BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Serikali imekiri kuwa na upungufu wa umeme kwa megawati 190 na ndiyo sababu za kukatika au kuwa na mgawo wa mara kwa mara. Kauli hiyo imetolewa leo Novemba 2, 2022 bungeni na Naibu Waziri wa Nishati, Stephen Byabato wakati akitoa maelezo kama alivyotakiwa na Spika wa bunge Dk Tulia Akson.
Dk Tulia alimtaka Naibu Waziri kutoa majibu ya jumla kuhusu kukatika umeme kwani jambo hilo limekuwa kero. Katika swali la msingi Mbunge wa Ndanda (CCM), Cecil Mwambe ametaka kujua mkakati wa Serikali kumaliza kero ya kukatika kwa umeme mara Kwa mara ikiwemo mikoa ya kusini.
"Tatizo tulilonalo ni upungufu katika vyanzo vya kuzalisha umeme, mheshimiwa Spika, kwa sasa tuna upungufu wa megawati 190 katika vyanzo vya kuzalisha umeme nchini," amesema Byabato. Hata hivyo ameliambia Bunge kuwa mwezi ujao mradi wa Kinyelezi One utakamilika na kuingiza megawati 185 ambazo zitapunguza makali ya mgawo wa umeme.
Kingine ni mpango wa Serikali wa kutenga Sh500 bilioni kwa ajili ya kusaidia kwenye ukarabati wa miundombinu. Hata hivyo Spika ameagiza suala la mgawo wa umeme litazame vipaumbele kwa baadhi ya maeneo ambayo yanahitaji umeme kwa shughuli za viwanda na huduma muhimu ikiwemo Afya