SERIKALI YAGOMA SIMBA /YANGA KUFANYA MABADILIKO

SERIKALI YAGOMA SIMBA /YANGA KUFANYA MABADILIKO

endrizzy

Senior Member
Joined
Oct 19, 2015
Posts
186
Reaction score
137
Jamani naomba kuuliza mi sifaham hili suala kwani serikali inaweza kubatilisha maamuzi ya wanachama wa klabu ya soka?
mfani wanachama wa simba wameamua kubadili mfumo wa uendeshaj wa timu yao kutoka ya wanachama mpaka jampuni na Yanga kukodisha je,serikali wana impact gani katika maamuz hayo ya wanachama maana nimeona magazeti mengi yanasema serikali inapinga uamuz huo...kwani simba na yana ni mali ya nani?
1475897773696.png
 
Si kweli.... BMT limetoa barua kabisa kuthibitisha kile kukicho fanyika pale klabuni Yanga..
 
Hebu ingia Boiplus kupata taarifa zaidi.. Nimeisoma ile barua ya BMT kutoka mule.
 
Utaratibu haujafuatwa,wanachama hawakushirikishwa,bodi iliyoidhinisha haipo kihalali (Nilivyomuelewa yule msemaji wa BMT)
 
Hizi club zinafanya ujinga tu, wanaweka club rehani kwa wahindi.
Wazee wetu wamezianzisha halafu wao wanapewa kirahisi namna hiyo tena baada kashindwa kwenye siasa.
 
Hizi club zinafanya ujinga tu, wanaweka club rehani kwa wahindi.
Wazee wetu wamezianzisha halafu wao wanapewa kirahisi namna hiyo tena baada kashindwa kwenye siasa.
Kwani wahindi sio watu or si wanachama wa hivyo vilabu? Hao wazee wapo wapi sasa? Akina mzee Akilimali na Kinesi? Acha ubaguzi
 
Kwani wahindi sio watu or si wanachama wa hivyo vilabu? Hao wazee wapo wapi sasa? Akina mzee Akilimali na Kinesi? Acha ubaguzi
Kusema wahindi ni sawa kusema wasukuma au wasamba na ndio maaana watoto wao wanajua kuongea kihindi kwanza kabla ya kiswahili.
Hao watu wanataka kuchukua hizo club hawana credibility yoyote.
 
Kusema wahindi ni sawa kusema wasukuma au wasamba na ndio maaana watoto wao wanajua kuongea kihindi kwanza kabla ya kiswahili.
Hao watu wanataka kuchukua hizo club hawana credibility yoyote.
Acha ubaguzi, ukija huku kwetu Lusewa utakuta watoto wote wanaongea kidendeule na kiyao baadaye ndio kiswahili kinafuata, kwa hio na sisi hatuna credibility?
 
Acha ubaguzi, ukija huku kwetu Lusewa utakuta watoto wote wanaongea kidendeule na kiyao baadaye ndio kiswahili kinafuata, kwa hio na sisi hatuna credibility?
Kama kuna wasambaa, au wasukuma maanake kuna wahindi pia hapo tatizo liko wapi.
Nimesema hao wanataka kuchukua hizo club hawana credibility yoyote ni watu wa scandals kiasi kwamba tuwaamini kuwakabizi uridhi wetu tuliowaachia na wazee tu kirahis namna hiyo.
 
Jamani naomba kuuliza mi sifaham hili suala kwani serikali inaweza kubatilisha maamuzi ya wanachama wa klabu ya soka?
mfani wanachama wa simba wameamua kubadili mfumo wa uendeshaj wa timu yao kutoka ya wanachama mpaka jampuni na Yanga kukodisha je,serikali wana impact gani katika maamuz hayo ya wanachama maana nimeona magazeti mengi yanasema serikali inapinga uamuz huo...kwani simba na yana ni mali ya nani?View attachment 414310
Tatizo hapa si Serikali, wewe mwanzisha mada, vilabu husika wala wananchi wanaotaka kuwekeza kwenye vilabu hivyo. Tatizo ni vyombo vya habari vinavyotumia matukio yaliyopo katika kujipatia faida, bila ya kujali athari ya uandishi huo wa kuvutia mashabiki, iwe kwa kuwafurahisha au kuwatisha.
Baraza la Michezo halijakataza mabadiliko yanayolengwa na mageuzi hayo. Lilichofanya ni kuvikumbusha tu vilabu hivyo kwamba ni lazima sheria ifuatwe kwenye mageuzi hayo. Mzazi anapohoji iwapo mwanawe ameshajiandaa kwanza kabla ya ndoa si sawa na kuwa amekataa mchumba wa mwanawe huyo! Vichwa habari kama 'Yanga Yetu Pwaa!' na kama hivyo, vinavyobuniwa ili kuwavutia watani wa Yanga wataokunwa nazo na washabiki wa Yanga wataoshtushwa nazo, si muhtasari wala mjumuisho sahihi wa msimamo huu wa Serikali kupitia BMT. Kadhalika ukisoma maelezo yenyewe hutashangaa kubaini nyongeza au kasoro nzito za habari yenyewe kulingana na ushabiki, utashi, chuki ama huba ya mwandishi inayotokana na kupewa ama kutopewa ''bahasha'. Waathirika wa upotoshaji wa aina hii wameamua kuacha kukanusha, maana matukio yao kunukuliwa visivyo kwa misingi hii kumekuwa ni jambo la kawaida. Wengine wamejaribu kuepukana na kutonukuliwa vyema kwa kutoa Taarifa kwa Vyombo vya Habari (press release), lakini hata hiyo haisaidii.
Na ilivyokuwa wasomaji (au wasomewa) wengi wa uandishi wa aina hii si wa kiwango cha kupambanua kasoro kama hizi, hubaki wanaamini kila kinachoandikwa au kusambazwa na chombo cha habari wanachojaaliwa kukiamini kutokana na msimamo wa chombo hicho juu ya hoja inayohusika. Masikini wadau hawa wa vyombo hivi wameishia kulishwa pumba kwa bei ya nafaka waliokusudia kuinunua, na kwa imani yao kwa muuzaji wanaishia kuzimeza wakidhani ni nafaka kweli. Kama kwamba wao ni malaika, wanahabari hawa matapeli wanataka kuhakikisha kwamba wateja wa aina hii wanabaki hukohuko mashimoni waliko, ili waendelee kuwa mashine zao za kukobolea fedha. Ndio maana kila muswada wa Sheria ya habari unaopendekezwa wanaendelea kuupinga kwa nguvu zao zote. Wanapaswa kufuata falsafa ya yule mwandishi gwiji kwamba habari iandikwe kwa ufupi ili imwahishe msomaji kuielewa, kwa usahihi ili imwezeshe msomaji kuelimika, na kwa kupendeza ili imfanye msomaji kuburudika.
 
Back
Top Bottom