mkarimani feki
JF-Expert Member
- Nov 8, 2023
- 302
- 1,212
Juzi nilimsikia Waziri wa Tamisemi akisisitiza watumishi wapya walipwe stahiki zao ikiwepo pesa ya kujikimu.
Mpaka sasa halmashauri kadhaa hazijafanya hivyo, najiuliza sana hayo matamko ya viongozi wana monitor vipi, kuhakikisha yanatekelezwa?
Imagine unaripoti Halmashauri X kutoka mkoa wako, nayo inakupangia kituo chako cha kazi takribani km 150 kutoka mjini. Nauli yako, hela ya chumba cha kupanga, chakula,mavazi, kusafirisha na kununua vitu vya ndani kama gesi na godoro juu yako mwenyewe!
Vitu viko juu nauli nayo sio mchezo, serikali kuu chunguzeni hali ya watumishi huko halmashauri! wakurugenzi hawatoi hela ya kujikimu, hali ni mbaya tunaishia kulala kwa wanakijiji.