Serikali yamsaka Nabii Namba 7 anayejitangaza kuponya Corona

Serikali ya Tanzania imemuonya vikali mtu anayejiita Nabii Namba saba ambaye jina lake halisi ni Mosses Mollel kuwa itamchukulia hatua kali iwapo atashindwa kuthibitisha madai kuwa na uwezo wa kutibu virusi Vya ugonjwa wa Corona.

Nabii huyo ambaye taarifa zake zilianza kusambaa mwishoni mwa wiki iliyopita kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii akidai anayodawa ya kutibu ugonjwa hatari wa Corona ulioanzia nchini China na kusababisha Vifo Vya watu zaidi ya 1100 hadi sasa,ametakiwa kujisalimisha wizara ya afya na kuthibitisha taarifa hizo.

Akiongea na Vyombo Vya Habari jijini Arusha,Naibu Waziri wa Afya,Dkt Faustine Ndugulile ameeleza kuwa anazo taarifa za Nabii huyo kujitangaza kuwa anayodawa ya kutibu ugonjwa huo na kumtaka athibitishe kauli yake.

"Kimsingi nimeiona hiyo taarifa ya huyo mtu anayejiita Nabii Saba kuwa anayo dawa ya kutibu ugonjwa wa Corona ,ila hapa kwetu Tanzania hatuna maambukizi yoyote ya ugonjwa huyo ,tunachotaka huyo mtu atuthibitishie uwezo wake wa kutibu huyo ugonjwa wa Corona" Amesema Ndugulile.

Ameongeza kuwa iwapo atashindwa kuthibitisha atachukuliwa hatua Kali za kisheria.

Amesema hadi sasa Serikali imetuma wataalamu wake kwenda kumsaka na kumhoji kama anavyo vibali Vya kutoa huduma ya Tiba na kujitangaza kuwa anatoa Huduma ya kutibu ugonjwa huo hatari ambao hadi sasa mataifa bado yanahaha kusaka Tiba ya ugonjwa huo.

Nabii Namba Saba ambaye ni mkazi wa Ngaramtoni Wilayani Arumeru,Mkoani Arusha amekuwa akijitangaza kuwa anayo dawa ya kutibu ugonjwa huo wa corona na kuweka mawasiliano yake kwenye mitandao.

"Ninayodawa hapa Arusha ya kutibu virusi Vya Corona inayowaua Wachina na mataifa mengine. " sauti ya Nabii huyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
ANATAFUTA KICK TU. SURELY HAKUNA LOLOOOOOTEEEEE
 
Yeye ni mtumishi wa Mungu, na hoja zake zitajikita katika imani na maombi.
Ni vigumu sana kumwambia athibitishe kwani hizo dawa siyo tangible, na kwa sababu kwa sasa hakuna mgonjwawa corona Tanzania, wakicheza atawaambia wakamlete mgonjwa toka china ili amtibu, kitu ambacho serikali na wizara haitaweza.
MTUMISHI GANI WEWE!!! KHAAA!
 
Wangemsikiliza kwanza siyo kila kitu ni cha kupinga "let us pay attention and learn"...
 
Yeye ni mtumishi wa Mungu, na hoja zake zitajikita katika imani na maombi.
Ni vigumu sana kumwambia athibitishe kwani hizo dawa siyo tangible, na kwa sababu kwa sasa hakuna mgonjwawa corona Tanzania, wakicheza atawaambia wakamlete mgonjwa toka china ili amtibu, kitu ambacho serikali na wizara haitaweza.
Mkuu huyu Nabii uchwara amewezaje kutibu ugonjwa ambao haupo Tanzania? Uthibitisho kwamba mtu alipimwa akagundulika na Corona akamtibu uko wapi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mnamwonea bure kwasababu Wachina wanateketea na huo ugonjwa wa Corona bila tiba. Mbona wako wengi wanajitangaza wanatibu Ukimwi na Ukimwi hauna tiba unaangamiza Watanzania hamjawahi kuwakamata? Acha hizo! Kisa Corona inaangamiza Wachina ndo mnajishabadua? Acha Wachina waje Tanzania wapigwe hela ndefu tutajirike au wakamateni pia wale wanaosema wanatibu ukimwi!
 
