The Sunk Cost Fallacy
JF-Expert Member
- Dec 1, 2021
- 19,582
- 14,167
Dah, Faults zipo Tanzania tu!!!
Katika miundo mbinu ya usambazaji umeme wa juu (overhead distribution) hutokea changamoto (faults) ambazo zinaweza kusababisha umeme kukatika. Sababu hizo huitwa.
Faults zipo nyingi (sina haja ya kuelezea)
Tabia ya fault inasababisha circuit Breaker (protection device) kujifungua kulingana na settings zilizowekwa. Hii yote ni kuilinda transformer pamoja na vifaa vingine.
Faults zipo ambazo zinang'ang'ania na kuondolewa ni mpaka mtu afike aondoe au arebishe tatizo. Mfano nguzo imeanguka kwenye msongo wa 11 au 33kV, au mti umeangukia waya za umeme kwenye misongo tajwa hapo. Hizi ni mpaka watu wafike watatue tatizo.
Kuna baadhi ya Faults ambazo hazing'ang'anii (transient Faults) au faults za kupita. Mfano tawi la mti limegusa tu na kutoka kutokana na upepo, au ndege kama kunguru kapigwa na kuanguka. Hapo ukirudisha umeme unawaka. Na hapa ndio jibu lako lilipo.
Kwa hiyo umeme unapokatika kuna kitu kinaitwa trial. Ikigoma kuwaka unajua shida hiyo fault ya kwanza ila ikiwaka ujue ni hiyo fault ya pili ambayo ndio inasababisha unaona umeme umekatika ndani ya sekunde kadhaa umeme umerudi.
Naamini umeelewa japo kidogo.
Bila shida hii ni kubwa kwenye Nchi zetu hizi ambazo miundombinu ya umeme ni duni Sana..Dah, Faults zipo Tanzania tu!!!
Mwisho tukupe wewe Wizara tuone kama umeme utakoma kukatikakatika?