Serikali yamsaka Nabii Namba 7 anayejitangaza kuponya Corona

Serikali yamsaka Nabii Namba 7 anayejitangaza kuponya Corona

Serikali ya Tanzania imesema itamchukulia hatua Moses Mollel maarufu Nabii Namba Saba iwapo atashindwa kudhibitisha kauli yake kuwa ana uwezo wa kutibu wenye maambukizi ya virusi vya corona.

Hayo yameelezwa na naibu Waziri wa Afya, Dk Faustine Ndugulile katika ziara yake ya kikazi jijini Arusha.
Nabii Namba Saba, mkazi wa Ngaramtoni wilayani Arumeru mkoani Arusha amekuwa akijitangaza kuwa na dawa ya kutibu ugonjwa huo na kuweka mawasiliano yake kwenye mitandao.

Dk Ndugulile amesema taarifa za mtu huyo zimesambaa katika mitandao ya kijamii na vyombo vya habari, kumtaka athibitishe.
Amesema Serikali imetuma wataalamu wake kumsaka na kumhoji kama anavyo vibali vya kutoa huduma ya tiba na kujitangaza.

“Kimsingi nimeiona hiyo taarifa ya huyo mtu anayejiita Nabii Namba Saba kuwa ana dawa ya kutibu ugonjwa wa Corona, ila hapa Tanzania hatuna maambukizi yoyote ya ugonjwa huo tunachotaka huyo mtu atuthibitishie uwezo wake wa kutibu huo ugonjwa wa corona,” amesema Dk Ndugulile.

Ameongeza kuwa iwapo atashindwa kuthibitisha atachukuliwa hatua kali za kisheria.
Dk Ndugulile amesema yeyote anayetoa tiba asili na mbadala lazima asajiliwe na Wizara ya Afya, dawa zake ziwe zimesajiliwa na Wizara hiyo na kusisitiza kuwa nabii huyo pia anapaswa kuthibitisha amesajiliwa wapi na lini.
 
Wangemwambia athibitishe, angeshindwa wangemfunga angeweza wangechukua shilingi 200 katika kila 500.


Asingeshindwa kuthibitisha kwa sababu Tanzania hatuna uwezo wa kupima kama umepona Corona, au hujapona, au ulikuwa nayo to begin with.

Senegal and South Africa peke yao ndio wana uwezo huo. Sasa hivi ukikutwa na ki temperature na una mafua, kohozi, koo kavu, umetoka china, unachukuliwa sample inatumwa SENEGAL tunasubiri majibu!

Wizara ya Afya hawana moral and technical authority kubwa saaaana ya kumshukia Nabii Mosses Mollel the Seventh.

Hakuna mganga wa jadi ambae huambiwa athibitishe madai ya ubora wa dawa. Serikali isivunje sheria ya Bunge ya Waganga wa Jadi.
 
Wamsake tu...
Ajitokeze, wampeleke Wuhan kwenye ile hospital, akapige show 1 kali ya kibabe, wagonjwa wapone, ile hospital majengo yake waendelee kufugia popo...


Everyday is Saturday................. 😎
 
Naibu Waziri wa Afya Dkt Faustine Ndugulile, amesema kuwa Serikali imekwishatuma wataalam wake kwa ajili ya kumhoji Nabii namba saba aliyejitokeza na kutangaza kuwa anao uwezo wa kutibu ugonjwa wa homa kali ya mafua inayosababishwa na Virusi vya Corona na iliyopewa jina la COVID-19.

ANATIBU%20CORONA.jpg
Pichani ni Nabii namba saba aliyetangaza anatibu virusi vya Corona, na Waziri wa Afya Dkt Faustine Ndugulile
Dkt Ndugulile amesema kuwa endapo watabaini mtu huyo hana utaalamu katika kile alichokitangaza, Serikali itamchukulia hatua stahiki na kuwataka wananchi kuepuka kutoa kauli ambazo zitachanganya jamii.

“Sisi tumeona hizo clip ambazo zinazunguka na sisi tumetuma timu yetu ya wataalam ili huyo bwana akatuthibitishie kama ana uwezo wa kufanya tiba hiyo na atuambie hiyo dawa yake imesajiliwa wapi na yeye amesajiliwa wapi na lini” amesema Dkt Ndugulile.

Hivi karibuni zilisambaa video mbalimbali katika mitandao ya kijamii, zikimuonesha Mosses Mollel, maarufu kama Nabii namba saba, kwamba anao uwezo wa kutibu virusi vya Corona.

HAWA WACHUNGAJI NA MANABII WA DUNIA YA LEO MBONA WANA VISA HIVI?
 
Izo picha mbili mbona kama ni mtu mmoja, tofauti megapixel tu.
 
Mbona CCM inaahidi kila awamu kuwaondolea watanzania matatizo yao lakini inashindwa na hakuna anaewachukulia hatua.Akiwaambia nipeni mgonjwa mmoja nimtibu wataweza? Halafu tuache kubeza tiba za asili.
 
Back
Top Bottom