Serikali yasaini mkataba ujenzi Daraja la Jangwani, Sh Bilioni 97.1 kutumika

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
WhatsApp Image 2024-10-22 at 17.05.30_89c50577.jpg

WhatsApp Image 2024-10-22 at 17.05.31_bd1da7b2.jpg

Serikali imesaini mkataba wa ujenzi wa Daraja la Jangwani lenye urefu wa mita 390 na barabara za maungio zenye urefu wa mita 700 katika barabara ya Fire - Ubungo kwa gharama ya Shilingi Bilioni 97.1 ambapo kazi ya ujenzi itatekelezwa kwa miezi 24.

Mkataba huo umesainiwa leo Oktoba 22, 2024 Mkoani Dar es Salaam kati ya Wakala ya Barabara (TANROADS) na Mkandarasi wa Kampuni ya China Communications Construction Company Limited na kushuhudiwa na Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa na viongozi wengine.

Akizungumza baada ya kushuhudia utiaji saini huo, Waziri Bashungwa ameeleza kuwa ujenzi wa daraja hilo utaondoa kero kwa wananchi na adha ya usafiri kutokana na eneo hilo kujaa maji mara kwa mara na kusababisha barabara kufungwa na kutopitika mvua zinaponyesha.

Bashungwa amemuelekeza Mkandarasi huyo kukamilisha maandalizi na kupeleka vifaa na mitambo ndani ya miezi mitatu katika eneo la Jangwani ili kazi iweze kuanza na kuhakikisha anajenga haraka kwa mujibu wa usanifu na mkataba kama ilivyopangwa.
WhatsApp Image 2024-10-22 at 17.05.27_c2dc6e9d.jpg

WhatsApp Image 2024-10-22 at 17.05.28_b1c6d4f6.jpg
Aidha, Bashungwa ameeleza kuwa ujenzi wa daraja hilo utaenda sambamba na ujenzi wa kingo za Mto Msimbazi ambao utatekelezwa na Ofisi ya Rais - TAMISEMI ikiwa ni katika programu ya uendelezaji wa Bonde la Msimbazi.

Bashungwa amebainisha kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa shilingi Bilioni 125 kwa ajili ya kurejesha miundombinu katika Mkoa wa Dar es Salaam iliyoathiriwa na mvua za El-Nino ikiwa ni pamoja na ujenzi wa daraja la Kigogo, daraja la Mpiji chini, daraja la Mtongani, daraja la Mkwajuni, daraja la Mzinga, daraja la Nguva na box kalavati la Mikadi, daraja la JKT – Ununio, daraja la Kisarawe, Amani, Gomvu, Geti jeusi, mifereji ya maji Kigamboni – Kibada na maeneo mengine.

Akitoa taarifa ya mradi, Mtendaji Mkuu wa TANROADS, Mhandisi Mohamed Besta ameeleza kuwa mkandarasi aliyeshinda zabuni ya ujenzi ni kampuni ya China Communications Construction Company Limited na kusimamiwa na kampuni ya Leporogo Specialist Engineers ya Afrika Kusini ikishirikiana na Afrisa Consulting Ltd ya Tanzania na Dong Myeong Engineering Consultants & Architecture Co. Ltd ya Korea Kusini.

Naye, Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Jimbo la Ilala, Mussa Hassan Zungu ameeleza kuwa utekelezaji wa ujenzi wa daraja la Jangwani ni matokeo ya 4R za Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila amemshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweka historia ya kuanza kutekeleza ujenzi wa daraja la Jangwani.

Mradi wa Ujenzi wa Daraja la Jangwani ni moja ya mikakati ya Serikali ya kuharakisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii Mkoani Dar es Salaam kwa kuboresha barabara ili kuongeza ufanisi katika sekta ya Usafiri.
WhatsApp Image 2024-10-22 at 17.05.31_a9b6d6bf.jpg

WhatsApp Image 2024-10-22 at 17.05.31_59233b9b.jpg
Pia soma ~ Barabara ya Kilwa kipande cha Mbagala Mzinga kuja Kongowe mpaka Kisemvule iboreshwe kabla ya kuleta maafa
 
good move…ila sasa ngoja waje wale wanaobubujikwaa na machozi watavyotusagia kunguni
Uamuzi wa kijinga kabisa. Uamuzi mzuri ungekuwa ni kujenga Dar mpya maeneo ya Bagamoyo na hii ya sasa ibaki kama ilivyo. Nasema hivi kwa sababu gharama za kurekebisha uharibifu amabo umeshafanywa na kulifanya jiji lipangike ni kubwa kulinganisha na huu ujinga wanaofanya.
 
