Serikali yapunguza riba ya mikopo

Serikali yapunguza riba ya mikopo

Mkuu Nyabukika, hili ni jambo jema, kwa maendeleo ya taifa na litasaidia sana wananchi, ila sasa naomba usilete siasa za uchawa katika hili kuwa 2025 atashinda kwa kishindo, huu uchawa uta waterdown nia njema na nia nzuri ya Mama kwenye hili la kushusha riba likaonekana ni kwa ajili 2025
P
Hata leo ukiwnda CRDB au NMB riba ni 17% sasa watuambie hiyo 11 ilikiwa inakatwa bank gani
 
Ni benki gani inatoa mikopo? Lini ilitoa mikopo? Masharti milioni ya kupata mkopo lazima uwe tajiri , uwe na hati ya nyumba, leseni ya bizness , risiti za mapato , uwe na akaunti benki unaijaza mapesa kila siku kwa miaka mitatu , uwe na jina la kihindi, kufuatilia mkopo ni miaka miwili au zaidi na kuna pesa ya afisa mikopo yaani lazima kwanza uwe bwanyenye .
Kiufupi mikopo si ya watu maskini!wanaboa sana kuizungumzia kama vile watu maskini wanapewa tu. Wamuogope Mungu.
Hebu kwanza watutajie majina ya wanufaika kama sio wahindi watupu. Watuoneshe maskini 5 tu waliopewa mikopo!
Mi stori zisizo na uhalisia za Nyerere kuwafanya watu wote ni wajinga (farasi) huwa napita tu!
Stori kama hizi zinaboa sana , zinakera masikioni na kuhamasisha wajanja kusaka Green card (deadline imepita)!

Kupata mkopo lazima uwe tajiri? Hiyo sherianimeandikwa wapi? Most of the time wanaochukua si matajiri
 
Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu iliahidi kumuinua mwananchi kiuchumi na sasa imekuja na punguza ya riba ya mikopo ya mtu binafsi

Benki Kuu ya Tanzania imetangaza kushusha riba ya mikopo binafsi kutoka asilimia kati ya 11 na 13 hadi asilimia 9.

Hatua hii inafuatia mwongozo wa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu kuongeza upatikanaji wa mitaji ya biashara kwa riba nafuu kwa kila mtu mwenye sifa.

Rais Samia Suluhu anaendelea kuteka mioyo ya watanzania walio wengi kwa jitihada hizi za kuinua uchumia wa mtanzania kwa maendeleo haya 2025 Rais Samia Suluhu atashinda kwa kishindo
Uandishi wa kichawa huu!!
 
Unamwamini samia. Nenda bank kama utakuta hiyo riba
 
Wananchi tunataka tuambiwe hiyo riba imeshushwa kwenye benki zipi?

Maana Watanzania bado wanaendelea kuumizwa kutokana na uwepo wa riba kubwa na zisizo rafiki kwenye mikopo ya hizo taasisi za kifedha; zikiwemo benki.
Huku mtaani wasisahau Kuna nyonya dam laki Kwa laki na hamsin 150000
 
Angekuwepo JPM utekelezaji ungeanza DECEMBER hii 2022
 
Back
Top Bottom