Serikali ya Tanzania imewakaribisha Wafanyabiashara na Wawekezaji kutoka Serikali ya Urusi kuwekeza Tanzania kwa maslahi ya pande zote mbili na ustawi wa Dunia kwa ujumla.
Mwaliko huo umetolewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk wakati aliposhiriki katika maadhimisho ya Siku ya Kitaifa ya Urusi Jijini Dar es Salaam.
“Tanzania ina mazingira tulivu ya biashara na uwekezaji yanayotoa fursa za uwekezaji, hivyo natoa rai wa Wafanyabiashara na Wawekezaji kutoka Urusi kuja kuwekeza Tanzania ili kuimarisha zaidi biashara baina ya Nchi zetu mbili,”
Balozi Mbarouk amesema Tanzania kwa kushirikiana na sekta binafsi zimeboresha mazingira ya biashara na uwekezaji ili kuhakikisha kuwa uwekezaji unafanyika katika mazingira rafiki na salama na kuwafanya Wafanyabiashara kutoka nje kufanya biashara zao katika mazingira salama na rafiki “Urusi imekuwa Mshirika wa maendeleo ya kijamii, kiuchumi, kiteknolojia na kisiasa nchini Tanzania”
Kwa upande wake Balozi wa Urusi nchini, Andrey Avetisyan amesema ushirikiano wa Urusi na Tanzania ni wa kihistoria na umekuwa imara wakati wote na kwamba Urusi itaeendelea kushirikiana na Tanzania kijamii, kisiasa na kiuchumi wakati wote
Source: millard ayo