Kwa hiyo anabishana na nabii? mbona kuna wale wengine walikandamiza kikombe cha babu mambo yao yapo swaafi kabisa na sasa kuna kukanyaga mafuta mambo yanaenda
 
Kwani ile dairekt flait ya Uchina ilyokuwa ikisemwa, haijaanza kazi bado!? Kama tayari, wamuweke tu ndani ya Mwewe akawatibie macho ndogo

Huu ungekua mwanya mzuri sana kwa nchi yetu kuanza kutambulika rasmi kama "dona kantre" naona hii nafasi tunaichezea.
 
Serikali ya Tanzania imemuonya vikali mtu anayejiita Nabii Namba saba ambaye jina lake halisi ni Mosses Mollel kuwa itamchukulia hatua kali iwapo atashindwa kuthibitisha madai kuwa na uwezo wa kutibu virusi Vya ugonjwa wa Corona.

Nabii huyo ambaye taarifa zake zilianza kusambaa mwishoni mwa wiki iliyopita kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii akidai anayodawa ya kutibu ugonjwa hatari wa Corona ulioanzia nchini China na kusababisha Vifo Vya watu zaidi ya 1100 hadi sasa,ametakiwa kujisalimisha wizara ya afya na kuthibitisha taarifa hizo.

Akiongea na Vyombo Vya Habari jijini Arusha,Naibu Waziri wa Afya,Dkt Faustine Ndugulile ameeleza kuwa anazo taarifa za Nabii huyo kujitangaza kuwa anayodawa ya kutibu ugonjwa huo na kumtaka athibitishe kauli yake.

"Kimsingi nimeiona hiyo taarifa ya huyo mtu anayejiita Nabii Saba kuwa anayo dawa ya kutibu ugonjwa wa Corona ,ila hapa kwetu Tanzania hatuna maambukizi yoyote ya ugonjwa huyo ,tunachotaka huyo mtu atuthibitishie uwezo wake wa kutibu huyo ugonjwa wa Corona" Amesema Ndugulile.

Ameongeza kuwa iwapo atashindwa kuthibitisha atachukuliwa hatua Kali za kisheria.

Amesema hadi sasa Serikali imetuma wataalamu wake kwenda kumsaka na kumhoji kama anavyo vibali Vya kutoa huduma ya Tiba na kujitangaza kuwa anatoa Huduma ya kutibu ugonjwa huo hatari ambao hadi sasa mataifa bado yanahaha kusaka Tiba ya ugonjwa huo.

Nabii Namba Saba ambaye ni mkazi wa Ngaramtoni Wilayani Arumeru,Mkoani Arusha amekuwa akijitangaza kuwa anayo dawa ya kutibu ugonjwa huo wa corona na kuweka mawasiliano yake kwenye mitandao.

"Ninayodawa hapa Arusha ya kutibu virusi Vya Corona inayowaua Wachina na mataifa mengine. " sauti ya Nabii huyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hawa wanaodai hadharani na mamia ya watu eti wanatibu kansa, ukimwi na tiba za mafuta, chumvi na maji mbona hatujaona wakithibitisha kwa kuwaweka kwenye hospitali za serikali. Kwanini baadhi ya watu wanaachwa wakiwahadaa wananchi lakini wengine wakitishiwa kukamatwa!
 
Mkuu huyu Nabii uchwara amewezaje kutibu ugonjwa ambao haupo Tanzania? Uthibitisho kwamba mtu alipimwa akagundulika na Corona akamtibu uko wapi?

Sent using Jamii Forums mobile app
Hoja ya hapa kwanini akamatwe huku wanaotibu kansa na ukimwi hawakamatwi au hawapelekwi kwenye hospitali za serikali kama wao walithibitisha, haki itendeke kwa wote.
 
Sasa atathibitishaje wakati ugonjwa wenyewe haupo hapa kwetu labda wamupeleke huko huko
 
Back
Top Bottom