Serikali yapiga marufuku mazao ya uhandisijeni(GMOs) nchini

Genetically Modified organism (People) akila Genetically Modified Organism (Food), matokeo yake yatakuwa balaa
 
Kwa hili kwa hakika naipongeza sana serikali, hiki kilikuwa kinakwenda kuwa kifo cha mende kwa wakulima. Ingebidi wawe wananunua mbegu kila msimu wa kilimo na kwa wakulima wa kujikimu isingewezekana kamwe. Ilikuwa ni kuwaingiza wakulima wadogo na wa kati kwenye umaskini kwa hakika. Pia tunahitaji na teknolojia zaidi kufanya kilimo hiki.
 
MOSANTO ko nyuma ya hii kadhia ya hii teknolojia maana wanataka waue mbegu zetu za asili ambazo unaweza kuvuna na kupanda tena... Watuletee mbegu ambazo ukivuna huwezi kupanda tena maana yake unakua mtegemezi wa mbegu kutoka hayo makamupuni FOREVER .
Pia mbegu hizi zinaua ardhi na kuifanya kua tegemezi kwa madawa na mbolea
 
Mmh we mjomba umechanganya madesa hapo, huelewi hata GMO's ni nini, unachanganya na mbegu za kisasa, ni bora ungekaa kimya! Pole
 
Mkuu ningekushauri kasome kwa taratibu na uzuri zaidi kuhusu GMO ndo uandike hayo uliyoandika. Nani kakwambia wazungu wote wanatumia vyakula vya GMO? Unajua nchi nyingi tu zilizoendelea zimeikataa? usichanganye GMO na teknolojia zingine za kilimo
 
Umenena vyema sana mkuu, kwa wenye uelewa japo kidogo wanajua sana madhara yake. Nchi nyingi tu za ulaya walikataa tangu mwanzo pamoja na MONSANTO kufanya kampeni ya nguvu. Mwisho kahamia Africa anakojua kuna jingalala wengi. Kiufupi umenimaliza ya kuandika
 
Mwenye madhara ya GMO anijuze ili nami nikatae au nikubali. Kwa sasa nipo kama bendela tu.
 
Kwa hili naipongeza sana serikali, GMO mazao yake ni hatari kwa afya ya binadamu, ardhi na mimea mingine, Europe na Asia wanasisitiza GMO kwasababu ardhi waliyonayo ni kidogo na watu ni wengi.
 
Hata haujui unaongea nini,
It’s important that we develop drought-tolerant varieties to ensure food security, said Dr. Kingstone Mashingaidze, a scientist with the National Agricultural Research Council of South Africa.
Under a royalty-free licensing agreement, seed companies in Tanzania, Kenya, South Africa and Uganda are already growing and selling drought-tolerant maize hybrids developed by WEMA to suit local conditions and branded as DroughtTEGOTM. Mozambique will introduce the TEGO brand seeds this year. The WEMA project has received commercial release approvals for more than 60 TEGO conventional hybrids across the five countries.
The TEGO hybrids caught on quickly as farmers growing the less-productive open-pollinated varieties saw their hybrid-cultivating neighbors reaping bigger harvests.
Haujui unaongea nini, genetic ni vinasaba vinachanganywa kwa kuleta ubora wa uzalishaji na kuvumilia ukame. Hiyo mbegu inakuwa na hizo sifa , ukija kuipanda tena inajitenganisha kwa huyo haupati ile combination. Unapochagua dume la ng'ombe lenye ubora ukatafuta na jike lenye sifa ya kutoa maziwa mtoto atakaezaliwa atakuwa na sifa za hao wazazi wake hapo na wewe umefanya Genetic modification . Soma Mendel's laws of inheritance
 
KWA MARA YA KWANZA IN A VEEEERY LONG TIME NAOMBA NIIPONGEZE SERIKALI KWA HILI, SAFI SANA
 
MOSANTO ko nyuma ya hii kadhia ya hii teknolojia maana wanataka waue mbegu zetu za asili ambazo unaweza kuvuna na kupanda tena... Watuletee mbegu ambazo ukivuna huwezi kupanda tena maana yake unakua mtegemezi wa mbegu kutoka hayo makamupuni FOREVER .
Pia mbegu hizi zinaua ardhi na kuifanya kua tegemezi kwa madawa na mbolea
 
Watu wanafikiria quantity badala ya quality, ila GMO haifai inatuuwa kwa magonjwa,
 
Na wakina bill gates wanasisitiza sana watu watumie hizo GMO's
 
hizo mbegu za GMO sio nzuri sana kuzituma maana baada ya miaka kadhaa tutajikuta totally dependent on them na hapo mbegu za asili unazoweza kupanda miaka na miaka hazitakuwepo tena, hizo za GMO ukishapanda msimu mmoja utavuna basi unauza mazao yote, ukijifanya uache kidogo kama mbegu ya msimu ujao haupati mazao bora. In short hizo zipo kibiashara zaidi.
 
Hii mada itavamiwa na wapingaji wengi wanaosaport GMO kumbuka haya mashirika yametoa hela. Nyingi sana na rushwa ili miradi yao isipingwe na ipitishwe na serekali mbali mbali!! So tutarajie supporters wengi kuja kutetea GMO kwa maslahi ya matupmbo yao sio afya za walaji na ustawi wa jamii
 
Ina maana mbegu za mahindi wanazotumia wakulima nowdays nazo ni gmo?

Mbona niliskia wanaziita hybrid/chotara

Nazo ukizipanda mara ya pili hazioti
Mkuu hybrid/chotara si GMO ni cross breeding ya mmea kupata tabia fulani unazozitaka k.v mazao mengi, kuvumilia ukame, kuzaa kwa muda mfupi n.k., off course ukizipanda zinaota vizuri sana hili mazao yanapungua kila unapoendelea kuzitumiatu but zinota. GMO ni teknolojia nyingine kabisa ya kucheza na genes za mimea. na mbegu zake ukizipanda hazioti lazima ununue toka kwa mzalishaji kwa maisha yako yote.
 
umeongea pumba halafu umetaka uonekane umeongea point hivi vitu si vya kukurupuka tafuta mada ya umbeya uchangie,pumbaaaaaaaaaaa mpk unakera
 
Wewe ni muuzaji nini wa hizo mbegu maana umenikemea kwelikweli lakini bado haiondoi ukweli kuwa hizo mbegu siyo salama hata kidogo mkuu
 
Kuna wateteI wengi sana wa hizo mbegu nawanakuja na facts ili mradi tu watuteke!! Hapa kuna kila dalili ya kufanywa wategemezi FOREVER
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…