Serikali yapiga marufuku kununua mazao shambani, yaagiza maghala yote kusajiliwa

Sio kweli. Mkukima asijue ghala liko wapi? Atakuwa mkukima wa wapi huyo. Acha hoja za mkato mkato. Kwa mbinu hii mkukima anaweza kunufaika sana kwa kupeleka mazao yake kwenye ghala atakatoa linatoa bei nzuri.
Nitajie maghala angalau 10 nchi nzima yaliyosajiliwa na yanatumika kama masoko ya mazao ndugu. Nipo hapa nakungoja!
 
Serikali wajanja sana,mwaka huu biashara ya Mahindi iko moto sana,Serikali inaweza usipate Mahindi ya kununua kutoka kwa Wakulima,sasa nadhani mbinu hii itapunguza kasi.
 
Uko sahihi Kabisa mkuu.
 
Hili nakataa, mkulima auze mazao yake pale na popote anapotakaaa, hii serikali haijui wakulima wanapitia nn ktk maisha yao ya kila siku.

Wawaachee kabisaaa.
 
Sio kweli. Mkukima asijue ghala liko wapi? Atakuwa mkukima wa wapi huyo. Acha hoja za mkato mkato. Kwa mbinu hii mkukima anaweza kunufaika sana kwa kupeleka mazao yake kwenye ghala atakatoa linatoa bei nzuri.
Wapii huko kuna maghala? Au unasemea magodauni ya vitengo? Wakulima hawataki hata kusikia walidhurumiwa mnoo mwaka juzii.

Wakulimaaa waachwee wauze mazao watakavyoo.
 
Shida zangu, mazao yangu, unipangie lini na wapi pa kuuza[emoji848][emoji848][emoji848]
 
Nitajie maghala angalau 10 nchi nzima yaliyosajiliwa na yanatumika kama masoko ya mazao ndugu. Nipo hapa nakungoja!
Labda anasemea magodauni ya mazao Yale ya vitengo kwa kila kata, wakulima hawataki hata kuyasikia.

Walidhurumiwa mnoo mwaka juzi.
 
Kwani serikali imemsaidia nini mkulima mpaka kwenye kuuza ianze kumpangia masharti?!

Biashara ni mapatano! Iachwe mkulima aamue nani wa kumuuzia na kwa muda gani! Haiwezekani mtu akope pesa, ajitume kulima mwenyewe kisha wakati wa mavuno umwambie apeleke mazao yake kwenye maghala ya serikali!!

Hapa ndio mwanzo wa mkulima kuanza kuambiwa alipe kodi TRA kwa mtonyo aliyouingiza mara baada ya kuuza mazao yake.

Kama humsaidii mkulima kwa chochote kile basi usimpangie wapi pa kuuza na nani wa kumuuzia. Haiwezekani mnunuzi anifate shambani na pesa Cash halafu nimgomee kumuuzia mazao yangu.
 
Hapa imewalenga madalali wanaoingiza Millions just kwa kununua kwa niaba ya mfanya biashara. Ni kama vile kwa mlango wa nyuma inataka kuwarasimisha.
Unataka madalali wakale wapi? Mna ajira za kuwaajiri huko serikalini?

Haiwezekani mtu atafute connection za wanunuzi huko South Sudan,Kenya,Congo au Uganda kisha akuletee wewe pesa shambani kwako bila ya yeye kunufaika kwa chochote.

Tembea ulimwengu mzima ,huwezi kumuondoa dalali katika chain ya biashara . Hakuna boss atakayesumbuka kutoka DRC au south Sudan kuja kufata mahindi yako huko kijijini mbigili, mbugani!!! Dalali wake ndie atakayefanya kazi ya kumkusanyia mazao na kumpakilia kwenye malori ili aupokee mzigo nchini kwake .
 
Kurasimishwa sio kuondolewa. Sajili biashara ya ununuzi na uuzaji wa mazao serikali ipate, wewe upate, mkulima apate.

Sasa hivi wewe unapata, mkulima anapata kidogo sababu unamlalia, serikali haipati kabisa kutoka kwako maana umekaa hapo katikati hujulikani ila upo.
 
Kwenye biashara hakuna kitu kinaitwa kulalia bali kuna negotiation na bargaining!!

Mkulima anapokubali kuuza ina maana ameridhika na bei laa sivyo ana uhuru wa kukataa bei. Tatizo lenu mnataka mtu aje akupe mamilioni ya pesa halafu yeye akale hasara sokoni!!
 
Sawa. Rasimishwa ili negotiation iwe rasmi. Kwani kuna tatizo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…