya habari ama ni mapenzi na nia njema iliyosukumwa na utu wake?. Tangazo halina hata siku tano leo watu mnamjia juu rais eti anayumbishwa badala ya kumpongeza au nyie ndio wale wale kama akina Cypian Musiba. Mmenihuzunisha kwa kweli, kuna baadhi ya watu humu hata jf inapopata misukosuko kama akina Melo kuburuzwa mahakamani mnafurahia wakati hii jf mnaitumia pia.
 
Waitike mazungumzo.
HUYU MWANAMKE SSH ASITU CHEZEE WANAUME......!

Abas na Baahungwa KAZENI, ONESHENI KUWA NINYI NI WANAUME.

Otherwise vyombo vya habari, VITA WADHARAU.
MLIFUNGA KWA SHERIA FUNGUENI KWA SHERIA.

Mwanamke ni mwanamke tu, hata AWE NANI.
wadanganye tu hapo atakapowapapasa makalio ndio tutajua amiri Jeshi mkuu ni nani ,hao mapapeti wa malaiaka wa chattle au Mama Samia
 
Huyu ni bure kabisa, atakuwa kituko kuzid Jiwe. Hamna kitu pale ni wasted resource
nenda zako Jiwe hata siku ina masaa mangapi hajui? sasa angalau magazeti yameanza kununuliwa.
 
Rais mbona analaumiwa kuwa hana msimamo? kwa kipi?, mbona watu hatuna subira? kwani Rais alishinikizwa kufungulia vyombo vya habari ama ni mapenzi na nia njema iliyosukumwa na utu wake?. Tangazo halina hata siku tano leo watu mnamjia juu rais eti anayumbishwa badala ya kumpongeza au nyie ndio wale wale kama akina Cypian Musiba. Mmenihuzunisha kwa kweli, kuna baadhi ya watu humu hata jf inapopata misukosuko kama akina Melo kuburuzwa mahakamani mnafurahia wakati hii jf mnaitumia pia.
Lawama ni kwa hao waliotengua agizo la RAISI. Walipaswa watekeleze sio kuligeuza geuza kukidhi matakwa yao. Kwani raisi alisema wakae na vyombo vya habari ndio wavifungulie ???
 
Yaani huyu Waziri anatufanya kuwa hatukumsikia mheshimiwa Rais kweli?
 
N mm cjamwelewa mama samia au hao wachini aliowapa maagizo ndio hawajamwelewa mama maana kila mmoja anasema lakee
Shida kubwa tanzania hawa mawaziri kujia chini siku zote husubiri neno la rais ndio wafanye kazi sio creativity wa mambo, Na Rais alisema wakawe wabunifu, hii nchi huko ilikotoka na hasa hapo alipokuja kuishika mama samia walikuwa wakiongozwa kwa mihemuko, mtu anadhalilika na taaluma yake anakuwa hawezi kuanya kazi kama taaluma yake inavyomuongoza, na kwa mfano kesho rais akisema hayo magazeti yafunguliwe watamtaka rais pia ataje na majina ya magazeti ili ku-specify. Ndio inferior ya hawa watu vichwa vyao kama vimewekwa gundi kali sana
 
Waziri wa habari mh Bashungwa amesema msamaha wa Rais Samia unahusu Online tv zaidi ya 460 zilizofungiwa pekee na siyo magazeti au kitu kingine chochote.

Bashungwa amesema atashughulikia magazeti yaliyofungiwa case by case hivyo wamiliki wa magazeti hayo wafike ofisini kwake kwa mazungumzo ya kutatua tatizo lililopo

Source BBC Dira ya Dunia

Ukinizingua Nitakuzingua!
Rushwa hapa IPO kwann wafike ofisini kwake!?? Kwa Rais alisema hivyo???
 
Mh Rais kua makini na watendaji has a walioachwa na Rais aliyepita watakuangusha amini.nakwambia kuna watu mawaziri walilewa vyeo sasa wana kuwekea maneno ambayo hukuyasema kua makini huku bara kuna midubwana hatari sana !!!! Ona. Suala LA kufungulia vyombo linavyochukuliwa na madubwana
 
Tangu lini Chadema wakaitakia mema ccm hadi wajipe kazi ya kumsifia rais Samia?.

Kazi ya kumsifia rais Samia ni ya MATAGA siyo ya chadema
Rais akifanya vizurri atasifiwa na kila MTU na akifanya hivyo kama bwana yule alipondwa hata na mridhi wake
 
Rais mbona analaumiwa kuwa hana msimamo? kwa kipi?, mbona watu hatuna subira? kwani Rais alishinikizwa kufungulia vyombo vya habari ama ni mapenzi na nia njema iliyosukumwa na utu wake?. Tangazo halina hata siku tano leo watu mnamjia juu rais eti anayumbishwa badala ya kumpongeza au nyie ndio wale wale kama akina Cypian Musiba. Mmenihuzunisha kwa kweli, kuna baadhi ya watu humu hata jf inapopata misukosuko kama akina Melo kuburuzwa mahakamani mnafurahia wakati hii jf mnaitumia pia.
Sasa kama ni mapenzi yake kwann aliyemteua abadili???
 
Back
Top Bottom