Serikali yampokea Mwanariadha Magdalena Shauri baada ya kushinda Medali ya Shaba

Melubo Letema

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2020
Posts
416
Reaction score
414

Mapokezi Makubwa ya Mwanariadha wa Kimataifa wa Tanzania, Magdalena Chrispin Shauri (alie vaa bendera ya ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ) Jijini Arusha, katika ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Arusha, na Kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongela , Charles Maguzu kutoka BMT na Kiongozi wake Jeshini (JWTZ) Arusha.

mara baada ya Ushindi wa mbio za kilomita 42 (42.195KM) na kushinda Medali ya SHABA katika Mashindano ya Berlin Marathon yaliyofanyika nchini Ujerumani tarehe 24:09:2023 na Kuweka ya Rekodi ya Taifa (NR) kwa muda wa 2:18:41 na kuvunja rekodi ya marathon kwa Wanawake Tanzania ya 2:24:59 ya Mwanariadha (Banuelia Mrashani ) toka 2002.
 
Serikali imefanya jambo jema kujihusisha na mapokezi yake kwakua ina mtia moyo mchezaji.

sasa wampatie ata fedha au zawadi yoyote ili kumpa motisha.
Ata feni au saa ya ukutani tu itakua ni zawadi ndogo ila ita mtia moyo.
 
Wazi Zuri
 
Riadha na boxing ndo michezo iliyokuwa inatuheshimisha miaka ile ya Mwalimu. Ila wakaja wapuuzi fulani wakaiweka kapuni michezo hiyo na kuzama kwenye soka (ambalo nalo ni tia maji, tia maji tu).

Kuna nchi hazijui hata priorities zao kama hii Tanzania yetu. Wenye kujua priorities wameelekeza nguvu kwenye michezo inayowapa heshima zaidi e.g Kenya na Ethiopia (riadha), USA (Basketball ๐Ÿ€, boxing, n.k), India (cricket). Nchi kama Uganda tangu Idi Amin aache kucheza mieleka na kupaki medali zake kabatini, mchezo huo ukakosa mwendelezo. Tuna matatizo ya problem!
 
Halafu serikali iwasaidie wanariadha nchini kumuondoa yule Filbert Bayi na genge lake TOC. Maana kwa sasa hiyo TOC ameigeuza kuwa mali yake. Ziingie damu mpya ili kuleta mapinduzi kwenye michezo ya riadha, nk.
 
Unafiki wa kiwsngo cha kami.

Je ilihusika na maandalizi yake au ndo inataka kupoka credits
 
Halafu serikali iwasaidie wanariadha nchini kumuondoa yule Filbert Bayi na genge lake TOC. Maana kwa sasa hiyo TOC ameigeuza kuwa mali yake. Ziingie damu mpya ili kuleta mapinduzi kwenye michezo ya riadha, nk.
Nakuunga Mkono Asilimia Mia Moja. Maandalizi yajayo ya Olympic na maandalizi ya Qualifications za Olympic, fungu zinatolewa na International Olympic Committee (IOC) ila Filbert Bayi na Henry Tandau, wanakula.

Ni Wezi Sana hawa wazee. Watoke
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