Serikali yapandisha bei ya zao la Cacao mpaka Tzs 5015 kwa kilo

Unapandishia watu tozo za simu ,mbolea ,mafuta halafu kwa ajili ya propaganda unasema bei ya cocoa imepanda ,zao inayolimwa na 0.2 % ya watanzania .Kama ana uwezo apandishe bei ya mahindi yanayouzwa Tanzania nzima
 
Aina hii ya Watanzania mnaturudisha nyuma sana kwakweli.

Hivi unaelewa hata ABCs za economics mkuu? Ni factor gani zinasababisha kupanda kwa bei ya bidhaa/raw materials?

Ni rais anapandisha bei?


Hizo factors zote zilikuwa zimamsuniri Samia? Acheni roho mbaya Mama kayapatia mambo kirahisi sana
 
Huyu Mama anakibali cha Mungu Case Closed,
Watu wa rohoni watanielewa,
Mimi nitamchagua 2025 tuombe uzima,
 
Unavyojaribu kumaanisha ni kama vile kila mtanzania ni mkulima wa 'kakao'. Mimi niliejariwa naona naumia tu kuanzia bei ya mafuta mpaka matozo ya kila kukicha. Sasa kama kipimo cha muelekeo wa mama ni kakao basi na aende mwenyewe tu.
 

ongezeko la tozo gesi mbolea hayo huoni ccm akili sijui mlipelekaga wapi??
 
Hakika....😍

Kazi Iendelee tu....

KONGOLE KWAKE CHIFU MKUU HANGAYA 🙏
 
Aina hii ya Watanzania mnaturudisha nyuma sana kwakweli.

Hivi unaelewa hata ABCs za economics mkuu? Ni factor gani zinasababisha kupanda kwa bei ya bidhaa/raw materials?

Ni rais anapandisha bei?


Sera anazozisimamia yeye, Ndio maana huyu miezi sita tu bei iko hapa,
 
😍
 
Watanzania tuna ushabiki wa kutisha, mpaka tunazuzuka. Bei ya mazao yote huamuliwa na mlaji, serikali ni 'speaker' tu. Tena 'speaker' iliowekwa sauti ya juu kabisa. Na ni ya njia moja, kuongea yale sisi wananchi yanatufurahisha. Siku soko la dunia bei ikiporomoka wananchi wakapiga kelele, sauti hupunguzwa na kusikika 'itaundwa tume kujadiliana na wanunuzi'.
 
Kapandishaje?

Yeye binafsi amefanya kitu gani hadi bei imepanda?
Apandishe na mahindi kama anao huo uwezo.
Wakulima wa mahindi wanasaga meno kwe bei ndogo ya mahindi.
Wanasiasa ni wajinga na wapumbavu. Leo hii hakuna kiongozi asimamae jukwaani kubwabwaja uongo wake bila kumtaja 'mama'. Kuongoza nchi si kama kulima mchicha. Kusema 'mama' kafanya hili au lile ni uhuni mkubwa. Bora hata wasemao hajafanya hili au lile, kwa sababu mwanzo hubashiri mwisho.
 
Hujui unachoongea
Hajui, huyo ni shabiki kindakindaki. Kesho atakuja na agenda ya mama kutawazwa kuwa mkuu wa watemi Tanzania nzima. Utemi ni kushabikia ukabila. Yale yale ya hayati Magufuli kuhutubia kisukuma tv ya taifa.
 
Huyu Mama anakibali cha Mungu Case Closed,
Watu wa rohoni watanielewa,
Mimi nitamchagua 2025 tuombe uzima,
Hujazuiwa, na wenzio wa aina yako wapo kibao. Ambao saa nne asubuhi yupo bado kitandani akiulizwa kwa nini hajaamka anajibu bado amelala.
 
Kapandishaje?

Yeye binafsi amefanya kitu gani hadi bei imepanda?
Apandishe na mahindi kama anao huo uwezo.
Wakulima wa mahindi wanasaga meno kwe bei ndogo ya mahindi.
Mwendazake alipowatingishia kiberiti Wakenya kwa kuzuia mahindi kuingia Kenya, ilibidi Kenya igeukie Brazili kuagiza mahindi jambo ambalo walikua ni nadra kufanya. Kenya ilitegemea sana Tanzania kwa mahindi ili kupeleka SOMALIA, SUDAN NA ETHIOPIA. Asili mia kubwa ya mahindi ya TZ yakiwepo ya kusini yaliuzwa Kenya na bei ilikua mpaka 120000shs gunia la kg 100. Ikushuka sana shs 80000. Walipoleta mahindi ya Brazil wakatuuzia Watanzania gunia elfu thelathini na huo ukawa ndio mwanzo wa kuporomoka soko la mahindi hadi leo. Waswahili husema ukila na kipofu usimshike mkono.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…