Serikali yapiga marufuku kununua mazao shambani, yaagiza maghala yote kusajiliwa

Serikali yapiga marufuku kununua mazao shambani, yaagiza maghala yote kusajiliwa

Kurasimishwa sio kuondolewa. Sajili biashara ya ununuzi na uuzaji wa mazao serikali ipate, wewe upate, mkulima apate.

Sasa hivi wewe unapata, mkulima anapata kidogo sababu unamlalia, serikali haipati kabisa kutoka kwako maana umekaa hapo katikati hujulikani ila upo.
FYI hakuna watu wanalipa kodi hapa TZ kama wafanyabiashara wachuuzi wa mazao!! Fikiria trip moja tu nikipakia mahindi tani 30 nalipa zaidi ya sh 900k kama kodi bado hapo maushuru mengine ya sokoni!! Kwa mwezi nikizungusha trip 5 tu tayari nishaiachia serikali zaidi ya 4M...piga kwa mwaka serikali inachukua kiasi gani
 
Ok, Mkuu, kwani kurasimishwa na kuendelea kulipa kodi kuna tatizo?
 
Wapi waliposema Serikali imepiga marufuku kuuza mahindi Nje ya Nchi?
Mkulima ndio anaesaidiwa,yakiuzwa sehemu ambayo inatambulika , Serikali itakusanya pesa na bei itakuwa nzuri..

Mwisho Maghala yatakuwa yanatoa taarifa za kiwango Cha mazao waliyonayo hivyo Serikali itakuwa na makadirio sahihi ya uzalishaji nk..
Uko sawa mkuu, Tanzania hatuna taarifa sahihi za mazao mana mkulima hatunzi kumbukumbu LAKINI pia kodi hailipwi kisahihi. Tatu mkulima hajui bei shindani mana bishara hizi zinafanyika kwa siri, n rahisi mfanyabiashara kutumia lugha kuwa jana tumenunua kg moja kwa tsh 500 tu kijiji cha pili hapo
 
Kulikuwa na soko la Kundemiti wakati fulani.
Wakulima walikuwa wanauza Kunde zao kwa bei nzuri tu.

Mala Serikali ikaingilia kati na kutaka wanunuzi wawe na maghala yaliyosajiriwa.

Toka tamko lile litolewe biashara ya kundemiti ikafa jamla hadi leo.

Haya matamko ya kusajiri maghala yanatolewa kwa vitisho kwa wanunuzi mazao.
Ni matamko yasiyo rafiki kwa mkulima.
Kama hawataki watu wanunue mazao basi inunue Serikali ili wafanya biashara wanunue serikalini.

Mkulima ana hiari ya kuuza mazao yake popote na kwa yeyote. Ili asomeshe watoto wake.
Hii nchi ni kama huwa ina laana
 
Serikali imepiga marufuku Wanunuzi kwenda Kununua Mazao ya Wakulima mashambani na kuagiza mazao yote yanunuliwe kwema Maghala yaliyosajiliwa.

My Take: Wenye Stoo na madalali Sasa kazi mnayo..

========

Wizara ya kilimo Tanzania imetoa taarifa kwa umma kuhusu utaratibu wa kuuza, kununua na kurasimisha biashara za mazao nchini ambapo moja ya taratibu ni wafanyabiashara wa mazao kusajili maghala yote binafsi, ya serikali na ushirika na kutoa taarifa za mauzo ya mazao ghalani.

😆😆😆 Wakunya wameanza kulia lia
Wakanunue GMO mbwa hao
Screenshot_20230529-135940.jpg
 
Serikali imepiga marufuku Wanunuzi kwenda Kununua Mazao ya Wakulima mashambani na kuagiza mazao yote yanunuliwe kwema Maghala yaliyosajiliwa.

My Take: Wenye Stoo na madalali Sasa kazi mnayo..

========

Wizara ya kilimo Tanzania imetoa taarifa kwa umma kuhusu utaratibu wa kuuza, kununua na kurasimisha biashara za mazao nchini ambapo moja ya taratibu ni wafanyabiashara wa mazao kusajili maghala yote binafsi, ya serikali na ushirika na kutoa taarifa za mauzo ya mazao ghalani.

Too late.
 
Back
Top Bottom