Serikali imesaini mkataba wa ujenzi wa Daraja la Jangwani lenye urefu wa mita 390 na barabara za maungio zenye urefu wa mita 700 katika barabara ya Fire - Ubungo kwa gharama ya Shilingi Bilioni 97.1 ambapo kazi ya ujenzi itatekelezwa kwa miezi 24.

Mkataba huo umesainiwa leo Oktoba 22, 2024 Mkoani Dar es Salaam kati ya Wakala ya Barabara (TANROADS) na Mkandarasi wa Kampuni ya China Communications Construction Company Limited na kushuhudiwa na Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa na viongozi wengine.

Akizungumza baada ya kushuhudia utiaji saini huo, Waziri Bashungwa ameeleza kuwa ujenzi wa daraja hilo utaondoa kero kwa wananchi na adha ya usafiri kutokana na eneo hilo kujaa maji mara kwa mara na kusababisha barabara kufungwa na kutopitika mvua zinaponyesha.

Bashungwa amemuelekeza Mkandarasi huyo kukamilisha maandalizi na kupeleka vifaa na mitambo ndani ya miezi mitatu katika eneo la Jangwani ili kazi iweze kuanza na kuhakikisha anajenga haraka kwa mujibu wa usanifu na mkataba kama ilivyopangwa.
Aidha, Bashungwa ameeleza kuwa ujenzi wa daraja hilo utaenda sambamba na ujenzi wa kingo za Mto Msimbazi ambao utatekelezwa na Ofisi ya Rais - TAMISEMI ikiwa ni katika programu ya uendelezaji wa Bonde la Msimbazi.

Bashungwa amebainisha kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa shilingi Bilioni 125 kwa ajili ya kurejesha miundombinu katika Mkoa wa Dar es Salaam iliyoathiriwa na mvua za El-Nino ikiwa ni pamoja na ujenzi wa daraja la Kigogo, daraja la Mpiji chini, daraja la Mtongani, daraja la Mkwajuni, daraja la Mzinga, daraja la Nguva na box kalavati la Mikadi, daraja la JKT – Ununio, daraja la Kisarawe, Amani, Gomvu, Geti jeusi, mifereji ya maji Kigamboni – Kibada na maeneo mengine.

Akitoa taarifa ya mradi, Mtendaji Mkuu wa TANROADS, Mhandisi Mohamed Besta ameeleza kuwa mkandarasi aliyeshinda zabuni ya ujenzi ni kampuni ya China Communications Construction Company Limited na kusimamiwa na kampuni ya Leporogo Specialist Engineers ya Afrika Kusini ikishirikiana na Afrisa Consulting Ltd ya Tanzania na Dong Myeong Engineering Consultants & Architecture Co. Ltd ya Korea Kusini.

Naye, Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Jimbo la Ilala, Mussa Hassan Zungu ameeleza kuwa utekelezaji wa ujenzi wa daraja la Jangwani ni matokeo ya 4R za Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila amemshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweka historia ya kuanza kutekeleza ujenzi wa daraja la Jangwani.

Mradi wa Ujenzi wa Daraja la Jangwani ni moja ya mikakati ya Serikali ya kuharakisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii Mkoani Dar es Salaam kwa kuboresha barabara ili kuongeza ufanisi katika sekta ya Usafiri.
Pia soma ~ Barabara ya Kilwa kipande cha Mbagala Mzinga kuja Kongowe mpaka Kisemvule iboreshwe kabla ya kuleta maafa
Hivi wame shindwa kupata mkandarasi wa ndani anae jua hilo eneo vizuri zaidi hizo shilling bn 97 zibaki hapa hapa nchini,........college of civi Engineering Udsm haina product wa kujenga hilo daraja la robo kilomiter kweli?
 
