Serikali yafuta vijiji na vitongoji vyote vya wamasai wa Ngorongoro kupitia Amri ya tangazo la Serikali namba 673

Serikali yafuta vijiji na vitongoji vyote vya wamasai wa Ngorongoro kupitia Amri ya tangazo la Serikali namba 673

Serikali kupitia kifungu cha 30 cha Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) Sura ya 287 kinachotoa ruhusa kwa mamlaka za Serikali kufanya mgawanyo wa Halmshauri za Wilaya;

Imetoa AMRI rasmi iliyotangazwa kwenye Gazeti la Serikali namba 673 la tarehe 02 Agosti, 2024; ili kufuta baadhi ya maeneo ya kiutawala kwenye mamlaka za Serikali za Mitaa hapa nchini kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa tarehe 27 Novemba, 2024.

Amri hii rasmi sasa inafuta Kata, Vijiji na Vitongoji katika Halmashauri za Wilaya zifuatazo; Ngorongoro, Bahi, Chemba, Kasulu, Kakonko, Hai na Rombo.

Katika Halmshauri ya Wilaya ya Ngorongoro pekee, kupitia AMRI hii, Serikali imezifuta Kata 11, Vijiji 25 na Vitongoji 96.

Garatwa,
Dar es Salaam, Tanzania.
20 Agosti, 2024.
View attachment 3074791
Ndivyo CCM inavyofuta haki za watu nchini, tuikatae!
 
Naomba mwenye kujua kilichofutwa wilaya ya Rombo anijulishe tafadhali!msaada
 
Kuna mamlaka za kishetani kama hii ya Bibi wa Kizimkazi, una maoni gani mh. Chawa.
sina haja kukuita nyumbu kwasabb ya kukurupuka kwako au uelewa na ufahamu mdogo wa masuala hayo...

hata hivyo,
muhimu zaidi ni kutii sheria bila shuruti wala ukaidi wa kuchochewa na wanaharakti uchwara na wanasiasa waliofilisika hoja nchini 🐒
 
Haiko hivyo ndugu. Binadamu hakamilishwi na hivi pekee.!!

Soma na sikiliza historia hii👇👇

Wa- Israel walihamishwa kwa nguvu toka ktk ardhi ya asili maelfu ya miaka iliyopita matukio yaliyofanyika mara mbili.

Mara ya kwanza: Mamilioni ya Wa - Israel walikuwa evicted kule Misri ya Kale. Baada ya kuishi miaka 430 Misri finally walirudi ktk nchi yao ya Asili na Mungu aliwaunga mkono..

Mara ya pili: Wa - Israel hawahawa kwa hila na kwa nguvu walihamishwa kwa mara nyingine tena toka ktk nchi ya asili yao na kupelekwa nchi ya kigeni ya Babel (Iraki ya leo). Wakaishi kule miaka 70 huku wakiwa na huduma zote muhimu..

Lakini baada ya miaka 70 walirudi ktk nchi ya asili yao..
===================================
Hata hawa Wamasai serikali inaweza kufanikiwa KUWAHAMISHA ktk nchi na ardhi yao ya asili kwa nguvu, ulaghai na udanganyifu...

Lakini baada ya muda fulani, nakuhakikishia kuwa wata trace asili yao na watakuja kurudi kwenye ardhi na nchi ya baba na babu zao huku Bi. Samia Suluhu Hassan mtekelezaji wa mpango huu mwovu akiwa amegeuka kuwa udongo na mavumbi ktk ardhi - yaani akiwa alishajufa na kuoza..

Asili ya mtu haipptei. Kama wewe uko huko uliko na hukumbuki kwenye asili yako, then wewe ni mfu na pengine siyo binadamu wa kawaida..!
Kweli kabisa, laana itawatafuna waliohusika na kupanga hizi njama
 
sina haja kukuita nyumbu kwasabb ya kukurupuka kwako au uelewa na ufahamu mdogo wa masuala hayo...

hata hivyo,
muhimu zaidi ni kutii sheria bila shuruti wala ukaidi wa kuchochewa na wanaharakti uchwara na wanasiasa waliofilisika hoja nchini 🐒
Nami sina sababu ya kukuita chawa kwa kuwa hata ubongo kichwani huna nafuu ya chawa anaganga njaa!
 
Mkuu naomba nisogezee hii barua kwa wakubwa:
👊💪🙏
 
Wajuzi naomba mnielekeze, serikali ikifutwa eneo maana yake ni kuwa haitakiwi kuwa na makazi ya watu??
Eneo linabadilishwa matumizi??
Na wakazi wake wanatafutiwa eneo lingine??
Mfano hivyo vijiji vya Rombo, kasulu nk.. inabidi watu wahame??
 
Nami sina sababu ya kukuita chawa kwa kuwa hata ubongo kichwani huna nafuu ya chawa anaganga njaa!
tuliza mihemko bas na makasiriko,

ni muhimu sheria za nchi zikazingatiwa na kufuatwa bila shuruti 🐒
 
Serikali kupitia kifungu cha 30 cha Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) Sura ya 287 kinachotoa ruhusa kwa mamlaka za Serikali kufanya mgawanyo wa Halmshauri za Wilaya;

Imetoa AMRI rasmi iliyotangazwa kwenye Gazeti la Serikali namba 673 la tarehe 02 Agosti, 2024; ili kufuta baadhi ya maeneo ya kiutawala kwenye mamlaka za Serikali za Mitaa hapa nchini kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa tarehe 27 Novemba, 2024.

Amri hii rasmi sasa inafuta Kata, Vijiji na Vitongoji katika Halmashauri za Wilaya zifuatazo; Ngorongoro, Bahi, Chemba, Kasulu, Kakonko, Hai na Rombo.

Katika Halmshauri ya Wilaya ya Ngorongoro pekee, kupitia AMRI hii, Serikali imezifuta Kata 11, Vijiji 25 na Vitongoji 96.

Garatwa,
Dar es Salaam, Tanzania.
20 Agosti, 2024.
View attachment 3074791
Amri batili hii

Haruhusiwi kufuta chochote...anaruhusiwa tu kubadili mipaka sio kufuta

Waziri kiazi
 
Siku inakuja ambayo haina jina. Ole wao mafisadi.
 
Back
Top Bottom