Huu mfuko wa Global Fund ulianzishwa mwakanl 2002 na Koffi Annan akiwa SG wa Umoja wa Mataifa. Ni mfuko ulioanzishwa kukabiliana na magonjwa ya UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaria katika nchi za Africa, Asia na South America.
Kabla ya Mfuko huu wagonjwa walikuwa wanashindwa ku afford matibabu hasa ya UKIMWI kwa kuwa bei dozi ya mwezi mmoja ilikuwa inakaribia Tsh 300,000. Hivyo basi ni watu wengi hasa wa Third World waliokufa kwa ugonjwa wa UKIMWI.
Vyanzo vya mfuko huu ni michango ya fedha kama msaada kutoka nchi za USA, United Kingdom, Sweden, Canada, EU na makampuni makubwa kama Cocacola, Gates Foundation, etc
Misaada hii huyolewa kwa nchi ambazo zinakidhi vigezo na siyo mkopo.
Kuhusu ku-miuse hela za mfuko huu siyo rahisi kwa kuwa wasimamizi wa fedha hizi ni makampuni makubwa ya ukaguzi wa mahesabu. Kwa Tanzania zinakaguliwa na PWC