Melubo Letema
JF-Expert Member
- Apr 1, 2020
- 416
- 414
Mapokezi Makubwa ya Mwanariadha wa Kimataifa wa Tanzania, Magdalena Chrispin Shauri (alie vaa bendera ya 🇹🇿) Jijini Arusha, katika ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Arusha, na Kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongela , Charles Maguzu kutoka BMT na Kiongozi wake Jeshini (JWTZ) Arusha.
mara baada ya Ushindi wa mbio za kilomita 42 (42.195KM) na kushinda Medali ya SHABA katika Mashindano ya Berlin Marathon yaliyofanyika nchini Ujerumani tarehe 24:09:2023 na Kuweka ya Rekodi ya Taifa (NR) kwa muda wa 2:18:41 na kuvunja rekodi ya marathon kwa Wanawake Tanzania ya 2:24:59 ya Mwanariadha (Banuelia Mrashani ) toka 2002.