Serikali yafuta ada ya Mitihani kwa watahiniwa wa shule za Serikali

Serikali yafuta ada ya Mitihani kwa watahiniwa wa shule za Serikali

Wangefuta Ada hata kwa shule binafsi na vijana wanaorudia mitihani wapunguze vizingiti kwa Wasomi..
 
Hivi wanafunzi wa shule binafsi sio Watanzania?
Wazazi wao hawalipi kodi?
Waumizwe ada na mitihani ambayo ni ya serikali?
Hii nchi ina viongozi wenye mawazo mgando sana! Cha kushangaza hao wazazi wenye watoto wanaosoma shule za kujitegemea, ndiyo hao hao wanao kamuliwa tozo nyingi zaidi kila siku na serikali.

Ubaguzi wa kijinga kabisa huu.
 
Hizi siasa bana, toka Zamani mitihan ya drasa la saba, kidato Cha nne walikuwa hawalipi toka elimu bila malipo ilipoanza, Leo hii wamemalizia na kidato Cha sita tu...
 
Taarifa iliyotolewa na Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) imesema watahiniwa wa Darasa la 7, Kidato cha 4 na 6 kutoka shule za Serikali hawatolipa ada hizo kuanzia sasa.

Hata hivyo Baraza limesema ada hizo zitaendelea kulipwa na wanafunzi wa shule za binafsi.

View attachment 2357463
shukrani nyingi na za kipekee kabisa ziende kwa serikali ya Ccm
 
Hivi wanafunzi wa shule binafsi sio Watanzania?
Wazazi wao hawalipi kodi?
Waumizwe ada na mitihani ambayo ni ya serikali?
Lengo ni kutaka wanafunzi wote wasome shule za serikali (umma). Kusoma shule za binafsi maana yake unajimudu na ukijimudu maana yake unafaa kuwa chanzo cha mapato, serikali tunakitumia chanzo hicho. Halafu hii ada ya mtihani wala hamjawahi kulalamika kuwa inawaumiza, kelele zinatoka wapi kuwasamehe wanaosoma shule za serikali??
 
This is rubbish, danganya toto, rubbish of the highest dsegree
 
Mtu kaisadia serikali kusomesha,na hayo ndo malipo yake
 
Hivi wanafunzi wa shule binafsi sio Watanzania?
Wazazi wao hawalipi kodi?
Waumizwe ada na mitihani ambayo ni ya serikali?
Tufunge shule zote za binafsi tuone matokeo yake. Shule za Serikali haziwezi kutosheleza mahitaji na wanao soma huko ni watanzania hivyo maamuzi haya ni ya kibaguzi. Serikali yetu bado ina kasumba ya ujamaa.
 
1663243635454.png

Kila mtahiniwa wa kidato cha nne na sita alitakiwa kulipa ada ya mtihani TZS 50,000. Baada ya kufuta ada na michango isiyo muhimu, Serikali imefuta ada ya mtihani kwa shule za Serikali ikiwa ni sehemu ya azma ya Mhe. Rais Samia Suluhu kuifanya elimu kuwa nafuu.
 
Waliwahi kufanya hivyo 2011 ila 2012 ilirudishwa. Ni suala la muda tu.

Serikali ya kurithi.
 
Kwanini iwe shule binafsi wakati wote ni watanzania
 
Kwa speed ya kutisha. Mwisho watakuja na kusema hawatapata fursa kwenye vyuo vya serikali,ajira nk.Yetu macho huwa wanaanza hivi hivi
Ubaguzi unaanza hivihivi kama maumivu ya kichwa
 
Back
Top Bottom