Ukweli ni kwamba hautaki kuwapatia kazi wakandarasi wa ndani. Mbona taifa gesi wanaweza Sana. Kuna shida kwenye uhongozi.
 
Uamuzi wa kijinga kabisa. Uamuzi mzuri ungekuwa ni kujenga Dar mpya maeneo ya Bagamoyo na hii ya sasa ibaki kama ilivyo. Nasema hivi kwa sababu gharama za kurekebisha uharibifu amabo umeshafanywa na kulifanya jiji lipangike ni kubwa kulinganisha na huu ujinga wanaofanya.
Hapana haupo Sawa , Ile ni barabara kubwa inayoingia city centre ambako ndio kuna kitovu cha biashara so Kwa namna yoyote Ile Daraja Bora litakalo weza kutatoa Kero ya mafuriko hapo jangwani linahitajika , cause mafuriko yanapokuwa yanatokea Kwa namna Moja au nyingine uchumi nao Una stuck

Ni kweli kuna makosa makubwa yalifanyika hapo awali ambayo ni kujenga sending ya mwendokasi pale jangwani but tukubali tukatae mabadiliko yanahitajika
 
Tatizo kubwa nikukosa uzalendo na kuweka rushwa au percentage yao katika huo mradi, wsbongo wanawasema wakishindwa kugawana, ila mchina ata ahidiwa watu mradi mgine tu.
 
Hapana haupo Sawa , Ile ni barabara kubwa inayoingia city centre ambako ndio kuna kitovu cha biashara so Kwa namna yoyote Ile Daraja Bora litakalo weza kutatoa Kero ya mafuriko hapo jangwani linahitajika , cause mafuriko yanapokuwa yanatokea Kwa namna Moja au nyingine uchumi nao Una stuck

Ni kweli kuna makosa makubwa yalifanyika hapo awali ambayo ni kujenga sending ya mwendokasi pale jangwani but tukubali tukatae mabadiliko yanahitajika
Umeelewa nilichoandika? Ni hivi. Kulikuwepo na mpango wa muda mrefu (zamani) wa ''kuhamisha'' jiji kwenda maeneo ya Bagamoyo ili kupunguza msongamano. Automatically hili lingefanya kusiwepo na hayo ''makosa'' (mimi nasema uzembe wa hali ya juu) wa kujenga stend ya mwendokasi na vitu vingine vingi ambavyo vimeshafanyika na sasa hivi huwezi kurudi tena nyuma.
 
Daraja lijengwe na huo mpango wako inaousema ufanyike
 
Uamuzi wa kijinga kabisa. Uamuzi mzuri ungekuwa ni kujenga Dar mpya maeneo ya Bagamoyo na hii ya sasa ibaki kama ilivyo. Nasema hivi kwa sababu gharama za kurekebisha uharibifu amabo umeshafanywa na kulifanya jiji lipangike ni kubwa kulinganisha na huu ujinga wanaofanya.
Uamuzi wa busara kwasababu hata ukisema ujenge dar mpya watu hawataacha kupita jangwani.
 
Umeelewa nilichoandika? Ni hivi. Kulikuwepo na mpango wa muda mrefu (zamani) wa ''kuhamisha'' jiji kwenda maeneo ya Bagamoyo ili kupunguza msongamano. Automatically hili lingefanya kusiwepo na hayo ''makosa'' (mimi nasema uzembe wa hali ya juu) wa kujenga stend ya mwendokasi na vitu vingine vingi ambavyo vimeshafanyika na sasa hivi huwezi kurudi tena nyuma.
Mji mkuu umehamishiwa Dodoma, inatosha. Kuhamishia Jiji Bagamoyo unamaansiha wananchi wa Dar tupelekwe Bagamoyo au unamaanisha nini?
 
Uamuzi wa busara kwasababu hata ukisema ujenge dar mpya watu hawataacha kupita jangwani.
Jangwani mbona imeharibiwa na CCM? Ingekuwa ni serikali ya watu wenye busara tatizo la hapo lingeshaisha siku nyingi tena kwa gharama ndogo
 
Back
Top Bottom