Unataka madalali wakale wapi? Mna ajira za kuwaajiri huko serikalini?
Haiwezekani mtu atafute connection za wanunuzi huko South Sudan,Kenya,Congo au Uganda kisha akuletee wewe pesa shambani kwako bila ya yeye kunufaika kwa chochote.
Tembea ulimwengu mzima ,huwezi kumuondoa dalali katika chain ya biashara . Hakuna boss atakayesumbuka kutoka DRC au south Sudan kuja kufata mahindi yako huko kijijini mbigili, mbugani!!! Dalali wake ndie atakayefanya kazi ya kumkusanyia mazao na kumpakilia kwenye malori ili aupokee mzigo nchini kwake .